Kijusi chapatikana katika tumbo la mtoto wa miezi 10

dsa

Chanzo cha picha, SHEIKH ZAYED MEDICAL COLLEGE

Maelezo ya picha, Shazia, kichanga wa miezi 10
Iliyochapishwa

Onyo: Taarifa hii inaweza kukushtua

Dkt. Mushtaq Ahmed alishtuka alipokuwa akimfanyia upasuaji wa tumbo Shazia mwenye umri wa miezi kumi, ili kutoa kile kilichoonekana ni tishu za uvimbe.

Aliona miguu iliyoharibika tumboni mwa mtoto. Hakuwahi kuona kitu kama hicho hapo awali.

“Tunatafuta uvimbe kwenye tumbo la mtoto ambaye amekuwa akilia kwa maumivu kwa miezi kadhaa. Hata hivyo, tulishangaa kuona vidole vya miguu na mgongo kwenye tumbo lake. Kwa dakika moja hatukuelewa ni nini," alisema.

"Sijawahi kuona kesi kama hii katika kazi yangu ya miaka 15 kama daktari wa watoto," alisema.

Dkt. Mushtaq anasema kilichomo tumboni mwa Shazia ni kijusi cha pacha wake. Kijusi kilichoacha kukua katika wiki ya nane au tisa.

"Tuliona umbo la miguu na mikono. Hata vidole. Macho yako nusu," Mushtaq anasema.

Upasuaji huo ulifanyika katika Hospitali ya Sheikh Zayed huko Rahim Yarkhan, Punjab, Pakistan.

Kijusi tumboni mwa mtoto

d

Chanzo cha picha, AFP

Hiki ni kijusi tumboni mwa mtoto. Hali hii hutokea katika hatua za mwanzo za maendeleo ya kijusi. Pale kiinitete kimoja kinapofunikwa na kiinitete kingine.

Kiinitete cha ndani hakikui vizuri. Kinakuwa kimelea myonyaji (parasite). Kinategemea kiinitete kikuu kwa ajili ya kuishi. Lakini, mapacha wa aina hiyo kawaida hufa wakati wa kuzaliwa.

Ripoti ya Chuo cha Marekani cha Madaktari wa Watoto ya mwaka 2000 ilifichua kwamba, mikasa hii hutokea katika kisa kimoja kati ya kila watoto 5,00,000 wanaozaliwa.

Kulia sana

kllk

Chanzo cha picha, SHEIKH ZAYED MEDICAL COLLEGE

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tumbo la Shazia lilikuwa kubwa tangu mwezi wa kwanza wa kuzaliwa. Wazazi wake wanasema alikuwa akilia kwa muda mrefu kutokana na maumivu makali.

“Hatuelewi tatizo hasa ni nini. Lakini tumbo lilikuwa limekaza,” babake Shazia, Mohammad Asif anasema.

Anafanya kazi ya kuchunga ng'ombe mashambani. Akiwa na mke wake na watoto wengine wawili, Shazia alipelekwa katika hospitali kadhaa za Sadiqabad. Kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya matibabu, hawakujua tatizo ni nini.

Huku afya ya Shazia ikizidi kuzorota, Afar aliamua kumpeleka katika hospitali ya Sheikh Zayed mjini Yarkhan, kilomita 30. Saa chache baadaye walikutana na Dokta Mushtaq.

“Baada ya kuuchunguza mwili wa mtoto huyo, ilishukiwa kuwa ana uvimbe tumboni. Mara moja tulifanya vipimo. Kisha kitu kama uvimbe kilionekana kwenye tumbo. Sikuwahi kufikiria kuwa ingekuwa kijusi," anasema.

Familia haikuweza kumudu kipimo cha MRI. Ambacho kingetusaidia kujua vizuri zaidi kilicho ndani ya tumbo. Mushtaq aliwaambia wazazi wa mtoto huyo kwamba wataondoa uvimbe huo kwa upasuaji.

