Kwanini watoto wako wapo hatarini katika mtandao?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo Julai 2020, polisi wa jimbo la Assam walipata malalamiko kuhusu ukurasa wa Facebook ambao walikuwa wanautilia shaka.
Taarifa hizo zilitolewa na shirika lisilokuwa la kiserikali.
Ukurasa wa Twitter wa taasisi hiyo ilitoa angalizo kuhusu kurasa ya Facebook ambayo ilikuwa na video na picha za watoto , na inawezekana kurasa hiyo inahamasisha unyanyasaji wa kingono kwa watoto.
Kuhusiana na hili, mwanaume mmoja mwenye miaka 28 anayeishi kijiji kilicho umbali wa kilomita 100 kutoka Guwahati alikamatwa mwezi Septemba na kuachiwa huru kwa dhamana.
Mtu huyu anashutumiwa kuanzisha kurasa hiyo ya Facebook.
Polisi wanadai kuwa video za unyanyasaji wa kingono kwa watoto zilikuwepo pia kwenye simu ya mtuhumiwa huyo.
Ingawa mtuhumiwa anakanusha madai hayo dhidi yake.
Kuchapisha , kusambaza na kumiliki picha za ngono za watoto ni kinyume na sheria nchini India.
Mwanaume huyo ambaye alikuwa amezungukwa na familia yake ameiambia BBC akiwa nyumbani kuwa: "Sijawahi kupakua video za unyanyasaji wa watoto kingono, sijawahi kuzisambaza au kuwa nazo."
Polisi wanadai pia kuwa mtu huyo alikuwa anajaribu kupata pesa kupitia kurasa huo wa Facebook na kusambaza picha hizo kwa kutumia programu ya SISAM.
Kwa mujibu wa polisi , kulikuwa na uhusiano wa programu ya Telegram na kurasa ya Facebook kama ukiibonyeza, utapata chaneli ya Telegram.
Inadaiwa kuwa kulikuwa na video za ngono za watoto kupitia programu ya SISAM na video za programu nyingine.

Kwa mujibu wa polisi , kulikuwa na mpango wa kujipata fedha katika chaneli ya telegram , lakini kwa mujibu wa polisi,ni kuwa mtu huyo alikuwa tayari yupo kizuizini kabla ya njama hiyo ya fedha kufanyika, lakini haijawekwa wazi ni namna gani mtu huyo alipata hizo fedha.
Geetanjali Dole, ambaye anafanya uchunguzi kesi hii anasema alivyoangalia video hizo, hakuweza kulala kabisa usiku; " Sikuweza kulala kwa siku kadhaa kutokana na kile nilichokiona."
Kurusa hiyo ya Facebook sasa imefungwa na kesi hiyo ipo mahakamani.
Kwa mujibu wa ripoti , mwaka mmoja kabla ya mlipuko wa corona, 2018, watoto 109 walikuwa wanafanyiwa unyanyasaji wa kingono kila siku.
Kwa mujibu wa wanaharakati na maofisa wa polisi, wanasema wakati wa mlipuko wa Corona nchini India, kumekuwa na ongezeko kubwa wa video za aina hiyo mtandaoni au kusambaa kwa video hizo.
Kwa mujibu wa Manoj Abraham,mkuu wa kituo cha polisi cha jimbo la Kerala ambayo inafanya kazi kubwa ya kupambana na uhalifu wa mtandaoni , takwimu zinaonesha kuna ongezeko la asilimia 200 mpaka 300 katika kipindi hiki cha mlipuko.

Imetubidi tuhamie Kerala kwasababu kwa mujibu wa wataalamu, Kerala inaongoza kwa kuwa na polisi wenye utaalamu wa masuala ya uhalifu wa mitandao katika upande wa matumizi ya teknolojia na kugundua uhalifu.
Manoj Abraham anahofia kuongezeka kusambaa kwa video hizo.
Video za unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto, zilipigwa picha katika eneo la Kerala au eneo lingine la India.
Wasiwasi wangu ni kuwa video nyingi zinarekodiwa ndani.
Manoj Abraham anasema, "Unaweza kuona katika video ni ndani ya nyumba na hakuna ambapo unaweza kuona nje.
Hivyo ni hatari sana kwani inawezekana mtu huyo anarikodi akiwa anaishi na watoto hao ndani ya nyumba hiyo.
Miguel das Quiha, ambaye ni mwanaharakati wa haki za watoto anasema, "Polisi wanashughulikia zaidi kuhakikisha sheria ya kukaa ndani inafuatwa ili watu wasipate maambukizi ya corona."

Chanzo cha picha, Getty Images
Hali ilivyo duniani
Mnamo Aprili 2020, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wametoa angalizo kuwa marufuku ya watu kutotoka kumeongeza matumizi ya mtandao na kunaweza kuongeza waangaliaji wa vido za ngono kuongezeka kwa udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia na watoto.
Uzalishaji wa video hizo za unyanyasaji wa kingono kuongezeka na hata mbinu za kusambaza na kutengeneza kukua.
Mwaka 2020, Kituo cha kutoa taarifa kuhusu uhalifu wa mtandaoni kilichopo Marekani kilitoa ripoti kuhusu picha na video za watoto ambao walipotea na kufanyiwa unyanyasaji wa kingono kwa mwaka 2017 na maudhui ya video hizo yalifanana na yanayosambazwa mtandaoni India.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna ongezeko la asilimia 28 ukilinganisha na mwaka 2019.
India inaongoza katika unyanyasaji huo. Sababu kuu si ngumu kuzibaini.
Ni kwa kuwa wakati wa marufuku ya kutoka nje kwa muda mrefu, video za watoto mtandaoni ziliongezeka.
Kwa mujibu wa wanaharakati wa mtandaoni.
Hali ni mbaya kiasi gani?
Mapema mwezi Agosti, kijana kiume mwenye umri wa miaka 16-alikuja kuripoti kwa mwanaharakati Siddharth Pillai huko Mumbai.
Kupitia mawasiliano ya meseji za simu ya mkononi, aligundua mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka 10 alikuwa katika mitandao ya kijamii.
Utafiti uliwasiliana na mfuko wa kulinda watoto nchini India mwaka 2019 Desemba mpaka Juni 2020 na kubaini:
Nchini India , asilimia 90 ya watumiaji wa programu ya maudhui ya ngono ya sesam ni wanaume na asilimia moja ni wanawake na wengine hawafahamiki.
Wengi walikuwa wanavutiwa na video za ngono za vijana wadogo na ngono shuleni.
Na wengi wao walikuwa wanatumia VPN ili wasijulikane wanapatikana wapi ili wasigundulike na serikali kwa ajili ya usalama.
Kuwafuatilia wasambazaji wa video za programu ya sesam
Kwa mujibu wa wataalamu, video nyingi za unyanyasaji wa kingono kwa watoto inayosambazwa katika mitandao ya kijamii , huwa wanatumia VPNs,kusambaza kwa watumiaji.
Maofisa wanasema maudhui ya Sesam yanatumwa mtandaoni kisiri, katika biashara nyingi zilizo kinyume na sheria zinafanyika.
Katika mitandao ya siri, ndio kona ambayo maelfu ya majukwaa ya mitandao au tovuti yana masoko yasiyo rasmi na haramu.
Aidha mtaalamu wa mtandao Manoj Abraham anasisita kuwa ni muhimu kwa wazazi kuwa makini na watoto wao kujua wanafanya nini mtandaoni, na watoto wanapaswa kufundishwa kile kilicho salama katika intaneti.Na vilevile wazazi kuwa makini na watu ambao wako karibu na watoto wao.














