Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 12.03.2024

Chanzo cha picha, Getty images
Manchester United Itagharamika zaidi ya pauni milioni 10 iwapo itamfuta kazi meneja Ten Hag na wakufunzi wake. (Times - Subscription Required)
United wataendelea na mpango wa kumnunua Branthwaite, ambaye thamani yake ni pauni milioni 75 na Everton, bila kujali mustakabali wa kocha Erik ten Hag. (Mirror)
Dortmund wana nia ya kumbakisha Sancho na wanaweza kutafuta makubaliano ya kubadilishana na United, ambayo yatamfanya mshambuliaji wa Uholanzi Donyell Malen, 25, kuhamia Old Trafford. (Fichajes - kwa Kihispania)

Chanzo cha picha, Reuters
Manchester United wamemfanya mlinzi wa Everton wa England chini ya umri wa miaka 21 Jarrad Branthwaite, 21, kuwa shabaha yao kuu ya uhamisho wa majira ya joto. (Star)
Winga wa Crystal Palace Mfaransa Michael Olise, 22, pia yuko juu kwenye orodha ya ya United ya majira ya joto. (Football Transfers)
Everton wanamtaka beki wa Hull City Muingereza Jacob Greaves, 23, ambaye anatarajiwa kuhamia Ligi ya Premia msimu huu wa joto ikiwa klabu hiyo ya Championship itakosa kupanda daraja. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City inachunguza kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle Mbrazil Bruno Guimaraes, 26, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 100 katika kandarasi yake. (Football Transfers)
Tottenham wameungana na Manchester City, Liverpool, Newcastle na Arsenal kwa matumaini ya kumsajili winga wa Ureno Pedro Neto, 24, kutoka Wolves msimu huu wa joto. (Football Insider)
Meneja anayeondoka Jurgen Klopp amependekeza Liverpool imsajili beki wa kushoto wa Algeria Rayan Ait-Nouri kutoka Wolves, ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 pia yuko kwenye rada za Manchester United. (TeamTalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Roma, Tiago Pinto, ambaye alifanya kazi na kocha Jose Mourinho katika klabu hiyo ya Italia, anasema ana nia ya kumrithi Dan Ashworth anayejiunga na Manchester United huko Newcastle. (i Sport - usajili unahitajika)
Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, hana hamu ya kurejea Manchester United baada ya muda wake wa mkopo katika klabu ya Borussia Dortmund huku akimlaumu meneja Erik ten Hag kwa kuvuruga maisha yake ya soka. (Bild, via 90min)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa pembeni wa Ureno Joao Cancelo, 29, amethibitisha kuwa anatarajia uhamisho wake wa mkopo kutoka Manchester City kwenda Barcelona ukikamilika msimu huu. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Chelsea ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia kiungo wa kati wa klabu ya FC Nordsjaelland ya Denmark Mario Dorgeles, 19. (Tipsbladet - kwa Kidenmark)
Tottenham wako tayari kumruhusu mlinzi wa Wales Joe Rodon, 26, kuhamia Leeds United msimu huu wa joto baada ya kuwa kwa mkopo katika klabu hiyo ya Championship msimu huu. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












