'Naushtaki mtandao uliyoniunganisha na mnyanyasaji wangu'

Mitandao
Iliyochapishwa

Onyo: Makala hii ina mada za watu wazima.

Akiwa msichana mdogo, Alice (si jina lake halisi) aliingia kwenye tovuti maarufu ya gumzo la video la moja kwa moja, Omegle, na alioanishwa mnyanyasaji ambaye alimshurutisha kuwa mtumwa wa ngono wa kidijitali.

Takriban miaka 10 baadaye Mmarekani huyo mchanga anaushitaki mtandao wa Omegle katika kesi ya kihistoria ambayo inaweza kuwa mwanzo wa wimbi la mashtaka dhidi ya majukwaa mengine ya kijamii.

Anakumbuka mnyanyasaji wake mtandaoni alikuwa anafuatilia sana muonekano wake katika video ambazo alimlazimisha kutuma.

"Nilikuwa na umri wa miaka 11 tu, lakini alitaka nionekane mchanga kadri niwezavyo," anasema.

Hadi wa leo, nywele za Alice zikivutwa upande wa kushoto anaingiwa na kiwewe.

Leo Alice ni msichana anayejiamini mwenye umri wa miaka 21 na yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini anasema makovu ya unyanyasaji aliyopitia utasalia maishani mwake.

Mtandao
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wakati Alice alipotembelea tovuti ya Omegle kwa mara ya kwanza, tayari ilikuwa inajulikana kama sehemu ya mtandao.

"Kila mtu shuleni alijua kuhusu mtandao huo. Lakini ni wazi kwamba hakuna aliyejua ni hatari gani."

Leo mtandao huo unapata wafuatiliaji milioni 73 kwa mwezi, kulingana na wachambuzi na watazamaji wa tovuti Semrush, wengi wao kutoka India, Marekani, Uingereza, Mexico na Australia.

Kwa vijana wengine ni jambo la kawaida kuunganishwa na mtu usiyemjua katika gumzo la moja kwa moja la video ambapo lolote linaweza kutokea.

BAlice aliingia kwa Omegle peke yake nyakati za usiku, na ndipo alipounganishwa na mwanadada Ryan Fordyce kutoka Canada.

Wakati huo alikuwa akipambana na mahangaiko ya ujana na Fordyce alimfanya ajisikie vizuri. Katika mazungumzo yao ya kwanza kwa njia ya video ya moja kwa moja alimshawishi kushiriki maelezo ya kibinafsi ya ujumbe.

"Alifanikiwa kunidanganya bila ugumu wowote," anasema. "Haikuchukuwa muda nilijikuta nikilazimishwa kufanya mambo ambayo mtoto hapaswi kufanya."

Mara tu alipomlazimisha Alice kumtumia picha, Fordyce alimshawishi kwamba alikuwa akishiri katika utengenezaji na ushirikishaji wa nyenzo za unyanyasaji wa watoto kingono.Kwa kuogopa kukamatwa, alificha kila kitu kutoka kwa familia yake na marafiki.

"Nilitumia sehemu kubwa ya utoto wangu kwa nia yake kila siku nikiwa nikiwa karibu na mtu ambaye alikuwa na nia mbaya zaidi kwa watoto."

Hii iliendelea kwa miaka mitatu, hadi mwishowe Fordyce alipopoteza hamu na mawasiliano kati yao kutoweka.

Alice alipanga kufa na siri hiyo lakini polisi wa Canada waliona mtu akishiriki nyenzo za unyanyasaji wa watoto kingono mtandaoni.

Pam Klassen, mtaalam wa uchunguzi wa idara ya polisi huko Brandon -magharibi mwa Winnipeg - alifuatilia anwani ya IP hadi nyumbani kwa familia ya Ryan Fordyce, na kupata hati ya upekuzi.

Fordyce hakuwepo nyumbani alipomtembelea tarehe 12 Januari 2018, lakini alifaulu kuingia kwenye kompyuta yake na kupata na mkusanyo wa kutisha wa picha na video za unyanyasaji wa kijinsia, zilizotumwa na watoto chini ya maagizo yake. Fordyce alipofika nyumbani kwa chakula cha mchana alimkamata.

