Kwanini Urusi inataka kufanya kura za maoni katika maeneo iliyoyateka?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vladmir Putin
Iliyochapishwa

Maafisa wanaoungwa mkono na Urusi katika mikoa minne inayokaliwa kwa mabavu ya Ukraine wametangaza kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu kujiunga na Urusi.

Kuna mwangwi wa unyakuzi kama ule wa Crimea, lakini hii ni tofauti, kwani mikoa yote minne iko vitani na Urusi iliiteka Crimea bila kufyatua bunduki.

Ni nini kinaendelea na kwa nini sasa?

Baada ya karibu miezi saba ya vita, Vladimir Putin amejipata mahala pabaya huku vikosi vyake vikirudishwa nyuma .. Mashambulizi ya Ukraine yamekomboa tena maeneo mengi yaliyotekwa miezi kadhaa baada ya uvamizi wa Urusi wa tarehe 24 Februari.

Anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa watu wenye msimamo mkali kujibu, na kuunga mkono kura za maoni kama ilivyofanyika Crimea. Vyombo vya habari vya Urusi tayari vinatoa matokeo ya mapema ya kura hizo zinazodai uungwaji mkono mkubwa wa kujiunga na Urusi, lakini ni za uwongo sawa na kura zilizopigwa katikati ya vita, bila kuchunguzwa ipasavyo au uhalali wake.

Kama zilivyokataliwa 2014 katika eneo la Crimea kuwa kura ya aibu na jamii ya kimataifa , pia kura hizi zimeshtumiwa na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani.

Lakini Rais Putin anaweza kuhisi kwamba kutangaza maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kuwa maeneo ya Urusi kunaweza kubadili mkondo wa vita, kwani kutamwezesha kuwaambia wafuasi wa nchi za Magharibi wa Ukraine kuacha kusambaza silaha. Vyombo vya kurushia makombora vya Himars kutoka Marekani vimeathiri vibaya vikosi vya Urusi.

Mchambuzi wa Urusi Alexander Baunov anasema matumaini ya Urusi ni kwamba nchi za Magharibi zitatilia shaka wazo la kupigana katika kile ambacho Urusi inakichukulia kuwa eneo lake.

Nini inachofanya kura hizo kuwa za aibu?

Kwa muda wa siku tano, kuanzia tarehe 23-27 Septemba, mikoa minne ya Ukraine ambayo inakaliwa kwa kiasi au yote na Urusi itashiriki katika kura za maoni ambapo watu watapiga kura binafsi au kwa mbali.

Kura hiyo ni ya kujiunga na Shirikisho la Urusi na mkuu wa mkoa wa Kherson aliyewekwa na Urusi kusini, Vladimir Saldo alisema kuijumuisha na Urusi "kutalinda eneo letu na kurejesha haki ya kihistoria".

Mji mkuu wa kikanda, Kherson , si mahali salama kwa sasa, huku wanajeshi wa Urusi wakijitahidi kuzuia mashambulizi makali ya Ukraine. Jengo kuu la utawala lilishambuliwa na mfululizo wa makombora wiki iliyopita tu, hivyobasi kura salama haiwezekani.

Halafu kuna mji mkuu wa Zaporizhzhia, ambao umesalia chini ya mikono salama ya Ukraine, kwa hivyo kura yoyote ya kujumuisha eneo hilo haina maana yoyote.

.
Maelezo ya picha, Ramani ya Ukraine
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Donetsk upande wa mashariki ipo 60% tu chini ya uvamizi wa Urusi na ndio kiini cha mzozo huo, wakati Urusi inadhibiti sehemu kubwa ya Luhansk kaskazini-mashariki licha ya kuanza kushindwa.

Idadi kubwa ya watu kabla ya vita wametoroka. Mkuu wa mamlaka ya wakala wa Urusi huko Donetsk, Denis Pushilin, aliamuru watu kuhamishwa siku chache kabla ya uvamizi huo.

Viongozi wa waliowekwa na Urusi wanaweza kuwa na nia ya kuandaa kura ya maoni kwa miezi kadhaa, lakini uamuzi huu wa haraka siku tatu tu unakatisha tamaa.

Kwa maneno ya Emmanuel Macron wa Ufaransa: "Urusi ilianza vita, ilivamia eneo hili, ilishambulia watu kwa mabomu, ikawafanya watu kutoroka na sasa wanasema katika eneo hili hili itaandaa kura ya maoni."

