Je, mtoto anaweza kujifunza nidhamu akiwa tumboni?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Kwa mujibu wa shirika la habari la PTI, Madhuri Marathe, katibu wa shirika hilo la kitaifa alisema, "Kampeni inayoitwa Garbh Sanskar imeanzishwa kwa wajawazito ili mtoto afundishwe maadili akiwa tumboni."

Kulingana naye, warsha iliandaliwa katika Chuo Kikuu cha Jawahar Lal katika mji mkuu wa Delhi, ambapo madaktari 80 wa magonjwa ya wanawake kutoka majimbo 12 pia walishiriki.

Madhuri Marathe alisema, "Programu hii itaendeshwa hadi mama mjamzito na mtoto watakapofikisha umri wa miaka miwili.

Mtoto anayekua tumboni anaweza kujifunza hadi maneno 500.

Lakini je, mtoto anayekua tumboni anaweza kuelewa kweli maneno au lugha yoyote?

Ulimwengu wa sayansi umegawanyika katika suala hili.

Mwanaharakati wa kike wa Mumbai na daktari wa magonjwa ya wanawake Dk. Suchitra Delvi anasema kwamba mtoto ambaye hajazaliwa anaweza kusikia sauti lakini hawezi kuelewa lugha yoyote.

Anasema, “Kadiri mwili wa mtoto unavyokua tumboni, masikio yake pia hukua.

Katika hali hiyo, mawimbi ya sauti pia humfikia.

Lakini mtoto haelewi maana ya sauti hizo. Katika hali kama hiyo, hata ikiwa mama anasoma chochote, mtoto ataelewaje?

Maoni tofauti

.

Chanzo cha picha, UMESH NEGI

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Anaamini kwamba hii ni dhana tu na haina msingi wa kisayansi.

Dk. Suchitra Delvi anasema kuwa badala ya kufikiria mambo kama hayo, tunapaswa kuwafikiria watoto waliokuja katika dunia lakini wananyimwa vitu vya msingi kama chakula, elimu. Lazima kuwe na majadiliano ya kuwapa watoto uraia mwema na utamaduni mzuri.

Kwa upande mwingine, mtaalamu wa mambo ya viungo Dr. SN Basu anasema kuwa utafiti unaonyesha kwamba kiumbe aliye tumboni anaweza kuota na na pia kuhisi.

Akirejea makala ya Fetal Psychology iliyochapishwa kwenye tovuti ya Marekani ‘Psychology Today’, anasema, "Imeandikwa wazi kwamba kwamba hadi ujauzito ufike wiki ya tisa, anaweza kusikia makelele au sauti ya juu, na katika wiki ya 13, anaweza kusikia vizuri. Wakati huo huo, yeye pia kutofautisha kati ya sauti ya mama na mtu asiyejulikana.

Anasema, "Imesemekana pia katika utafiti huu kwamba ikiwa kijusi kinachokua ndani ya tumbo la uzazi kinasimuliwa hadithi mara kwa mara, basi pia huguswa nayo."

Ameongeza zaidi, "Pia imeandikwa katika utafiti huu kwamba pamoja na uwezo wa kuhisi, kuona na kusikia kwa kiumbe aliyetumboni, uwezo wa kujifunza na kukumbuka pia hukua."

Kama vile kijusi hushtushwa kwanza na kelele lakini kisha huacha kuitikia kwa wakati.

Anasema, “Mtoto anakua tumboni. Wakati huu mama akifanya mambo mazuri, basi huathiri mtoto pia.

Homoni na athari kwa mtoto

.

Chanzo cha picha, SCIENCE PHOTO LIBRARY - SCIEPRO

Daktari Suchitra Delvi anasema, "Kama mwanamke mjamzito ana matatizo na homoni zinazozalishwa katika mwili wakati huu huathiri mimba pia".

Dr. Suchitra Delvi anaeleza, "Athari ya homoni inayotokea wakati huo humfikia mtoto kupitia mama. Ina maana ya homoni za mfadhaiko na furaha pia huathiri mtoto akiwa tumboni na hili lina msingi wa kisayansi.

Mukta Dabholkar, mwanaharakati, anakubaliana na suala la mama kuhakikisha anakula chakula chenye virutubishi, kuwa na mawazo mazuri na kuweka akili katika hali ya utulivu kwa mwanamke mjamzito.

Anasema, "Wakati mtoto anakua tumboni hawezi kuelewa lugha, jinsi gani atajua kwamba mama anasoma kitabu takatifu".

Kulingana naye, "Ni muhimu kwa mama kuwa na furaha na inastahili kuwa jukumu la familia kuhakikisha anakuwa na furaha yake ".

Kueneza itikadi

Utafiti umeanzishwa katika Chuo Kikuu cha Banaras Hindu huko Uttar Pradesh ambapo unathibitishwa ni nini athari za kelele na muziki kwa mtoto akiwa tumboni.

Daktari Sunita Suman, Idara ya Obstetrics na Colnecology, Kitivo cha Ayurveda, BHU, anasema, "Utafiti huu unaoitwa ‘Garbh Sanskar therapy’ ndio kwanza umeanza. Itachukua muda kupata habari zaidi. Lengo la hii pia ni kwamba kama mama anapitia mfadhaiko, utafiti unaendelea kufuatilia kuhusu athari za aina hii ya matibabu kwake.

Baadhi ya wachambuzi wa siasa wanaamini kwamba hili ni jaribio la kueneza na itikadi.

Mchambuzi Rajesh Sinha anasema kuwa vitu kama hivyo vimewekwa ili kuibua dhana za Wahindu, ambazo hazina msingi wa kimantiki.

Watu nchini India wamejaa ushirikina kweli ambapo wana imani maalum.

Mambo kama haya yanaongeza msingi wa kisiasa na kitamaduni.