'Nilifungwa jela kwa kuwa mimba yangu ilitoka'

Elsy
Maelezo ya picha, Elsy alitumikia kifungo cha miaka10 jela kwa kosa la mauaji mabaya baada ya kuuugua mimb a ilipotoka 
Iliyochapishwa

Taarifa kutoka Marekani kwamba wanawake wanakabiliwa na sheria kali ya utoaji mimba imepokelewa  nchini El Salvador kihisia, ambayo inasheria kali za kuzuwia upatikanaji wa hudumua ya utoaji mimba. 

 Mwezi Februari, wanawake wanne waliketi mbele ya vyombo vya habari vya habari vya El Salvador. Miongoni mwao, wamekwisha kutumikia kifungo cha jela kwa karibu miaka 50.

 Uhalifu wao ulikuwa ni bahati mbaya ya kuugua kutokana na mimba kutoka- katika nchi yenye sheria kali zaidi za utoaji mbimba duniani.

 Miongoni mwao alikuwa ni Elsy.

 Mnamo mwezi Juni 2011, Elsy alikuwa mjamzito na alikuwa akifanya kazi kama mfanyakazi wa nyumbani katika mji wa kwao. Anakumbuka alipokuwa akienda chooni, ambako alipoteza fahamu,

 Baada ya kupata fahamu muda mfupi baadaye, alijipata akiwa amezingirwa na maafisa wa polisi. Mtoto wake alikuwa amefariki. Mwajiri wake alikuwa amemripoti kuwa ametoa mimba. 

 Katikia kesi yake, Elsy alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa mauaji mabaya. Alihudumu miaka 10 kabla ya wanakampeni kuweza kufanikiwa kufupisha kifungo chake. 

Salvador

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, PICHA: Katika mwezi Mei 2022, wanawake wanne Wasalvador walizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kufungwa kwa mimba za kutoka   

"Nilihisi vibaya sana katika gereza, nilicjhoweza kufikiria tu ilikuwa ni miaka 30 ya kifungo," Elsy aliiambia  BBC. "Nilifikiri sitaweza tena kamwe kumuona mama yangu au mtu mwingine wa familia yangu tena."

Akiwa sasa amerejea kuishi na familia yake, Elsy anasema hukumu ilikuwa   "ukosefu wa  haki ambao anyika" katika El Salvador. Anasema kuwa kuna wengi ambao bado wanaopitia aliyoyasema. 

Hivi karibuni mnamo mwezi Mei, mwanamke aliyetambuliwa kama  "Esme" alihukumiwa kufungwa miaka 30 jela, pia kwa kuua kifo kibaya kufuatia mimba yake kutoka. 

Mariana Moisa sanasema haki za utoaji mimba ni mada inayoumiza kwa watu kiasi kwamba wanaona afathari wasiizungumzie.
Maelezo ya picha, Mariana Moisa sanasema haki za utoaji mimba ni mada inayoumiza kwa watu kiasi kwamba wanaona afathari wasiizungumzie.

Lakini maandamano yamekuwa magumu tangu rais  wa nchi hiyo mwenye utata, Nayib Bukele, kuweka hali ya kipekee ambayo inawapatia polisi mamlaka makubwa ya kuwakamata watu.

 Mariana Moisa ni mmoja  wa wanawake wanaoongoza wanaharakati wanawake wanaopigania haki za wanawake nchini El Salvador .

 "Lazima tuendelee kufanya kazi, inategemea sisi wenyewe na sio vyama vya kisiasa  ", anasema katika makao makuu ya shirika lake katika mji wa San Salvador. "Ni lazima tukabiliane na uhalisi wet una kupigia debe mabadiliko halisi ya kiutamaduni."

 Nchini Marekani, Mahakama ya juu zaidi imebatilisha uamuzi ambao ulikuwa umehalalisha utoaji mimba katika haki ya kikatiba. 

Wanaharakati kama Bi Moisa wanahofu kuwa hii itaimarisha mkono wa Waconservative kote katika Amerika ya Kati.   

Salvador

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, El Salvador imeshuhudia maandamano machache yanayounga mkono haki za utoaji mimba hivi karibuni ikilinganishwa na mataifa mengine Jirani ya Amerika Kusini 
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kubadilisha mitizamo katika El Salvador halitakuw ajambo rahisi hatahivyo. 

Padre Vito Guarato ni makazi ya watoto waliotelekezwa katika San Salvador, ambao wengi wao wana aina fulani ya ulemavu.

 Ana Lucia mwenye umri wa miaka mitano ana hali ya ulemavu inayoitwa microcephaly, ambapo watoto huzaliwa wakiwa na vichwa vidogo sana, labda kutokana na maambukizi ya virusi vya Zika.

Huku akiwa amelala kwenye eneo lake la mucheza, akiwa amezingirwa na wanasesere, Ana Lucia anahitaji uangalizi wa kila wakati. 

Lakini kusema kweli, kutokana na ukosefu wa chaguo la kutoa mimba katika El Salvador,  baadhi ya wazazi wasio kuwa na la kufanya huamua kuwatelekeza watoto wenye matatizo kama ya Lucia.

"Ninadhani akina mama wanapaswa kuchukua jukumu lao ", anasema  Rosa Evelyn, mmoja wa mameneja wa kanisa linaloendesha kituo cha  malezi ya watoto.

 "Kama Mungu amekupatia baraka ya kuwa mama, basi unatakiwa kuwa mama kwasababu Mungu ameruhusu hilo ,"anasema.

Ni maoni waliyonayo wengi katika nchi hii ambayo ni taifa la Kikatoliki.  Zaidi ya hayo dini inayokuwa kwa haraka katika Amerika ya Kati ni ya Ukristo.

Baadhi wanakadiria kuwa ha  40% ya Waelsalvador ni Wainjilisti
Maelezo ya picha, Baadhi wanakadiria kuwa hadi 40% ya Waelsalvador ni Wainjilisti 

Huku mafundisho ya Kikristi yakiendelea kusambaa, ndivyo siasa zinavyoendelea pia kushika mkondo wa kikristo, huku maadili ya kiinjilisti na mitizamo ikiendelea kuongezeka ndani ya bunge.

Guillermo Gallegos, ambaye ni mmoja wa mamakamu war ais wa bunge la taifa, ni mpinzani mkuu wa utoaji mimba. 

 Katika hotuba ya taifa katika maadhimisho yam waka wake wa tatu mamlakani Rais  Bukele alisifu mpango, ulioongozwa na mke wake, wa kufanya watoto wazaliwe salama mahospitalini. 

 Utoaji mimba, hatahivyo, unazuiwa kabisa, hata mtuanapobakwa- mtizamo ambao sasa umeimarishwa na uamuasi wa Mahakama ya juu zaidi ya Marekani.