Marufuku ya kutoka nje inavyohusishwa na ongezeko kubwa la picha za ngono za watoto

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Picha zinazoonesha watoto wadogo wakifanya vitendo vya ngono mbele ya kamera zinaongezeka kwa zaidi ya mara kumi tangu marufuku ya kutoka nje ya janga la corona, takwimu mpya zinaeleza.

Taasisi ya The Internet Watch (IWF) inasema takwimu zinaangazia jinsi wahalifu walivyotumia hali hiyo. 

Picha za kwenye mitandao ya kijamii ziliongezeka kwa kasi mwanzoni mwa mwaka 2020 wakati wa janga hilo lilipoanza.

Mwaka jana IWF iliainisha zaidi ya kurasa 63,000 za wavuti zinazoonesha kile kinachoitwa video na picha za unyanyasaji wa watoto, ikilinganishwa na idadi ya 5,000 kabla ya janga hilo.

Hali hii inaonesha picha za watoto wakinyanyaswa kingono kwenye kamera na kuekwa kwenye mtandao.

"Wakati wa janga la corona, intaneti ilikuwa njia mbadala wa kuokoa maisha lakini sasa tunaona athari zake," mtendaji mkuu wa IWF Susie Hargreaves alisema.

"Kilicho wazi kwetu ni kwamba watoto wadogo wanasukumwa katika mazingira ya dhuluma na watu waovu, mara nyingi wakiwa katika vyumba vyao vya kulala."

Kwa ujumla IWF hufuatilia, huchunguza na kujaribu kuondoa mamia ya maelfu ya matukio ya  unyanyasaji wa kingono kwa watoto katika mitandao yote duniani.

Shirika hilo la kujitolea linasema lina uhakika kwamba ongezeko la picha zinazozalishwa ni  sababu kubwa la ongezeko la uhalifu huo mtandaoni, kwa sababu viwango vya kuripoti vimesalia kuwa sawa katika miaka ya hivi karibuni.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Video na picha za unyanyasaji wa watoto sasa ni theluthi mbili ya picha zinazochunguzwa na watafiti.

Watafiti wanasema video nyingi zimerekodiwa au kuwekwa moja kwa moja kutoka vyumba vya kulala au bafuni, na sauti za shughuli za nyumbani zinasikika kwa mbali.

Mara nyingi huwa ni video zinazoenda moja kwa moja mtandaoni, na kurekodiwa bila mtoto kujua na kuuzwa na kwa watu wanaovutiwa kufanya mapenzi na watoto.

IWF ni shirika lenye makao yake nchini Uingereza na linasema mara nyingi ni vigumu kufahamu ni wapi watoto wanatoka kwenye video hizo.

Hata hivyo, hupitisha kesi kwa mamlaka ikiwa sare ya shule au vitambulisho vingine vinaonekana.

Katika picha ambazo shirika hilo la msaada limeona linakadiria kuwa ni za watoto wenye umri wa miaka saba hadi 10.

Huku zaidi ya video 8,000 zilikuwa zimeainishwa katika A.

Kundi hilo unaweza kujumuisha vitendo vya ngono, picha zinazohusisha ngono na mnyama, au ugomvi.

Katika video moja iliyoonekana na wachambuzi wa IWF, msichana mwenye umri wa miaka tisa anaagizwa na watu wazima kwenye jukwaa la mtandaoni kuigiza vitendo vya ngono akiwa katika chumba chake cha kulala huku amezungukwa na wanasesere wa kupendeza.

Anaambiwa kufanya “vitendo vichafu" kwenye kamera lakini video inakatizwa wakati mtu anayedhaniwa kuwa mwanafamilia, ambaye hajui kama kuna unyanyasaji wa kingono unaofanyika, anamuita binti huyo kumuogesha kaka yake mdogo.

IWF inatoa wito kwa serikali ya Uingereza lakini shirika hilo linasisitiza kuwa video nyingi zinazopatikana zinatoka duniani kote na nyingi hazitengenezwi nchini Uingereza. 

Kituo cha Kitaifa cha Marekani cha Watoto Waliopotea na kunyanyaswa hakikuwa na takwimu za 2022, lakini kiliripoti ongezeko la video za unyanyasaji wa kingono kwa watoto kwa mwaka wa 2021. CyberTipline ya shirika la misaada ilipokea ripoti milioni 29.4, kutoka milioni 21.7 kwa mwaka wa 2020.