"Alishangaa," asema, "na mke wake alifikiri lazima kulikuwa na kosa."

Polisi walipata sehemu sehemu saba maalum kwenye kompyuta, kila moja ikiwa na jina tofauti la msichana. Moja ilikuwa na picha na video 220 za Alice, mwenye umri wa kati ya miaka 11 na 14, ambazo baadhi yake alilazimika kupiga punyeto.

Pam Klassen alimfuatilia Alice kutokana na sare yake ya shule, ambayo ilionekana katika baadhi ya nyenzo, na ndipo Fordyce alihukumiwa mnamo Desemba 2021 kifungo cha miaka minane jela.

Fordyce, baba wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 30 hivi, pia alikuwa amemtumia Omegle kuwachumbia wahasiriwa wake wengine wawili.

Leif K Brooks aliunda Omegle alipokuwa na umri wa miaka 18 na alikuwa kwenye orodha ya Forbes Under 30 mnamo 2018.

Chanzo cha picha, TWITTER

Maelezo ya picha, Leif K Brooks aliunda Omegle alipokuwa na umri wa miaka 18 na alijumuishwa kwenye orodha ya Forbes Under 30 mnamo 2018.

A.M vs Omegle

Baada ya Fordyce kuchukuliwa hatua ya kisheria, Alice alielekeza juhudi zake kwa mtandao wa Omegle katika kesi inayofuatiliwa kwa karibu kote ulimwenguni.

Hii inaweza kuwa mara ya kwanza dhidi ya jukwaa la teknolojia kushtakiwa kwa kuendekeza unyanyasaji dhidi ya watoto.

Timu ya wanasheria inahoji kuwa Omegle aliweza kuwa "eneo la mawindo kwa wanyanasaji watoto" kwa sababu ya ukosefu wa mfumo wa kuthibitisha umri wa watumiaji wake.

Wanatumai hatua hii inaweza kumpatia Alice fidia ya mamilioni ya dola, na kulazimisha mabadiliko kwenye muundo wa Omegle.

Mabadiliko yoyote yatayotokana na visa kama hivyo, nchini Marekani au kwingineko, yatawanufaisha watumiaji wa mitandao kote duniani.

Omegle pia anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria nchini Uingereza iwapo Mswada wa Usalama Mtandaoni uliocheleweshwa kwa muda mrefu hatimaye utapitishwa.

Mswada huo unapendekeza kampuni zitozwe faini kubwa iwapo zitashindwa kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji mtandaoni.

Wanasheria wa Omegle wametoa hoja mahakamani kwamba mtandao huo haufai kulaumiwa kwa kile kilichomkumba Alice na kukanusha kuwa ni chanzo cha wanyanyasaji watoto.

Hata hivyo lakini mtandao wa Omegle umehusishwa na zaidi ya visa 50 vya unyasasaji dhidi ya watoto katika miaka miwili iliyopita iliyopita.

Visa zaidi ya 20 viliripotiwa nchini Marekani, na vingine kadhaa nchini Uingereza, Australia, Uhispania, Colombia na Cyprus.

Mwasisi wa mtandao huo, Leif Brooks, hakutaka kuangazia kisa cha Alice kupitia barua pepe kwa hivyo BBC ilikutana naye nyumbani kwake Orlando, Florida, kwa matumaini ya kuzungumza naye lakini juhudi hizo hazikufua dafu baada ya Bw Brooks kukataa kuongea kwa mara nyingine tena.

Brooks amefanyia mtandao huo marekebisho madogo wiki chache baada ya kuarifiwa kuhusu hatua za kisheria za Alice, sanduku lilionekana kwenye Omegle amabap watumiaji wanapaswa kuweka kubainisha wana zaidi ya miaka 18, kabla ya kujinga.

Lakini wanasheria ya Alice wanasema hii "haitoshi".

Alice mwenyewe anasema angependa kuona Omegle ikifungwa.