Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 04.08.2023

Harry Maguire

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Beki wa Manchester United na Uingereza Harry Maguire
Iliyochapishwa

Everton wamewapiku Tottenham na West Ham katika mbio za kumsajili beki wa Manchester United na Uingereza Harry Maguire, 30. (Football Insider)

Meneja wa Wolves Julen Lopetegui anatafakari kuhusu nafasi yake kama kocha wa klabu ya Midlands. (Mirror)

Chelsea na Manchester City wanaongeza juhudi zao za kumsajili winga wa Crystal Palace Mfaransa Michael Olise,21, huku kukiwa na mkanganyiko kuhusu kipengele cha kutolewa katika mkataba wa Eagles . (Mirror)

Paris St-Germain wanakaribia kumpata mshambuliaji wa Benfica na Ureno Goncalo Ramos mwenye umri wa miaka 22 kwenye klabu hiyo. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Michael Olise

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chelsea na Manchester City waongeza juhudi za kumsajili winga wa Crystal Palace Mfaransa Michael Olise

Clement Lenglet anapinga mpango wa Barcelona wa kumuuza kwa klabu ya Saudia ya Al-Nassr - huku beki huyo wa Ufaransa, 28, akidhamiria kurejea Tottenham, ambako alicheza kwa mkopo msimu uliopita. (Sport - kwa Kihispania)

Matumaini ya Chelsea kubadilishana mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, na mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 23, katika mkataba wa mchezaji pamoja na pesa, yanalemazwa na matakwa ya wababe hao wa Italia ya kutaka ada ya pauni milioni 35. (Star)

Manchester United wanafuatilia kiungo wa Bayern Munich na Ujerumani Leon Goretzka, 28, ambaye tetesi zinadai ''hayuko'' katika mipango ya kocha Thomas Tuchel. (Mail)

Lukaku

Chanzo cha picha, Getty Images

Aston Villa wako tayari kutumia kipengele cha kuachiliwa kwa kiungo wa Leeds United Tyler Adams, 24, cha pauni milioni 25 na wanasubiri jibu kutoka kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani kuhusu mustakabali wake, huku Chelsea pia wakifikiria kumnunua. (Mail)

Tottenham wanajadili kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Argentina mwenye thamani ya pauni milioni 12 Alejo Veliz, 19, kutoka Rosario Central - na wanatazamia kuwatoa kipa wa Ufaransa Hugo Lloris, 36, kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 27, Mfaransa Tanguy Ndombele, 26, na winga wa Uhispania Bryan Gil, 22. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 26, atafanyiwa vipimo vya afya siku ya Ijumaa kabla ya kukamilisha uhamisho kutoka Barcelona kwenda Paris St-Germain. (RMC Sport - kwa Kifaransa)

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

West Ham na Nottingham Forest wanamwinda mshambuliaji wa PSG mwenye umri wa miaka 21 Mfaransa Hugo Ekitike. (RMC Sport, via Mail)

Mpango wa West Ham kumnunua kiungo wa kati wa Southampton James Ward Prowse umetibuka huku mkurugenzi wa ufundi wa Hammers Tim Steidten akipinga kumleta mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 28, ambaye anasakwa na kocha David Moyes. (Guardian)

Southampton wanatarajiwa kufufua nia yao ya kumsajili beki wa Norwich, Max Aarons, 23, ili kuziba pengo la Tino Livramento anayekipiga Newcastle. (Talksport)

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Burnley wameanzisha mazungumzo kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Denmark Mohamed Daramy, 21, kutoka Ajax. (Fabrizio Romano)

Bournemouth wako tayari kumsajili kiungo wa kati wa Italia Gaetano Castrovilli mwenye umri wa miaka 26 kutoka Fiorentina kwa euro 12m pamoja na nyongeza. (Sky Sports Italia)

Kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie, 26, anakaribia kuhamia Al-Ahli ya Saudi Arabia kwa pauni milioni 12.9 kutoka Barcelona. (Athletic - Usajili unahitajika)