Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Alijaribu kupata mtoto kwa miaka 7, akazaa watoto 5 mara moja
Ankita Kumari na Prakash Kumar Saw kwa sasa wako katika hali nzuri ya furaha katika hospitali ya Taasisi ya Rajendra ya Sayansi ya Tiba (RIMS) huko Ranchi kwa kuwa wana watoto baada ya karibu miaka saba ya ndoa. Lakini katika furaha hii kuna wasiwasi fulani pia.
Madaktari wanasema watoto na mama yao wanaendelea vizuri, lakini watalazimika kukaa hospitalini wiki chache zijazo.
Binti zao huwekwa kwenye viingilizi katika chumba cha wagonjwa mahututi cha ICU cha hospitali mbili tofauti.
Ankita Kumari amelazwa katika hospitali ya RIMS tangu Mei 7 na anaendelea na matibabu katika kitengo cha Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Madaktari wa Uzazi Dk Sasibala.
Wakati wa uchunguzi wa ujauzito, daktari alimwambia kwamba alikuwa na watoto wengi tumboni mwake.
Alasiri ya tarehe 22, ghafla alianza uchungu na ndani ya nusu saa alijifungua wasichana watano mmoja baada ya mwingine.
Dk. ambaye ni sehemu ya timu ya Dkt. Sasibala Bulupriya alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa watoto watano kuzaliwa kwa wakati mmoja huko Rims. Hapo awali, mwanamke mmoja alizaa watoto wanne kwa wakati mmoja, lakini rekodi hiyo sasa imevunjwa.
Akizungumza na BBC, Dkt Bulupriya alisema, “visa kama hivi hutokea lakini hii haishangazi sana. Uzazi kama huo unatokea ulimwenguni kote. Ni mchakato wa kawaida kwa yai zaidi ya moja kuunda kwenye kiinitete. Hii haileti hatari, lakini ikiwa zaidi ya kiinitete kimoja kitatokea kutoka kwa mayai hayo, kuna hatari ya kuzaa kabla ya wakati na watoto wenye uzito mdogo."
"IVF sio muujiza kwa wale ambao hawawezi kuwa wazazi kawaida."
“Ankita hajaweza kuwa mama kwa miaka saba iliyopita. Kwa hivyo alifanya IVF kutoka hospitali ya Hazaribagh. Kwa miezi kadhaa wenzi hao walikuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Uchunguzi ulionyesha kuwa kijusi kilikuwa na viinitete vingi, kwa hivyo vilitumwa kwa RIMS."
"Ankita alikuwa na ujauzito wa wiki 28 alipokuja kwetu. Tulitaka siku zake ziwe kamili, lakini alianza kupata hali ya uchungu wa uzazi mapema. Jambo zuri kuhusu hilo ni kwamba alijifungua kawaida, bila upasuaji."
“Mkuu wetu Dk. Neelam na timu yake walimzalisha Ankita. Watoto wake watatu walizaliwa wima na wawili juu chini. Wakati huo huo, hali ya Ankita ilikuwa shwari. Ikiwa hali yake itaendelea hivi, tutamwachia baada ya wiki chache. Lakini huenda binti zake wakalazimika kukaa hospitalini kwa majuma machache.”
Ankita na Prakash
Ankita mwenye umri wa miaka 27 anaishi katika kijiji cha Malakpur wilayani Chatra katika jimbo la Jharkhand. Mumewe Prakash Sav ni mwendeshaji wa gari la kubebea matuna, kazi anayofanya kujipatia riziki.
Hapo awali, alikuwa akifanya kazi katika hoteli fulani. Anauza matunda tangu alipoacha kazi. Yeye ndiye mkubwa kati ya ndugu zake.
Akizungumza na BBC, Prakash Sav alisema, "Sikuwahi kufikiria kuwa ningekuwa na binti watano kwa wakati mmoja. Tumefurahi kupata mtoto baada ya miaka mingi ya ndoa lakini sasa tuna wasiwasi pia juu ya kuokoa maisha ya wasichana hawa. Nimelazimika kuwalaza wasichana wawili waliozaliwa katika hospitali ya kibinafsi kwani hakuna vitanda vinavyopatikana Rims. Wasichana watatu waliobaki wako Rimes.
Malalamiko ya Prakash Sav (baba watoto)
"Swali langu ni kwamba ikiwa mke wangu alilazwa hapa kwa siku 16 zilizopita basi kwa nini hospitali ya RIMS haikupanga kitanda kuokoa binti zangu.
Kila mtu alijua kuwa mke wangu alikuwa na watoto watano tumboni mwake. Jana usiku ghafla niliambiwa kuwa hakuna nafasi hapa NICU, unapaswa kuwapeleka watoto wawili hospitali ya kibinafsi. Mimi ni maskini, siwezi kumudu hospitali binafsi.”
Uongozi wa Rims haujatoa maoni yoyote rasmi kuhusu madai ya Prakash. Lakini madaktari wanaofanya kazi katika idara ya watoto wanasema kuwa vitanda vya NICU vilikuwa vimejaa. Kwa hiyo wasichana hao wawili waliombwa kulazwa NICU ya hospitali ya kibinafsi.”
Daktari mkuu kwa sharti la kutotajwa jina alisema, "Idadi ya vitanda katika NICU ni ndogo. Watoto wachanga tayari wamelazwa huko. Hawawezi kuondolewa huko kwani hali zao ni mbaya."
Aliongeza, “Ankita amejifungua kabla ya wakati wake, na kuongeza kuwa kuna utaratibu wa kuwahifadhi watoto katika kifaa cha kuhifadhia watoto waliozaliwa kabla ya muda wao (inkubator) kwa hiyo shutuma za baba yao si sahihi.
Alimshauri awapeleke watoto wake katika hospitali ya kibinafsi ili kuokoa maisha yao. Kipaumbele chetu ni kuwatendea watoto, sio kumdhulumu mtu yeyote”, aliongeza
Baba yao Prakash alilalamika kuwa alitumia pesa nyingi sana huko Ranchi kwa matibabu, malazi, chakula na dawa hivi kwamba alilazimika kuchukua mkopo.
Kwa mujibu wa kitabu cha recodi ya dunia cha Guinness Book, rekodi ya kuzaa watoto wengi zaidi kwa wakati mmoja inashikiliwa na Halimah Cisse wa Mali.
Alizaa watoto 9 kwa wakati mmoja katika mwaka wa 2021. Kulikuwa na wasichana 5 na wavulana 4.