Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 11.06.2024

''

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Chelsea wamefikia makubaliano ya kibinafsi na winga wa Ufaransa wa chini ya umri wa miaka 21 Michael Olise, 22, na wanatazamiwa kupanga malipo ili kutimiza masharti yake ya kuondoka Crystal Palace. (Givemesport)

Fulham inakadiria thamani ya kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28, kuwa mara mbili ya dau la pauni milioni 30 lililowasilishwa na Bayern Munich. Barcelona na Manchester United pia wanavutiwa na Palhinha. (Sky Sports)

Manchester United na Tottenham wanatarajiwa kumenyana katika kinyang'anyiro cha usajili wa winga wa Crystal Palace na Uingereza Eberechi Eze, 25. (Football Insider)

''

Chanzo cha picha, Getty Images

West Ham ni miongoni mwa klabu zinazowania kumsajili beki wa Argentina Nehuen Perez, 23, kutoka Udinese. (Gianluca Di Marzio)

Brighton wanatarajia kumtangaza Fabian Hurzeler, ambaye aliiongoza St Pauli kupanda daraja hadi Bundesliga mwezi uliopita, kama kocha wao mpya wiki hii. (Guardian)

Bayern Munich wanavutiwa na mlinzi wa Chelsea Levi Colwill, 21, na mazungumzo ya awali ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza tayari yamefanyika. (Sky Germany)

Atletico Madrid wamefufua nia yao ya kumnunua kiungo wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg mwenye umri wa miaka 28 baada ya uhamisho wa pauni milioni 15 kutoka Tottenham kugonga mwamba msimu uliopita. (mail)

Leicester wamemtambua mkufunzi wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter kama mrithi wa Enzo Maresca lakini pia wanafikiria walengwa wengine akiwemo Steve Cooper. (Guardian)

Pierre-Emile Hojbjerg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg

Crystal Palace wanatazamiwa kumsajili kiungo wa kati wa Japan Daichi Kamada kwa uhamisho wa bure baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye alichezea Lazio msimu uliopita, kukamilisha hatua ya kwanza ya uchunguzi wa kimatibabu. (Fabrizio Romano)

Sporting Lisbon wanavutiwa na winga wa Wolves Chiquinho, 24, na wako tayari kulipa ada ya takriban euro milioni 10 (£8.45m) kwa mchezaji huyo wa Ureno. (O Jogo - kwa Kireno)

Chelsea wamefikia makubaliano ya kibinafsi na beki wa Brazil Pedro Lima, 17, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza katika klabu ya Sport Recife mwezi Januari. (HITC)

Luiz

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Juventus wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Brazil na Aston Villa Douglas Luiz

Juventus wanajiandaa kuzungumza na Aston Villa hivi karibuni kuhusu mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, lakini uhamisho huo unaweza kutokea iwapo tu mchezaji atahama kutoka klabu hiyo ya Italia kwenda Villa. (Fabrizio Romano)

Ipswich iko tayari kuchuana na Besiktas ya Uturuki kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Rangers na Wales Tom Lawrence, 30. (Mail)

Manchester United wamepewa nguvu katika harakati zao za kumsaka kiungo wa kati wa Benfica na Ureno Joao Neves, 19, ambaye amekataa ofa ya kandarasi kutoka kwa klabu hiyo ya Ureno. (Record - kwa Kireno - usajili unahitajika)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi