Vita vya Ukraine: Wapiganaji wa Ukraine walilia vifaru vya Magharibi

Chanzo cha picha, Joe Phua
Huku Uingereza na mataifa mengine ya Ulaya yakijiandaa kutuma vifaru nchini Ukraine ili kusaidia kukomboa maeneo zaidi yanayoshikiliwa na Urusi, mwandishi wetu Andrew Harding amekuwa akiwatembelea wanajeshi wa kitengo cha vifaru cha Ukraine ambacho tayari kinakabiliana na vikosi vya Urusi karibu na miji inayozozaniwa vikali ya Bakhmut na Soledar.
Milipuko husikika kila baada ya sekunde chache, wakati mwingine katika makundi ya kasi ya milipuko sita au zaidi, wakati mwingine ya mikubwa na mirefu, ikivuma kwenye milima iliyo ya theluji karibu na Bakhmut na Soledar.
Hii hutokea kila siku, na mara kwa mara, kwenye vita huko Donbas, ambapo mizinga ya Kiukreni na Kirusi, roketi na vifaru vikipambana katika mapambano makali, lakini kwa kiasi kikubwa ambayo hayajakamilika ili kuvunja msuguano wa miezi kadhaa.
"Tuna lengo," Roman, kamanda wa kitengo cha vifaru wa Ukraine alisema, ghafla akivua glavu zake, akipanda juu ya kifaru, (T-72) kinachoteleza, kilichofunikwa na theluji , na kujaribu kufungua tundu lenye chuma nzito.

Chanzo cha picha, Joshua Pua
Mpiganaji mwingine, Vlad, alitokea, ili kusaidia. "T-72 ni vifaru vya zamani - huyu ana umri sawa na mimi," alisema Bogdan, mwanajeshi wa kujitolea wa Ukrain mwenye umri wa miaka 55, akigeukia na kuipapasa kifaru hicho kikubwa cha enzi ya Sovieti.
"Nilikuwa nikiendesha kifaru kama hiki karibu miaka 40 iliyopita - siwezi kuamini kuwa ninaifanya tena. Lakini inasaidia. Inafanya kazi." "Lakini Leopard(aina nyingine ya kifaru) itakuwa bora," Volodymr, mpiganaji mwingine anasema, na kucheka chini kwa chini.
Mipango ya kuleta vifaru vya mizinga ya Leopard iliyotengenezwa Ujerumani na Challengers ya Uingereza kuja hapa Donbas imepokelewa kwa msisimko mkubwa unaoonekana na vikosi vya Ukraine, ambavyo vimekuwa vikipata hasara kubwa katika wiki za hivi karibuni, karibu na Bakhmut, na, haswa, wakati wa mapigano makali ya mji wa karibu wa Soledar.
"Kulikuwa na hasara kubwa sana. Inasikitisha sana. Ni ngumu," alisema Danylo, afisa anayehusika na ukarabati wa vifaru vya Kikosi cha 24 cha Mitambo. hiyo.
Alisema mkwamo uliopo hautavunjwa isipokuwa vifaru vya kigeni vifike kwa wingi. "Ndiyo, tutakwama hapa. Tunahitaji [vifaru vya Magharibi] ili kukomesha uvamizi wa Urusi. Kwa askari wa miguu, wenye silaha za kutosha, tutashinda kwa hakika," alisema.
"Leopards, Challengers, Abrams - kifaru chochote cha kigeni ni kizuri kwa ajili yetu! Nadhani tunahitaji angalau vifaru 300. Na tunahitaji sasa!" Alisema Bogdan. Waukraine wote walikiri kwamba Urusi ilikuwa na vifaru vya kisasa zaidi lakini walikuwa wanakashifu kuhusu mbinu zao.
Kamanda muandamizi wa kikosi hicho cha 24, alitutembeza kwenye vifaru vilivyofichwa msituni tayari kwa mapambano

Chanzo cha picha, Joshua Pua
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"T-72 hizi vimeonekana kuwa na ufanisi katika hali ya majira ya baridi. Lakini ni vya zamani, na hazifai kabisa kwa vita vya kisasa. Siku hizi ni kutumia ndege zisizo na rubani na teknolojia nyingine za kisasa." Khan alisema anaamini itachukua muda mfupi sana kwa wafanyakazi wake kuzoea vifaa vya kisasa zaidi vya Ulaya.
"Ikiwa wewe ni dereva wa vifaru tayari wewe ni uko na uweledi wa juu ya wastani. Wataweza kujifunza na kukabiliana haraka," alisema.
Vita nchini Ukraine, kwa njia nyingi, vimekuwa dhahiri ni mzozo wa kizamani, uliojikita kwenye ugomvi, mashambulizi mabaya ya risasi, na maeneo ya kuchimbwa yanayokumbusha mahandaki ya Vita vya Kwanza vya Dunia.
Lakini vita pia vimefichua ukomo wa vifaru - kwa uwazi zaidi katika wiki za kwanza za vita wakati askari wa miguu wa Ukraine walipoharibu nyenzo nyingi kubwa za kivita za Urusi kwa roketi za begani.
"Katika siku za zamani, kila kitu ilikuwa kuhusu mizinga. Sasa ni kuhusu mifumo hii mipya ya roketi," alisema Volodymr. Lakini miezi ijayo bado inaweza kushuhudia makombora ya Magharibi - ikiwa itatumwa haraka, na kwa idadi kubwa - kusaidia jukumu muhimu.