"Tunaona kwamba raia wote wanapendelea kurejea Ukraine, na hii ndiyo sababu kuna upinzani mwingi wa waasi katika maeneo haya, kwa hivyo kura hizi za maoni hazifai," mshauri wa wizara ya ulinzi ya Ukraine Yuriy Sak aliiambia BBC.

Kipi kitajiri baada ya kuyatenga?

Yote ni tofauti na 2014. Kiongozi wa viongozi waliowekwa na Urusi Donetsk ametoa wito kwa Bw Putin kujibu uamuzi chanya baada ya 27 Septemba - "ambao hatuna shaka nao" - utazingatia kuwa sehemu ya Urusi.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba rais wa Urusi ataamua kunyakua mikoa yote minne, lakini kutakuwa na mabadiliko japo kidogo kutokana na mashambulizi ya Ukraine yanayoendelea.

Huenda Urusi ikataka nchi za Nato ziache kuipatia Ukraine silaha lakini hakuna hata mmoja wao atakayetambua kura hizo. Kama Taasisi ya Uchunguzi wa Vita inavyoonyesha, Ukraine tayari imefikia malengo ya kijeshi ya Urusi huko Crimea, na hakukuwa na kisasi cha Kirusi.

Je Urusi inajiandaa kutangaza vita?

Hadi sasa, rais wa Urusi hajatangaza vita, akiitaja kampeni hii  ya uvamizi wa Ukraine"operesheni maalum ya kijeshi". Hilo limezuia uhamasishaji kamili na kuna mazungumzo kwamba anaweza kuwa katika harakati za kuchukua hatua hiyo.

Wakati maeneo hayo manne yalipokuwa yakitangaza kushirika kwa kura ya maoni , baraza la chini la bunge la Urusi lilikuwa likiharakisha mabadiliko ya sheria ya kuanzisha dhana ya "maandalizi ya vita huku adhabu zikipewa watakaotoroka vita, kujisalimisha au kutokuwepo bila likizo (AWOL).

Mazungumzo ya kutangaza vita huenfda yapo mezani, lakini si kwa haraka.

Bw Putin anatoa ishara kwa washirika wake waliosalia kuwa anajaribu kumaliza vita. Rais wa Uturuki alisema Putin alimwambia kuwa anajaribu kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo, kama hilo halitafanikiwa, Alexander Baunov anaamini kuwa basi ataweza kuwalaumu wengine na kugeuza uvamizi wake nchini Ukraine kuwa vita vya kujihami. Kisha Moscow ingetumai kuhalalisha mzozo huo miongoni mwa Warusi wa kawaida na kuchukua hatua zaidi.

Je, kuna hatari ya shambulizi la kinyuklia?

Waenezaji wa propaganda wa Urusi mara kwa mara wanatishia matumizi ya silaha za nyuklia za nchi hiyo, haswa wakati huu ambapo vikosi vyao vyenye silaha vinashindwa kwenye uwanja wa vita huko Ukraine. Pia wamejenga kampeni ya vita vya Ukraine kama vita visivyo vya moja kwa moja dhidi ya  Nato, ingawa viongozi wa Magharibi wamekuwa waangalifu sana kuepusha migogoro ya moja kwa moja.

Naibu mkuu wa baraza la usalama la Urusi, Dmitry Medvedev, alitoa tishio siku ya Jumanne aliposema kwamba baada ya Urusi kunyakua maeneo hayo, uvamizi wowote kwenye eneo la Urusi unaweza kukabiliwa na "nguvu zote za kujilinda".

Mtangazaji wa propaganda za Urusi Margarita Simonyan alisema kwamba mashambulizi katika eneo la Urusi yatakuwa "vita kamili kati ya Ukraine na Nato na Urusi, hali itakayoiondolea lawama  Urusi".

Mbunge wa Conservative nchini Uingereza Bob Seely, ambaye ametembelea Kyiv, anaamini tishio la nyuklia kwa kiasi kikubwa ni tishio la  kuzitia hofu nchi za Magharibi kusitisha usambazaji wa silaha kwa Ukraine.

Lakini anaonya juu ya hatari ambayo inaweza kujitosheleza, ili Urusi ihalalishe matumizi ya silaha za nyuklia "kwa kiwango ambacho kitakuwa jibu la busara, hata hivyo hatufikirii kuwa ni majibu ya busara".