“Waliposikia hivyo, walipata hofu kidogo. Hawakuelewa kwa nini mtoto mdogo kama huyo angefanyiwa upasuaji," aliongeza.

Hata hivyo, wazazi wa Shazia awali hawakukubali kufanyiwa upasuaji huo. Wakamrudisha nyumbani.

Hata hivyo, baada ya siku chache walirudi tena. Afya ya mtoto huyo ilipozidi kuzorota, hawakujua la kufanya.

"Wao ni familia masikini. Ndiyo maana tulifikiria kuwasaidia kwa upasuaji,” anasema Dkt. Mushtaq.

Siku ya upasuaji Agosti 29, Dkt. Mushtaq alishituka baada ya kuona kijusi hicho kikiwa kimeumbika vizuri kwenye tumbo la Shazia, waligundua kuwa itahitaji upasuaji mgumu sana kukiondoa.

“Tulishangaa kukuta kijusi kikiwa kimeharibika tumboni mwa mtoto huyo mwenye utapiamlo,” alisema Mushtaq.

Kiinitete kinakuwa vimelea vinyonyaji na huchukua damu na virutubisho kupitia utumbo. Matokeo yake, Shazia hapati virutubisho vya kutosha.

Dkt. Mushtaq alisema kuwa Shazia anaendelea kupata nafuu baada ya upasuaji na afya yake inaendelea vizuri kwa sasa.

“Sasa kilio cha mtoto kimepungua. Baada ya upasuaji huo, afya yake pia iliimarika,” aliongeza.

Alirudishwa nyumbani kutoka hospitalini Septemba 4, siku nne baada ya upasuaji. Maelezo ya kesi yake yalichapishwa katika jarida la sayansi.

Mtoto hana ujauzito

kk

Chanzo cha picha, SHEIKH ZAYED MEDICAL COLLEGE

Maelezo ya picha, Muhammad Asif, baba wa mtoto

Kwa kuwa ni jambo la nadra sana, kumekuwa na shauku kubwa ya vyombo vya habari. Hata hivyo, baba yake Shazia alishindwa kujibu baadhi ya maswali na akazima simu yake.

“Magazeti na vituo vya televisheni vinauliza ikiwa ni mimba ya mtoto. Hatuwezi kujibu maswali kama haya," alisema.

Timu ya hospitali hiyo ilisema kuwa waandishi wa habari wa eneo hilo walipewa taarifa za wazi kuhusiana na suala hili.

Dkt. Nadeem Akhtar, mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Watoto katika Taasisi ya Pakistani ya Sayansi ya Tiba (PIMS), Islamabad, alisema kuwa kuna haja ya kusema wazi kwamba kijusi ni kijusi na hakihusiani na ujauzito.

“Waandishi wengi wa habari hawaelewi hili. Kutokana na hali hiyo, wazazi wa mtoto huyo wanasumbuliwa,” alisema.

Kisa chengine India

sdxz

Chanzo cha picha, MUSHTAQ AHMED

Maelezo ya picha, DKT. MUSHTAQ AHMED

Kesi kama hiyo imetokea nchini India pia. Tumbo la mwanamume mwenye umri wa miaka 36 lilikuwa limepanuka kiasi kwamba ilikuwa vigumu kwake hata kupumua.

Madaktari walidhani uvimbe unaweza kuwa unakua tumboni mwake kutokana na maumivu makali ya tumbo. Katika vipimo vilivyofanyika, ilibainika kuwa alikuwa na kijusi tumboni mwake.

Kijusi hicho kilibaki kama kimelea kwa miaka mingi. Kinachukua damu kutoka kwa mtu kupitia mirija kama kitovu.

Madaktari wanasema katika vijiji na miji midogo ambako vifaa vya matibabu ni duni, kuna uwezekano wa vijusi vilivyoharibika vikawepo kwenye matumbo ya baadhi ya watu.