'Kiti changu cha magurudumu hakitanizuia mashindano ya kuendesha gari'

Mtumiaji wa kiti cha magurudumu Nikhil Sachania (kushoto) akishindana kama dereva  sambamba na Deep Patel (kulia)

Chanzo cha picha, KCB BANK KENYA

Maelezo ya picha, Mtumiaji wa kiti cha magurudumu Nikhil Sachania (kushoto) akishindana kama dereva sambamba na Deep Patel (kulia)
Iliyochapishwa

"Niligonga shimo na gari likanirushkurushwa nje ya usukani. Nilianguka na uti wa mgongo wangu ukapinda," anakumbuka Nikhil Sachania. "Hapo ndipo ulipovunjika."

Dereva huyo wa kwanza wa Kenya mlemavu wa miguu hakuwahi kufikiria kuhusu kuacha mchezo wa magari licha ya jeraha lililobadilisha maisha. Badala yake, Sachania ataanza tena kushiriki mashindano ya magari ya langalanga ya Safari Rally yanayotarajiwa kuanza mjini Nairobi Alhamisi.

Tukio hili, linachukuliwa kama mojawapo ya mashindano magumu zaidi duniani, ni la sita katika mashindano ya dunia ya magari na ni shindano pekee la aina yake linalofanyika katika Afrika.

"Hakikuwa kisa cha 'Hii imetokea kwasababu ya mchezo wa magari, na ninahitaji kuzuwia hili'," Sachania mwenye umri wa miaka 33 aliiambia BBC michezo Afrika.

"Imenifanya nifikirie njia nyingine, ambazo ninaweza kuzitumia kuendelea. "Na nina uhakika kwamba hilo linawatia moyo watu kuendelea kusonga mbele pia. Nina matumaini wanafikiria jinsi ninavyofikiri - kwamba kama anaweza kufanya hili, ninaweza kufanya kitu fulani. Sio lazima iwe lazima kushiriki katika mashindan ya magari ya langalanga."

Mapenzi ya mchezo huu wa magari ya Sachania yalianza tangu alipokuwa na umri mdogo, alipokuwa akimtazama baba yake akishindana katika mashindano ya washindi ya magari.

"Nilikuwa nikienda nje na kumsaidia kama fundi wa gari mvulana mdogo , na kuelewa tu kuhusu mashindano ya langalanga ," anasema.

'Sikuweza kuihisi miguu yangu'

Wakati alipokuwa kijana mdogo Sachania tayari alikuwa ameanza kupenda matukio ya mchezo wa magari, lakini alipokuwa na umri wa miaka 22 alipata ajali alipokuwa akifanya mazoezi katika gari la mataili makubwa ambayo ilitishia mapenzi yake ya mchezo.

"Baada ya kupata ajali, nilikuwa makini sana," Sachania anakumbuka. "Niligundua kitu fulani hakikuwa sawa miguuni mwangu lakini kwa kuwa nilihisi ongezeko la msukumo wa damu ,sikuhisi kuwa hali ilikuwa mbaya. "Kichwani mwangu, nilikuwa tu ninafikiria, 'Oh baba yangu ataniua. Atakasirika'."

Sachania alipelekwa katika hospitali mjini Nairobi kufuatia ajali hiyo, lakini hawakuwa na vifaa muhimu vya kufanya operesheni iliyohitajika. Alihamishiwa katika hospitali nchini India ambako madaktari walithibitisha kuwa hataweza kutembea tena.

Sachania anasema katika baadhi ya siku wakati alipokuwa akitibiwa jeraha la mgongo lilimuelemea

Chanzo cha picha, Other

Maelezo ya picha, Sachania anasema katika baadhi ya siku wakati alipokuwa akitibiwa jeraha la mgongo lilimuelemea
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Baada ya kufanyiwa upasuaj, niligusa miguu yangu na sikuweza kuihisi. Ilikuwa kama nimegongwa na lundo la matofali ," Sachania anaeleza. "Mtu fulani alinisaidia kuwa tayari, mtu fulani alinisaidia kuoga, mtu fulani alinisaidia kwenda choo na halafu nilihitaji mtu wa kunisukuma kwenda kufanyiwa mazoezi ya viungo, kujaribu na kujifunza jinsi ya kurejea katika maisha ya kawaida.

"Ilikuwa ni muhimu, hususan hiyo miezi michache ya kwanza, kuelewa kwamba ndio, maisha yangu yamebadilika, lakini kuna njia ya kuishi bado maisha ya kawaida ."

Kwa Sachania, kuendelea kuwa na mtizamo chanya ilikuw amuhimu ingawa kwa taktiban miezi minane ya kupona, lakini kulikuwa na siku ambazo alihisi kuwa nzito kwake.

"Katika siku zangu ngumu, iinakuwa ni kwa mfano; Sitaki kuongea na mtu yeyote, sitaki kwenda kufanyiwa matibabu, sitaki tu kuamka ," anasema. "Ninataka tu kuketi, ninataka tu kullala. Zilikuwa siku ngumuhizo siku chache za mwanzoni.

