Kurunzi ya Qatar 2022: Taarifa 5 kubwa jioni hii kuhusu kombe la dunia

Chanzo cha picha, Getty Images
1: Wilson kumbe alijitabiria kwa 'notebook' kwamba ataenda Qatar

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Newcastle Callum Wilson anasema alijitabiria kwa kuandika 'paki kwa ajili ya Qatar' katika ‘Notebook’ yake miezi minne kabla ya kuchaguliwa kwenye kikosi cha Gareth Southgate kitakachoshiriki Kombe la Dunia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 aliitwa katika kikosi cha wachezaji 26 cha England licha ya kutocheza mchezo wa kimataifa tangu 2019.
"Nilikuwa nikipitia ‘notebook yangu siku na sikuwa nimeitumia kwa miezi kadhaa na nilikuwa nimeandika kwenye siku ya Jumapili 'paki (kwa ajili ya safari) ya Qatar'.
"Ninaamini tu katika uwezo wa taswira na uthibitisho huo chanya. Wiki chache zilizopita, watu walikuwa wakiniuliza ninakwenda wapi wakati wa mapumziko ya majira ya baridi na niliwajibu Qatar."
2. Kauli ya Ronaldo yasahaulisha Qatar

Chanzo cha picha, Getty Images
Mashabiki na wachambuzi wameshambulia Twitter kuchagiza mjadlaa mkubwa leo baada ya Cristiano Ronaldo kusema anasalitiwa na klabu yake ya Manchester United na hamuheshimu meneja Erik ten Hag.
Mjadala leo ni Ronaldo zaidi na kufunika kiasi mijadala ya michuano ya kombe la dunia huko Qatar.
Mwandishi waliyemuhoji Ronaldo, Piers Morgan ameonekana kuonyesha kama kuna mengi zaidi katika vipande vingine vya mahojiano hayo ambavyo havijasikika.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
3. Ghana watangaza kikosi chao, Partey aongoza nyota kibao
Ghana imetangaza kikosi chake cha wachezaji 26 watakaoiwakilisha nchi hiyo kwenye fainali za kombe la dunia zinazoanza juma lijalo huko Qatar.
Thomas Partey, Denis Odoi, Tariq Lamptey, Daniel Amartey, Andre Ayew, Jordan Ayew na Inaki Williams 24 ni miongoni mwa nyota walioitwa na Kocha wa ‘The Black stars’ Otto Addo.
Wakati Ghana ikitangaza wawakilishi wengine wa Afrika, Morocco wamepata pigo, baada ya mshambuliaji wake Amine Harit kuumia kifundo cha mguu katika mchezo wa mwisho kabla ya kuelekea Qatar.
Alijumuishwa kwenye kikosi wiki iliyopita lakini sasa ataukosa michuano hiyo kwa kuumi katika mchezo wa ushindi wa Marseille wa 3-2 dhidi ya Monaco, katika ligi kuu ya Ufaransa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
4. Dua Lipa 'agoma' kutumbuiza katika ufunguzi wa kombe la dunia Qatar

Chanzo cha picha, PA Media
Dua Lipa amekanusha ripoti kwamba atatumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia la Fifa kwa Wanaume nchini Qatar Jumapili.
Mwimbaji huyo alisema "atatarajia kuzuru Qatar ikiwa imetimiza ahadi zote za kuheshimu haki za binadamu ilizozitoa" wakati ilipotangazwa kuwa mwenyeji.
Qatar imekosolewa kwa msimamo wake kuhusu mahusiano ya watu wa jinsia moja, rekodi yake ya haki za binadamu na jinsi inavyowatendea wafanyakazi wahamiaji.
Wasanii wengine wamekubali kutumbuia ikiwemo Robbie Williams na Jung Kook wa BTS.
5. Ashton United yamtaka Haaland kwa wiki sita

Chanzo cha picha, Getty Images
Inamtaka Erling Haaland kwa makubaliano ya wiki sita. Norway haijafuzu kwenda Qatar hivyo mshambuliaji huyo atasubiri kwa wiki sita kabla ya ligi kuu England na michuano mengine inayoshiriki timu yake ya Manchester City ili kurejea dimbani.
Meneja Michael Clegg alisema. "City haichezi, na tunataka kusaidia kwa kumweka sawa Erling, inaleta maana zaidi kuliko yeye kucheza gofu kwa wiki sita. "Tunafikiri atakuwa anatufaa sana, na angeingia kwenye kikosi chetu vizuri sana."














