Dereva 'bodaboda' mwenye ulemavu wa kusikia Tanzania

Dereva 'bodaboda' mwenye ulemavu wa kusikia Tanzania
Iliyochapishwa

Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani (WHO) ajali za barabarani huua watu 1.3milioni kila mwaka duniani.

Nchini Tanzania asilimia 6% ya vifo vinavyotokea kila mwaka vinasababishwa na ajali za barabarani.

Ili kuepuka ajali, ungetamani kuendeshwa na dereva unaemuamini zaidi atakayekuhakikishia usalama wako barabarani. Lakini Sio wote wangetamani kuendeshwa na mtu asiyesikia. Licha ya ulemavu wake wa kutosikia, Ally Jumanne amekuwa dereva wa 'bodaboda' kwa miaka 11 akiendesha Maisha yake na familia yake.

Unaweza kujiuliza anawasilianaje na abiria wake? na je usalama wake na abiria barabarani ukoje? Yusuph Mazimu amemtembelea mkoani Dodoma katikati mwa Tanzania na hii ni taarifa yake.