Je, kugandisha yai kuna uhusiano gani na mwajiri wako?

Chanzo cha picha, Carol Chen
Alizaliwa na kukulia Texas, mjasiriamali aliyefanikiwa Carol Chen amejifanyia mengi kimaisha na katika biashara kadhaa za mitindo huko Singapore.
Alikuwa na ndoto ya kuwa mama. Lakini atachuku muda kidogo kufikia ndoto hiyo. Kuonyesha mitindo yake katika maonyesho ya wiki nzima ya mitindo mjini Pareis – hakuna shida. Kupata mwenzi wa maisha – ndio shida zaidi.
Alipofika katikati ya miaka yake ya thalathini, alianza kuwa na wasiwasi.
"Nilikuwa nimeanza tu kusoma taarifa kadhaa mtandaoni ambazo zinasema mwili wako unakuwa na uwezo mdogo sana baada ya miaka 35. Nilianza kushangaa," anasema.
Alikuwa mseja, ndipo akaamua wakati ulikuwa umewadia wa kugandisha mayai yake - njia ya kuhifadhi uzazi, ili ajaribu kupata watoto baadaye.
Ni mchakato mpya na viwango vya mafanikio vinatofautiana kwa kiasi kikubwa, kulingana na ni mayai mangapi ambayo mwanamke hugandisha na umri wake kwa wakati huo.
Utafiti wa 2016 uliojumuisha watu 1,171 waliotungishwa mimba kwa njia ya IVF kutumia mayai yaliyogandishwa, ulibaini kuwa wanawake waliogandisha mayai matano wakiwa na umri wa miaka 35 au chini, nafasi ya mtoto kuzaliwa hai ilikuwa 15%. Wakati nafasi hii iliongezeka hadi 61% kwa wanawake waliogandisha mayai 10 na 85% kwa wanawake waliogandisha mayai 15 au zaidi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ijapokuwa utafiti wa hivi karibuni ulinyesha 70% ya wanawake waliogandisha mayai yao wakiwa na umri wa chini ya miaka 38, na kuhifadhi walau mayai 20 kwa ajili ya kutumia baadaye, walipata watoto, wakati wa kuchanganua hizi data ni vyema kutilia maanani viwango vya uzazi kupitia mfumo wa IVF viko chini; ni 24% ya vijusi vinavyopachikwa, kulingana na Mamlaka ya Urutubishaji Binadamu ya Uingereza, Embryology.
Licha ya uwezekano huu, ugandishaji wa yai unaendelea kupata umaarufu, Kwa mfano, nchini Marekani mwaka wa 2017, wanawake 10,936 waligandisha mayai yao - au mara 23 zaidi ya walivyofanya mwaka wa 2009.
Singapore ndiyo nchi ya hivi punde zaidi kuondoa marufuku ya kugandisha yai kwa sababu zisizo za kiafya - marufuku hiyo itaanza kutekelezwa Januari 2023.
Nchini Uingereza, ugandishaji wa yai haushughulikiwi kwa kawaida na NHS, isipokuwa hali ya kiafya inayoathiri uwezo wako wa kushika mimba, kwa mfano, baadhi ya saratani au lupus. Ingawa hivi majuzi Serikali ya Uingereza ilitangaza kikomo cha miaka 10 cha kuhifadhi mayai yaliyogandishwa, manii na viinitete vitaondolewa.
Uwekezaji mkubwa
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Carol alitumia karibu $14,000 (£11,400) kwa mzunguko mmoja wa kugandisha yai na ilimbidi kusafiri Marekani kufanya hivyo. Hakuwa na mayai mengi alivyotaka, jambo ambalo anasema lilimfanya ajihisi "mwanamke mdhaifu."
Mwishowe, Carol alikuwa na bahati. Hakuhitaji kamwe kuwa na wasiwasi juu ya kulipia mzunguko mwingine wa kugandisha yai. Miaka miwili iliyopita, alikutana na mume wake wa sasa na aliweza kupata mimba kwa kawaida katika miaka yake ya 40.
Kwa kweli, asilimia ya wanawake ambao hutumia mayai yao yaliyogandishwa inabaki chini sana, chini ya 10%.
Utafiti mwingine mdogo ulichanganua data kutoka kliniki mbili kubwa zaidi za uzazi mjini London; katika kipindi hiki cha miaka kumi, 2008-2017, ni karibu theluthi moja tu ya wagonjwa ambao walikuwa wamegandisha mayai yao kwenye kliniki - walirudi kuyatumia.
Lakini mwelekeo huo haujawazuia waajiri kuijumuisha katika jalada linalozidi kupanuka la faida za uzazi. Hali hiyo ilianza, kwa njia isiyo ya kushangaza, huko Silicon Valley mnamo 2014, wakati Facebook na Apple zilipoanza kutoa huduma ya kugandisha yai kwa wafanyikazi wao kama sehemu ya kifurushi chao cha faida.
Nchini Uingereza, kampuni kama vile Banking Group, NatWest na kampuni ya nishati, Centrica, hutoa hadi £45,000 kwa kila mfanyakazi kwa matibabu au huduma ifaayo.
Jenny Saft, ni mwanzilishi mwenza wa jukwaa la teknolojia linalotoa manufaa ya uzazi, akifanya kazi na waajiri kote Ulaya. Anasema picha hiyo ni ngumu na kuna vikwazo na vikwazo vingi katika kupata matibabu ya uzazi yanayofadhiliwa na serikali - hivyo makampuni yanazidi kuingia.
Nchini Ujerumani, kwa mfano, bima ya afya hulipa nusu ya gharama kwa hadi mizunguko mitatu ya IVF, lakini tu ikiwa umeolewa, katika uhusiano wa watu wa jinsia tofauti na wenye umri wa chini ya miaka 40 ikiwa wewe ni mwanamke, anasema.

