Tetesi za soka Ulaya Jumatano 17.04.2024

..

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jadon Sancho
Iliyochapishwa

Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, atakuwa tayari kurejea na kucheza tena soka yake katika klabu ya Manchester United iwapo meneja Erik ten Hag ataondoka. (News)

Arsenal wanatarajiwa kufufua nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa na Brazil Douglas Luiz, 25, msimu huu. (Football Insider)

Fulham imeweka kipaumbele kumsajili Trevoh Chalobah wa Chelsea, 24, kama mbadala wa mlinzi mwenzake wa kati Tosin Adarabioyo, 26, ambaye anatarajiwa kuondoka mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (TeamTalks)

Manchester United wameelekeza mawazo yao kwa beki wa Nice mwenye umri wa miaka 24 Jean-Clair Todibo baada ya kupunguziwa bei ya kumsajili beki wa kati wa Everton, 21, Jarrad Branthwaite. (TeamTalks)

.
Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Man United na Brazil Antony mbele

United wanataka kumuuza winga wa Brazil Antony, 24, msimu ujao (Rudy Galetti)

Bayer Leverkusen wameweka bei ya euro 150m (£128m) kwa kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz mwenye umri wa miaka 20 huku Barcelona na Real Madrid wakimtaka. (Radio Marca via Mundo Deportivo – In Spanish)

Arsenal na Liverpool wanavutiwa na beki wa kati wa Ecuador Willian Pacho, 22, anayechezea Eintracht Frankfurt. (Florian Plettenberg)

Arsenal itamfanya mshambuliaji wa Uingereza Eddie Nketiah, 24, kupatikana kwa uhamisho msimu huu wa joto lakini wataomba £40m. (HITC)

Tottenham wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Giorgi Sudakov, 21. (Offside).

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kobi Mainoo

Newcastle wameanzisha upya nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Nottingham Forest Muingereza Morgan Gibbs-White, 24. (Football Insider)

Liverpool wanatazamiwa kumteua David Woodfine kama mkurugenzi msaidizi wa michezo wa Richard Hughes, baada ya kurejea Anfield chini ya mwaka mmoja baada ya kuihama klabu hiyo. (Liverpool Echo)

Manchester United itaanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 18 kuhusu kandarasi mpya msimu ujao. (Sun)

Everton wana nia ya kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, 27, ambao unamalizika mwishoni mwa msimu ujao. (Football Insider)

.

Chanzo cha picha, Getty Imagdes

Maelezo ya picha, Authur Okonkwo

Wrexham wanataka kubadilisha mkopo wa mlinda lango wa Uingereza Arthur Okonkwo, 22 kutoka Arsenal kuwa mkataba wa kudumu. (Subscription Required)

Juventus itasikiliza ofa kwa fowadi wa Italia Federico Chiesa, ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool na Newcastle, baada ya kutofautiana kati ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na bosi Massimiliano Allegri kuhusu jukumu lake. (Tuttosport – In Italy)

Imetafsiriwa na Seif Abdalla na kuhaririwa na Florian Kaijage