"Lakini ni lazima ujikaze. Nilikuwa na familia kubwa na marafiki wengi, kwahiyo nimekuwa na watu wengi wanaonizingira ambao walinitia moyo.

Kurejea katika mashindano ya magari - na udhibi wa mkono

Sachania na Patel walishikilia nafasi ya 21 katika Safari Rally Kenya mwaka jana

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sachania na Patel walishikilia nafasi ya 21 katika Safari Rally Kenya mwaka jana

Mwaka 2014, miaka mitatu baada ya ajali , Sachania alikuwa amerudi kwenye usukani - mara hii katika gari la mashindano lililofanyiwa ukarabati kulingana na ulemavu wake. "Kilikuwa ni moja ya vitu vilivyonisisimu sana nilivyowahi kufanya," anakumbuka.

"Nilipoanza kwanza, ilikuwa rahisi sana kudhibiti kwa mkono katika uendesheji wangu wa gari wa kawaida. Na katika gari langu la kwanza la mashindano, nilikuwa nimeweka ukarabati rahisi wa kusukuma na kudhibiti. "Nilikuwa naendesha kwa mkono mmoja kwenye usukani na mkono mwingine nikiutumia kubadilisha gia na kushika breki. Siku mbili za kwanza kidogo zilikuwa ngumu lakini nilipozowea, lilikuwa ni jambo la kawaid . "Katika sula ya kukata kona na kufuata muda, hilo linakuja na mazoezi na uzoefu."

Tangu wakati huo Sachania amefuzu katika matumizi ya gari linalodhibitiwa kwa mkono ambalo anaona ni rahisi kulitumia zaidi, kwa usaidizi wa Deep Patel.

"Mara nyingine huwa ninaketi tu nikimtazama jinsi anavyocheza na usukani . Inafurahisha sana," Patel, ambaye aliunda timu moja na Sachania miaka mitatu iliyopita.

"Ni mtu ambaye nimejifunza makubwa kutoka kwake . Watu wengine hawawezi kuamini kuwa mtu katika kiti cha walemavu kama Nikhil anakimbiza gari, inashangaza sana." Uhusiano wao wa dereva na muongozaji ni wa kipekee kwasababu ya ulemavu wa Sachani.

"Kwangu mimi, kipaumbele changu ni yeye, hata iwe vipi," Patel anaelezea. "Katika mashindano yaliyopita, moshi ulitokea ndani ya gari. Nilisema egesha gari upande wangu kwahiyo ikatoa nafasi kwa upande wake ili kama anaweza kuruka nje au kama ninaweza kumbeba nje.

''Hayo ni mambo ambayo tunafikiria kuyahusu kila mara . kama tutapata pancha, ni mimi ninayebadili gurudumu. Ninachukua jukumu la kufanya kila kitu ."

Kuwa na mtizamo chanya

Sachania na  Patel, wakipokea tuzo mwaka 2019, wameshindana pamoja kwa miaka mitatu

Chanzo cha picha, Other

Maelezo ya picha, Sachania na Patel, wakipokea tuzo mwaka 2019, wameshindana pamoja kwa miaka mitatu

Mwaka huu wawili hao watakuwa miongoni mwa magari 15 yanayoshindana katika kitengo cha taifa katika shindano la mwaka huu la Safari Rally, bada ya kushikilian nafasi ya 21 mwaka jana.

Sachania anatumai kuendela kushiriki kwake katika mashindano ya aina hiyo kunaweza kuwa mfano wa kuigwa na wengine, hata kama sio kila mtu anayefahamu kinachomchochea kuendesha gari la mashindano baada ya ajali. "Ninaona jinsi watu wanavyofurahia wanaponiona, hasa pale ninaporuka nje ya gari na watu kugundua niko katika kiti cha magurudumu ," alisema.

"Watu wengi humiuliza 'Unawezaje kuendesha?' na ninasema inafurahisha.Na halafu unapata upande mwingine wa wanaosema: 'Una wazimu? Kwanini unafanya hivi?Ulipata jeraha ndani ya gari la michezo '. "Ninazuia yote hayona kujaribu kupokea mawazo yote yaliyo chanya kadri niwezavyo ."

Sachania amekataa kuruhusu ajali kuelezea nini anachoweza kufanya na asichoweza kufany, na kuhakikisha anafurahia uzoefu mbali mbali wa maisha yake.

"Nimeisha cheza michezo ya kurupwa kwa kamba kutoka angani. Mimi ni dereva kwenye kibali. Ninashindana katika mashindano ya magari. Ninakwenda kufanya kazi. Yote hayo. Sijawahi kuwa na wasi wasi pale ninapokuwa na kitu ninachoweza kufanya katika kitu ninachokifanya ."

Unaweza pia kusoma: