Tetesi za soka Jumamosi: Man United yataka £52mil kwa Hojlund

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United wameweka bei ya kumnunua Rasmus Hojlund, Manchester City wamejua kima cha kumnunua Morgan Gibbs-White, huku Real Madrid wakisubiri kwanza kabla ya kuwa na mkataba na William Saliba.

Manchester United itakubali tu ofa za £52m (euro milioni 60) kwa mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, huku Juventus ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Tuttomercatoweb - in Italian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City italazimika kulipa £100m ikiwa wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Nottingham Forest na Uingereza Morgan Gibbs-White, 25, msimu huu wa joto. (Talksport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid watasubiri kwanza katika azma yao ya kuwa na mlinzi wa Arsenal Mfaransa William Saliba, 24 - wakilenga kuwa naye mkataba kwa gharama ya kima cha chini mwaka 2026 au uhamisho wa bure mkataba wake utakapokamilika 2027. (Athletic - subscription required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkufunzi wa Manchester United Ruben Amorim atafanya mazungumzo 'kuondoa mashaka' na mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford msimu huu wa joto ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hatasaini mkataba kabisa na Aston Villa. (Daily Star)

Manchester City wanaendelea na mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa kiungo wa kati wa England chini ya umri wa miaka 20 Nico O'Reilly, baada ya Chelsea kuonyesha nia ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 mwezi Januari. (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Inter Miami wanakaribia kufikia makubaliano na mshambuliaji mkongwe wa Argentina Lionel Messi, 37, kuhusu kuongezwa kwa mkataba ili abaki na klabu hiyo ya MLS. (Athletic - subscription required)

Tottenham Hotspur wanafikiria kufanya kuwa wa kudumu uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Bayern Munich na Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Mathys Tel, 19, lakini hawako tayari kutimiza kipengele cha chaguo la kununua cha euro 50-55m (£43m-£47m) katika mkataba huo. (Florian Plettenberg)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United, Newcastle, Arsenal, Aston Villa, Nottingham Forest na Tottenham wote wanawinda kumpata mshambuliaji wa Wolves na Brazil Matheus Cunha, 25 . (Daily Mail)

Kiungo wa kati wa Real Betis Sergi Altimira, 23, atatia saini mkataba mpya hadi 2029, licha ya Manchester City kutaka kumnunua Mhispania huyo, ambaye mkataba wake utakuwa na kipengele cha kumnunua cha euro 60m (£51.9m). (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, EPA

Beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk, 33, amekubali masharti ya mkataba mpya na klabu hiyo ambao atasaini nao mkataba kabla ya mwisho wa msimu huu. (Fabrizio Romano)

Imefasiriwa na Asha Juma