'Biashara halali ya bangi sio rahisi kama inavyodhaniwa'

Jimbo la California nchini Marekani limeanzisha mradi wa kuwapa watu walioathirika na ''vita dhidi ya mihadarati'' nafasi ya kujikimu kimaisha kwa kuuza bangi iliyohalalshwa. Lakini wanaofanya biashara hiyo wanasema kutajirika kutokana na biashara hiyo ni ngumu kuliko inavyodhaniwa.
Kila usiku, Julian Nelson analala kwenye kochi ndani ya ofisi ya biashara yake ya bangi mjini Oakland, California kwa kuhofia majambazi waliojihami kwa silaha wanaweza tena kuvamia duka lake. Duka hilo linaendesha shughuli zake kwa njia halali baada ya kutimiza masharti yote yaliyowekwa na mamla ya jiji hilolakini limekuwa likilengwa mara kwa mara nawezi.
"Nilipoanza, mtu alivamia na kuniibia kila kitu kabisa," Bw Nelson alisema.
Alinunua vifaa zaidi vya usalama, lakini aliibiwa tena mapema mwaka huu akiwa nje na kupoteza bidhaa za thamani ya dola 15,000.
Kuendesha biashara halali ya bangi kunamaanisha mengi kwa Bw Nelson. Aliwahi kukamatwa mara kadhaa kwa kupatikana na bangi siku za nyuma na hata kutumikia kifungo jela.
Lakini mpango unaoitwa Social Equity ulimpa Bw Nelson fursa ya kufungua biashara halali.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mpango wa jiji unalenga kupunguza vizuizi kwa tasnia ya kisheria ya bangi kwa wale wanaolengwa katika kile kinachojulikana kama "vita dhidi ya dawa za kulevya" Marekani- sera ya miongo kadhaa ambayo iligunduliwa kuwalenga Wamarekani weusi na Wahispania isivyo haki, kuweka watumiaji wa muda mdogo au wauzaji gerezani kwa kupatikana na dawa za kulevya.
Programu hiyo iliyoanza mwaka wa 2017, ilikuwa ya kwanza ya aina yake nchini Marekani na imepokea maombi zaidi ya 280, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
Leseni ya Usawa wa Kijamii inapaswa kuzipa jamii hizi kipande cha tasnia ya kisheria ya bangi ya California yenye thamani ya mabilioni ya dola na kuleta utofauti. Jimbo liliharamisha bangi mnamo 2016.
Imeigwa katika majimbo mengine ya Marekani na hata Meya wa London Sadiq Khan ametembelea biashara ya Usawa wa Kijamii huko Los Angeles ili kujifunza kuyahusu.
Lakini wakati ambao wamefungua maduka wameonyesha kujivunia kuweza kufanya kazi zao kihalali, pia wamekumbwa na matatizo.
Upatikanaji wa mtaji, matatizo ya benki, urasimu, ushuru wa juu kwa bangi inayouzwa kisheria na uhalifu ni baadhi tu ya vikwazo ambavyo wamelazimika kukabiliana navyo.
Bw Nelson alisema kuwa ingawa biashara ni nzuri, haikuwa rahisi kwake au kwa wengine kila wakati, na bado ni swali la wazi iwapo Usawa wa Kijamii umefungua sekta ya kisheria ya bangi kama ilivyonuia.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mpango huo ulizinduliwa zaidi ya miaka 50 baada ya Rais wa Marekani Richard Nixon kutangaza "vita dhidi ya madawa ya kulevya" mwaka 1971 dhidi ya kile kilichoitwa matumizi ya dawa za kulevya "adui namba moja wa umma" na uraibu ambao ni "janga la kitaifa".
Tangu wakati huo, ukubwa na uwepo wa mashirika ya serikali ya udhibiti wa madawa ya kulevya uliongezeka, kama vile kukamatwa na kufungwa, ambayo iliathiri zaidi Wamarekani weusi.
Kulingana na utafiti wa 2020 wa Muungano wa Uhuru wa Kiraia wa Marekani, Wamarekani weusi wana uwezekano wa karibu mara nne zaidi kuliko Wazungu kukamatwa kwa kupatikana na bangi, licha ya kuitumia kwa viwango sawa.
Utafiti muhimu uliofanywa na halmashauri ya Jiji la Oakland mwaka wa 2017 uligundua kuwa Wamarekani wenye asili ya kiafrika huko Oakland walikamatwa napolisi kwa kupatikana na bangi kwa hadiasilimia 80-90 kila mwaka huku Wazungu wakijumuisha asilimia nne tu ya watu waliokamatwa.
Chini ya Usawa wa Kijamii, nusu ya leseni za bangi huenda kwa waombaji wanaoishi katika maeneo ambayo yana idadi kubwa ya kukamatwa na kufungwa kwa kupatikana na bangi. Pia hupata malipo ya leseni na wanaweza kutuma maombi ya usaidizi wa kifedha kwa njia ya ruzuku na mikopo.
Kutoka kuwa askari hadi mshauri wa bangi

Bw Nelson anasema biashara nyingi za bangi huko Oakland zimevamiwa na kuibwa.
Anaamini ni kwa sababu wanafanya kazi na pesa taslimu na bangi halali ina thamani ya juu ya barabarani, imekuwa chini ya majaribio na udhibiti, kwa hivyo inachukuliwa kuwa bidhaa bora na salama.
Siku chache zilizopita, alikutana na Chris Eggers, 40, askari wa zamani wa siri ambaye aligeuka kuwa mshauri wa biashara ya bangi huko Oakland.
Bw Eggers aliondoka katika jeshi la polisi zaidi ya mwaka mmoja uliopita na kuanzisha kampuni ya bangi inayozingatia usalama, ambayo inatoa ushauri wa kiusalama kwa makampuni ya bangi kote Marekani.
Anasaidia biashara chache za usawa wa kijamii kama ya Bw Nelson bila malipo.
Aligundua kwamba uzoefu wake wa kujipenyeza kwenye magenge ya wahalifu ulimpa ufahamu juu ya aina za udhaifu ambao majambazi wenye silaha hutafuta.
Lakini wizi ni mwanzo tu wa tatizo kwa biashara nyingi za bangi. Bw Nelson bado anasubiri malipo ya bima yake ya bangi - jambo la kawaida, kulingana na Bw Eggers.
Bima ya bangi mara nyingi ni ngumu na sio rahisi kuelewa kwamba wamiliki wa biashara ya Usawa wa Jamii mara nyingi hupata majibu hasi kutoka kwa bima kuhusu madai yao, alisema.
"Ujambazi hakika unaumiza, lakini ni matokeo ambayo yanaua biashara hizi," Bw Eggers alisema.
Biashara ya familia
Tatizo jingine kwa wapokeaji wa Usawa wa Kijamii ni mapambano ya kuhama kutoka bangi haramu hadi halali.
Linda Grant, 53, anaishi katika kitongoji cha wafanyikazi wa makazi mashariki mwa Oakland na familia yake.
Amekulia katika mazingira ya watu wanaotumia na kuuza bangi maisha yake yote. Alianza kuivuta alipokuwa na umri wa miaka 11 na alianza kuuza bidhaa hiyo shuleni alipokuwa na umri wa miaka 13.
Alipata mamia ya dola kwa wiki kutokana na uuzaji wa bangi kinyume cha sheria na alikamatwa mara kadhaa, lakini aliacha kuuza baada ya kupata watoto.
Miaka kadhaa baadaye, alisikia kuhusu mpango wa Usawa wa Kijamii na akaamua kuwa hii ilikuwa njia yake ya kurudi kwenye tasnia ya bangi.
Alisema anataka iwe biashara ya familia na kuwashirikisha watoto wake wakubwa, na kwamba anaona mpango huo kama njia ya fidia.
Lakini kufanya kazi katika soko haramu la bangi hakukumtayarisha kwa urasimu katika ule wa kisheria.
"Hilo ndilo jambo gumu zaidi - kulazimika kufuata sheria kutoka kuwa mvunja sheria hadi mtu anayezingatia sheria," alisema.












