Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uhalifu dhidi ya Mungu unaotumiwa na Iran kuwanyonga wandamanaji ni wa aina gani?
Ni kosa ambalo mahakama nchini Iran hulielezea kama uhalifu mbaya sana, kwani , adhabu yake kulingana na muktadha wa sheria ya Kiislamu, ni hukumu ya kifo: uhalifu wa ‘’chuki dhidi ya Mungu’’ au "moharebeh".
Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran imewahukumu mamia ya watu kwa kosa hili.
Wiki hii, iliwanyonga waandamanaji wawili kuhusiana na maandamano ambayo yamekuwa yakifanyika kote nchini humo tangu mwezi septemba kufuatia kifo cha kijana wa kike ambaye alikamatwa na polisi wa maadili kwa kuvaa hijabu, au kilemba cha Kiislamu kwa namna isivyofaa.
Mohsen Shekari na Majidreza Rahnavard, wote wakiwa na umri wa miaka 23, walinyongwa katika kipindi cha saa chache baada ya kupatikana na hatia ya moharebeh na mahakama ya nchi hiyo.
Shekari alipatikana na hatia ya kumshambulia mwanajeshi wa Basij Resistance Force kwa upanga mjini Tehran, huku Rahnavard akihukumiwa kwa madai ya kuwauwa wanajeshi wawili wa kikundi hicho.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yalipinga hukumu hiyo huku yakesema kuwa waandamanaji walihukumiwa kifo katika mahakama zisizo halali na mchakato wa kisheria unaofaa haukufuatwa yakionya kuhusu "hatari kubwa ya kunyongwa kwa waandamanaji wengi " .
Walisema kuwa watu binafsi walioshutumiwa kwa uhalifu wa moharebeh hawana haki ya kupata mawakili huru na nyingi kati ya kesi hizi ziliendeshwa kwa misingi ya ushahidi wa kulazimishwa.
La akushangaza zaidi, kulingana na mtizamo wa sheria ya kitamaduni, kosa linaweza kutafsiriwa kwa namna mbali mbali. "mashitaka yanategemea Imani ya jaji kwamba vita vimeanzishwa dhidi ya Mungu," anaelezea Amir Azimi, mhariri mkuu wa Idhaa ya Persia ya BBC
Maadui wa Mungu"
Baada ya Mapinduzi ya Iran ya mwaka 1979, sheria ya Iran ilianza kubadilika kutoka sheria isiyofuata dini yoyote na kuwa sharia (Sheria ya Kiislamu), anasema Amir Azimi.
"Kuundwa kwa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran kulianza na matumizi ya sheria hiyo kote nchini, kwani ni sheria ya maadili kwa Waislamu ," anasema Amir Azimi.
Kulingana kipengele cha 279 cha sheria ya Kiislamu, moharebeh inaweza kumaanisha kuchora silaha kwa nia ya kushambulia maisha, mali au heshima ya watu au kuwatisha, ili kusababisha ukosefu wa usalama katika mazingira.
Hiyo ni moja ya misingi ya shutuma, zilizoelezewa na mhariri mkuu wa Idhaa ya Persia ya BBC . "iwapo mtu atachukua silaha( Inamaanisha kuwa anaweza kufyatua risasi) na kuzitumia 'kumtisha mtu, wanachukuliwa kuwa wametekeleza moharebeh .
Kwahivyo , hapa inategemea na jinsi itakavyotafsiriwa, na kwasababu vizuizi vya barabarani kila mara huwekwa wakati maandamano yanapofanyika, hata kama ni maandamano ya amani, sawa na yale yanayoendelea sasa.
Hatua ya kibinafsi
Sehemu muhimu ya tafsiri ya uhalifu pia inategemea juu ya iwapo shambulio ni la mtu binafsi au la.
Kwa mfano, iwapo mtu fulani atamuua mtu mwingine sio lazima apatikane na hatia ya moharebeh . "Muuaji, iwapo atalipia uhalifu wake au familia ya mhanga itaamua kumsamehe, hawezi kuepuka kuhukumiwa kunyongwa," anasema Azimi.
Lakini katika maandamano, waandamanaji hawaelekezi hasira yao kwa yeyote, kwahiyo kitendo chao hakimlengi mtu binafsi. Kwa kisa hiki, wanakabiliwa na shitaka la moharebeh.
Hilo linairuhusu sheria kutumiwa zaidi na zaidi kisiasa. Ni sawa na "kutisha".
Wanaharakati wengi wa kisiasa wamekamatwa, kufungwa na kuhukumiwa kwa kufanya maandamano.
Silaha ya kisiasa
Kutokana na hali halisi ya kisiasa, utawala huitumia sheria hii dhidi ya upinzani a watu binafsi na makundi yanayoukosoa utawala, ambao marengo yao ya kisiasa inaweza kuonekana kwa muktadha mwingine kama halali. Lakini nchini Iran watu hawa huwekwa katika hali ambayo inakuwa vigumu kwa wao kujitetea.
"Hilo limetokea kabla dhidi ya Wakurdi na jamii za walio wachache," anasema Amir Azimi.
Shirika la haki za binadamu la Iran lenye makao yake nchini Norway lilipinga hukumu ya kunyongwa dhidi ya wafungwa wanasiasa wa Kikurdi Loghman Moradi na Zanyar Moradi mwezi wa septemba 2018, likidai kuwa walilazimishwa kukiri makis ana hawakuwa na uwakilishi unaofaa wa kisheria katika kesi dhidi yao.
Huu ni baadhi ya ukosoaji mkubwa dhidi ya utekelezwaji wa hukumu hiyo katika uhalifu huu, kwani washitakiwa hawawezi kupata mawakili binafsi wa kuwawakilishamahakama huwapatia wakili ambaye hurudia uamuzi wa jaji.
Kama mshitakiwa anaweza kumkodi wakili wake , hapewi ruhusa ya kuwasiliana naye na hakuna njia ya kutoa ushahidi mwingine. Huwezi pia kukata rufaa kwa hukumu iliyotolewa.
Viongozi wa Iran wameyaita maandamano ya "ghasia" zilizochochewa na maadui wa kigeni.
"Kwa mtazamo wa serikali, ni kwamba watu hawa wamedanganywa na maadui wa kigeni kufanya fujo," Azimi anasema, " kwahiyo iwapo utasema kuwa ulidanganywa haukuwa unaelewa kinachoendelea, unaweza kusamehewa ."
Katika miongo minne iliyopita Iran imewauwa maelfu ya watu wa kuwanyonga. Baada ya uchina , Iran ni nchi ya pili kwa kuwauwa watu wengi zaidi duniani kila mwaka.