Chanzo cha picha, DR LUCY VAN DE WIEL
Lakini sio kila mtu anafikiria kuhusisha kampuni moja kwa moja, au bosi, katika uzazi wako ni habari njema.
Dkt Lucy Van De Wiel ni mhadhiri wa Global Health and Social Medicine katika Chuo cha King's College London. Anaziita sera hizi za ajira "teknolojia ya PR", ambayo inafanikiwa "kuvutia na kubakiza wafanyikazi wa kike, na hivyo ndivyo inavyouzwa na kampuni za bima kwa waajiri."
Dkt Van De Wiel ana wasiwasi kwamba mwekezaji wa bima anapata jukumu kuu katika jinsi watu wanavyozingatia uchaguzi wao wa uzazi, hali ambayo inaweza kusababisha biashara nyingi za uzazi.
Anatambua kwamba, kwa upande mmoja, ni vyema wanawake kupata taarifa zaidi kuhusu uzazi wao, lakini wasiwasi wake ni kwamba, elimu hii inaweza kuwa inatoka kwa wataalamu ambao yanasimama kupata fedha kutoka kwa watu wanaotumia teknolojia hizo. "Ni vigumu sana kuepuka aina yoyote ya mgongano wa kimaslahi."
Hili ni jambo la kuhangaisha sana linapokuja suala la kugandisha yai kwa sababu, dhidi ya IVF, karibu wanawake wote walio chini ya umri fulani wanaweza kutibiwa kama mteja anayetarajiwa. Kila mwanamke ambaye anaweza kutaka kuwa na mtoto katika siku anaweza kuwa fursa ya kufungia yai.
Dkt Van De Wiel anasema kuna tafiti zinazoonyesha wanawake ambao wanapewa huduma hizi wanafurahi sana kuwa na chaguzi lakini pia wanahisi mwajiri wao anaweza kuwa anawaambia lazima 'wape muda' kupata watoto.

Chanzo cha picha, NYASHA
Wakili wamasuala ya burudani mwenye makao yake mjini, Nyasha Foy, anafahamu mgongano wa kimaslahi unaoweza kutokea hapa.
Kampuni yake ilijitolea kulipiaawamu mbili za kugandisha na kuhifadhi mayai, na kuamua kuchukua hatua hiyo.
"Si kukutana na mpenzi wangu chuoni, sikukutana naye katika chuo cha uwakili," anaelezea, "Kwa hivyo aliona haja ya kuharakisha kupata mtoto. Niko sawa na uboreshaji wake, hasa nchini Marekani, kwani tunahitaji kutathmini tena kesi ya Roe v Wade. Ili kuweza kusema kama mwanamke , Naamua kusubiri muda mrefu kidogo. Chaguo hilo sio maumbile uhuru wa mwili, huo ni uhuru wa maisha," anahitimisha.

Chanzo cha picha, Aimee Eyvazzadeh
Bila shaka ugandishaji wa yai unazidi kushika kasi katika ulimwengu ulioendelea, na kliniki za uzazi zinawania kuvutia wateja kwa njia yoyote inayoruhusiwa.
Daktari wa uzazi, Aimee Eyvazzadeh, AKA "egg whisperer", anahudumu mjini California, na ana julikana kwa kufnya sherehe za ugandishaji wa yai katika "migahawa ya kifahari yenye baa nzuri na vyakula vya kupendeza."
Anakubali kuwa ni wasiwasi kwamba kugandisha yai kunazungumzwa kama njia ya "kuchukua udhibiti", au kama sera ya bima. "Unaweza kuwa umejipa nafasi ya baadaye, lakini nafasi inaweza kuwa si kubwa kama vile ulivyofikiria hapo awali," anaongeza.
Mgonjwa wa wastani wa Dk Eyvazzadeh ana umri wa miaka 39. Anadhani kuwa katika miaka 15 ambayo inaweza kuongezeka hadi 49.
Kwa hiyo, anaamini kwamba wanawake wadogo, ambao hawana masuala ya uzazi, wanapaswa kuzingatia sana kuhifadhi mayai yao - "kwa ajili ya kutumia wakati watakapotimia miaka 40.
"Wakati huo huo, kwa upande mwingine wa Marekani, Nyasha Foy anazingatia hatua zake zinazofuata. Bado hajatumia mayai yake yaliyogandishwa na bado anatarajia kukutana na "baba mtoto" kwanza.
"Nina umri wa miaka 37 sasa. Nikifika mahali ambapo siwezi kushika ujauzito, nitakuwa katika nafasi ya kuweza kupata mrithi," anasema.












