Trump: 'Nilimwambia Netanyahu kutofanya jambo lolote litakalovuruga mazungumzo ya nyuklia na Iran'

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Trump
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Rais wa Marekani Donald Trump alisema wiki iliyopita alimuonya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutochukua hatua yoyote ambayo inaweza kuvuruga mazungumzo ya nyuklia na Iran, akielezea matumaini kwamba mazungumzo na Tehran yatatimia.

"Kusema kweli, ndio, nilisema hivyo," Bw. Trump alisema akimjibu mwanahabari aliyemuuliza ikiwa alimwomba Netanyahu katika simu wiki jana asifanye lolote litakalodhuru mchakato wa kidiplomasia.

Bw. Trump aliendelea kusema "Nilimwambia [Netanyahu] kwamba haikuwa sahihi kwa wakati huu, kwa sababu tulikuwa karibu sana na suluhu."

"Ni kweli, hali hii inaweza kubadilika wakati wowote," alisema

Iran na Marekani zinafanya mazungumzo yenye lengo la kuzuia shughuli za nyuklia za Iran ili kubadilishana vikwazo na Marekani, shughuli ambazo zimepanuka kwa kasi tangu Donald Trump ajiondoe kwenye mapatano ya nyuklia ya mwaka 2015 (JCPOA).

Katika wiki za hivi karibuni, Tehran na Washington zimefanya duru tano za mazungumzo, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi cha mawasiliano kati ya nchi hizo mbili tangu Trump ajitoe kwenye makubaliano ya nyuklia mnamo 2018.

Katika hotuba yake, Donald Trump amesema anataka makubaliano yenye nguvu na Iran na kuongeza, "Nataka makubaliano makali sana; ili tuweze kutuma wakaguzi, kuchukua chochote tunachotaka, kulipua chochote tunachohitaji, lakini bila kuua mtu yeyote. Kwa mfano tunaweza kuharibu maabara, lakini hakuna mtu ndani yake. Sio kila mtu yuko kwenye maabara na tunailipua.

'Ikiwa tunaweza kufanya makubaliano, maisha mengi yataokolewa'

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na rai wa Marekani Donald Trump

Kwa mujibu wa Rais wa Marekani, "Kuna njia mbili za kufanya hivyo. Nilimwambia kwamba sasa si wakati mwafaka kwa sababu tunakaribia sana kufikia suluhu na hali hii inaweza kubadilika wakati wowote. Kila kitu kinaweza kubadilika kwa kupiga simu. Lakini sasa hivi nadhani wanataka kufanya makubaliano. Na ikiwa tunaweza kufanya makubaliano, maisha mengi yataokolewa."

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Matamshi ya Bw.Trump yanajiri huku Iran ikitangaza kuwa iwapo makubaliano yataafikiwa, huenda ikafikiria kuwakubali wakaguzi wa Marekani kupitia Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki.

Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran alisema: "Kwa miaka mingi, tumejaribu kila mara kutokubali wakaguzi kutoka nchi zilizotuchukia na zenye tabia mbaya, kama vile walivyotenda kwa kujibu na hawakubali wakaguzi wa Iran." Hata hivyo amesema: "Katika mazingira ya sasa ya mazungumzo, ikiwa masuala yataibuliwa na kufikiwa makubaliano na matakwa ya Iran yazingatiwa, basi tutazingatia tena kukubali ukaguzi wa Marekani kupitia Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki."

Katika ziara yake nchini Oman, Rais wa Iran Masoud Pezzekian pia aliishukuru nchi hiyo kwa upatanishi wake katika mazungumzo ya Iran na Marekani.

Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na mpatanishi mkuu amesema tarehe ya duru mpya ya mazungumzo itajulikana katika siku zijazo.

Imetafsiriwa na Seif Abdalla na kuhaririwa na Ambia Hirsi