Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 18.08.23
Mshambulizi wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, amewaambia wasaidizi wake kuwa atasalia PSG mwaka huu lakini mwaka 2024 anataka tu kuchezea Real Madrid. (El Chiringuito TV – In Spanish)
Chelsea wamemuongeza mshambuliaji wa Nottingham Forest na Wales Brennan Johnson kwenye orodha ya washambuliaji na wamefanya mazungumzo ya awali na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Guardian)
Forest wameweka dau la pauni milioni 40 kwa Johnson, huku Tottenham na Brentford pia wakifikiria kumnunua mshambuliaji huyo kabla ya dirisha kufungwa. (Independent)
Chelsea wameulizia kuhusu winga wa Rennes wa Ubelgiji Jeremy Doku, 21, baada ya uhamisho wao wa kumnunua Michael Olise wa Crystal Palace kushindikana. (90 Min)
West Ham, Manchester City na Tottenham pia wanamtaka Doku. (Independent)
Chelsea iliafiki makubaliano ya kumsajili winga wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Olise, 21, wakati Palace ilipowafahamisha mawakili wa klabu hiyo kwamba watafikiria kupeleka kesi hiyo kwenye mahakama ya kimataifa. (Fabrizio Romano)
Chelsea pia inamtazama winga Mfaransa Bradley Barcola, 20, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Paris St-Germain ambao wamelazimika kutoa ofa ya euro 35m (£29.8m) na klabu yake ya Lyon. (RMC Sport – In French)
Davinson Sanchez analengwa na Monaco baada ya Tottenham kumfanya mlinzi huyo wa Colombia, 27, kupatikana kwa ajili ya kuhama msimu huu. (Telegraph – Subscription Required)
Manchester City wanajaribu kuipiku Brighton katika kumsajili beki wa kushoto wa Argentina mwenye umri wa miaka 19 Valentin Barco kutoka Boca Juniors. (Mail)
Bayern Munich haitamsajili mlinda mlango wa Uhispania David de Gea, 32, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Manchester United, huku meneja Thomas Tuchel akipinga wazo hilo. (Florian Plettenberg)
Beki wa Bayern Mfaransa Benjamin Pavard, 27, anatazamiwa kuchagua kati ya kuhamia Manchester United au Inter Milan kabla ya mwisho wa dirisha. (L'Equipe – In French)
Liverpool wako tayari kukamilisha usajili wa Wataru Endo, huku Stuttgart ikiwa imekubali dau la pauni milioni 16 huku kiungo huyo wa kati wa Japan mwenye umri wa miaka 30 tayari akiwa amekubali masharti ya kibinafsi. (Football Insider)
Liverpool wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Gabon Mario Lemina, 29, kutoka Wolves. (Footmercato – In French)
Fulham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Arsenal wa Marekani Folarin Balogun, 22. (Mail)
West Ham wanakaribia kuafikiana na Stuttgart kwa ajili ya kumnunua beki wa Ugiriki Konstantinos Mavropanos, 25. (Sky Sports, via Football Daily)
The Hammers wanasonga mbele katika mazungumzo na Ajax kuhusu kiungo wa kati wa Ghana Mohammed Kudus, 23, ambaye anatazamiwa kuongeza hamu ya kumnunua mshambuliaji wa Montpellier wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Elye Wahi, 20, na pia wanafikiria kumpa mkataba wa muda mfupi kama mchezaji huru. Jesse Lingard, 30. (Guardian)
Everton na West Ham wana nia ya kumsajili winga wa Porto Mreno Goncalo Borges, 22. (Fabrizio Romano)
Arsenal wanafikiria kuingia kwenye soko la uhamisho wa beki mpya baada ya mchezaji aliyesajiliwa majira ya kiangazi, Jurrien Timber kuwa nje kwa msimu huu kutokana na jeraha baya la goti. (Telegraph – Subscription Required)
Beki wa pembeni wa Manchester City na Ureno Joao Cancelo, 29, anasalia kulengwa na Barcelona lakini sasa vilabu vya Saudi Arabia pia vina nia kubwa. (Subscription Required)
PSV Eindhoven wanatamani kumsajili beki wa pembeni wa Marekani Sergino Dest, 22, kwa mkopo kutoka Barcelona. (ESPN)
Manchester City wamelipa £1m kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa Tyrese Noubissie mwenye umri wa miaka 14 kutoka Leicester. (Talk Sport)