Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 14.03.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jamal Musiala
Iliyochapishwa

Chelsea wako tayari kupata ada nzuri ikiwa Bayern Munich itakubali kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Jamal Musiala, ambaye anahusishwa na uhamisho wa pauni milioni 80 kutoka kwa wababe hao wa Bundesliga, huku Manchester City na Liverpool wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Mail)

Chelsea wamefikia makubaliano na Brentford kumsajili Bernardo Cueva kuwa kocha wao mpya kuanzia mwisho wa msimu huu. (Athletic -Usajili unahitajika)

Rashford

Chanzo cha picha, Getty Images

Paris St-Germain wanatayarisha dau la pauni milioni 80 kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, na watakuwa tayari kumlipa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 takriban pauni 500,000 kwa wiki. (Star)

PSG pia wanavutiwa na winga wa Liverpool Mcolombia Luis Diaz, 27, kama mbadala wa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe, 25, ambaye anatarajiwa kujiunga na Real Madrid. (El Pais - kwa Kihispania)

Mwenyekiti wa Chelsea Todd Boehly yuko tayari kuwauza mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, ambaye yuko Roma kwa mkopo, na kipa wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 29, ambaye yuko kwa mkopo Real Madrid, kwa vilabu vya Saudi Pro League majira ya joto katika jaribio la kuongeza pauni milioni 100 kutokana na mauzo ya wachezaji. (Talksport)

Romelu Lukaku akichezea Roma

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Romelu Lukaku akichezea klabu ya Roma

Timu ya Manchester United inazuru vilabu vikubwa zaidi barani Ulaya mapema kabla ya uhamisho wa wachezaji kuanza katika juhudi za kuunda kikosi cha majira ya joto. (ESPN)

Manchester United wamepatia kipaumbele usajili wa beki wa kati msimu huu wa joto, huku mlinzi wa Juventus na Brazil Gleison Bremer, 26, akiwa juu kwenye orodha ya timu zinazomwania pamoja na mlinzi wa Everton, 21, Muingereza Jarrad Branthwaite. (i Sport)

Beki wa Liverpool Joe Gomez, 26, mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, 27, na kipa wa Rangers Jack Butland, 31, wanatazamiwa kujumuishwa katika kikosi cha England kitakachocheza dhidi ya Brazil na Ubelgiji wakati wa mapumziko ya kimataifa ya Machi. (Sky Sports)

Xavi Simons

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Paris St-Germain huenda ikamuuza kiungo wa Uholanzi Xavi Simons, 20, ambaye yuko kwa mkopo RB Leipzig, kama sehemu ya mpango wa kubadilishana mchezaji wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 29. (CaughtOffside).

Barcelona wapania kumuuza mlinzi wa Uruguay Ronald Araujo, 25, ambaye amekuwa akihusishwa na Bayern Munich, ikiwa watapokea ofa ya euro milioni 100. (ESPN)

Mtendaji mkuu wa Inter Milan Giuseppe Marotta hatarajii changamoto yoyote kati ya klabu hiyo ya Serie A na mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 26, kuongeza mkataba wake . (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Arsenal wanatazamia dili la kumnunua mlinda mlango wa Columbus Crew na Marekani Patrick Schulte, 23, iwapo kipa wa Uingereza Aaron Ramsdale, 25, ataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chelsea wako tayari kupata ada nzuri ikiwa Bayern Munich itakubali kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Jamal Musiala, ambaye anahusishwa na uhamisho wa pauni milioni 80 kutoka kwa wababe hao wa Bundesliga, huku Manchester City na Liverpool wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Mail)

Chelsea wamefikia makubaliano na Brentford kumsajili Bernardo Cueva kuwa kocha wao mpya kuanzia mwisho wa msimu huu. (Athletic -Usajili unahitajika)

Southampton watatarajiwa kumsajili mshambuliaji wa Argentina Matias Soule kutoka Juventus iwapo watapandishwa daraja hadi Ligi ya Premia, huku Crystal Palace, Newcastle United na Aston Villa pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi