Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Seneti ya Marekani yapitisha muswanda wa sheria ya ndoa ya jinsia moja
Bunge la Seneti la Marekani limepitisha muswada wa sheria wa kihistoria ulioungwa mkono na pande mbili za kisiasa ili kulinda ndoa ya watu wa jinsia moja na ndoa ya watu kutoka asili tofauti.
Sheria hiyo sasa itakwenda tena katika Bunge la wawakilishi, ambalo linatarajiwa kuiidhinisha na kuipeleka kwa Rais Biden aitie saini.
Wanaounga mkono muswada huo wanatumai utapitishwa kabla ya Warepublican kuchukua udhibiti wa Bunge la wawakilishi mwezi Januari.
Muswada huo, hatahivyo, haujatimiza vigezo vya kitaifa kwamba majimbo yote lazima yahalalishe kisheria ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Muswada ulipata mvuto zaidi wakati wa uamuzi wa wa Mahakama ya juu zaidi mwaka huu uliotupilia mbali haki ya shirikisho ya utoaji mimba. Watetezi wa wapenzi wa jinsia moja -LGBT walihofia kuwa ndoa ya watu wa jinsia moja inaweza kukabiliwa na tisho katika miezi ijayo.
Hesabu ya kura ya wabunge kuhusu muswada huo iliyopigwa Jumanne ilikuwa ni wabunge 61 kwa wabunge 36, huku Warepublican 12 wakipiga kura kuungano mkono muswada huo.
Sheria hiyo ilipata uungaji mkono zaidi kutoka kwa idadi ya maseneta kadhaa wa Warepublicans baada ya kurekebishwa na kujumuishwa kwa vipengele vya kulinda uhuru wa kidini.
Lengo la muswada huo ni kuingiza haki za ndoa za watu wa jinsia moja chini ya sheria ya shirikisho, ingawa ushirika huo bado unalindwa kitaifa chini ya uamuzi wa mwanzo wa Mahakama ya juu zaidi ya Marekani. Katika taarifa, kiongozi wa walio wengi katika bunge la seneti Chuck Schumer alisifu uamuzi kama hatua ya kusonga mbele katika " mwendo mrefu lakini usiobadilika wa bila kukata tamaa ".
"Kwa kupitisha muswada huu, seneti inatuma ujumbe kwamba kila Mmarekani anahitaji kusikia: bila kujali wewe ni nani au unampenda nani, unahitaji heshima na usawa chini ya sheria."
Senata Tammy Baldwin, Mdemocrat ambaye ni seneta aliyejitangaza wazi kama mtu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja na mdhamini kiongozi wa muswada huo, alisema sheria ita "linda mafanikio yaliyopiganiwa kwa nguvu"
Je sheria ya kulinda Heshima ya Ndoa inasemaje?
Sheria mpya ilibadilisha rasmi kinga ya sheria ya ndoa, ya mwaka 1996 ambayo inaelezea ndoa baina ya mume na mke pekee. Mahakamu ya juu zaidi iliamuru kuwa sheria hiyo ni kinyume cha katiba mwaka 2013.
Muswada wa Seneti pia unayataka majimbo kutambua ndoa za jinsia moja ambazo zimefanyika katika majimbo mengine, na kuhakikisha maslahi ya shirikisho yanawafikia wenzi waliooana kama wapenzi wa jinsia moja.
Kura hiyo imepigwa baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo ua pande mbili za kisiasa, na kura hii ya Seneti ilifanyika baada ya uchaguzi wa nusu muhula.
Toleo la wali la muswada huo liliidhinishwa na Bunge la Wawakilishi mapema mwaka hu una baadhi ya Warepublicans mwaka huu. Huku baadhi ya Warepublicans wakielekea kufanikiwa kupitisha miswada katika Bunge la seneti na Bunge la wawakilishi, wengi katika chama hicho bado hawaiungi mkono sheria hiyo. .
Mwezi Julai 2022 kura ya maoni ya Gallup ilibaini kuwa 71% ya Wamarekani waliunga mkono ndoa ya jinsia moja.
Kesi ya Obergefell v Hodges na Mahakama ya juu zaidi
Mahakama ya juu ya marekani ilianzisha sheria inayolinda ndoa ya watu wa jinsia moja katika uamoji wake wa kihistoria wa mwaka 2015 katika uamuazi wa kesi ya Obergefell v Hodges.
Uamuzi huo uliondoa marufuku zilizopo za jimbo dhidi ya ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, na kuwapa wenzi wa jinsia moja haki ya kuoana kote nchini Marekani na kuwapatia haki za kisheria na maslahi ya kimataifa ambayo watu walioona kama mume na mke wanayapata nchini Marekani.
Mahakama ya juu zaidi ya sasa ina msimamo mkali zaidi, na haki kuhusu ndoa zimekuwa hofu yake ya kwanza tangu ilipoondoa haki ya kikatiba ya utoaji mimba katika kesi ya Dobbs v Jackson , kesi iliyohusisha Shirika la wanawake la afya mepema mwaka huu.
Katika uamuzi wake, Jaji, Clarence Thomas, pia alisema kuwa maswala hayo yalichangia msingi wa maamuzi muhimu – ikiwa ni pamoja na haki za za ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, na dawa za kuzuia mimba – yanaweza kupingwa.
Jim Obergefell, ambaye alikuwa mlalamikaji mkuu katika kesi hiyo ya Mahakam ya juu mwaka 2015 aliiambia BBC kwamba "hajaridhishwa kabisa" na Sheria ya Heshima ya Ndoa.
Alisema kwamba, huku ikiyataka majimbo yote kutambua usawa wa ndoa, baadhi ya majimbo bado yanaweza kukataa kutoa vibali vya ndoa kwa wanandoa wa jinsia iwapo uamuzi wa mwaka 2015 utaondolewa.
Anasema anasikitishwa na marekebisho yaliyopelekea kuwepo kwa uhuru wa dini ambayo yataruhusu mashirika ya kidini kuzuia kutoa huduma au mahala pa kufanyia sherehe za harusi za watu wa jinsia moja.
Makundi kadhaa ya kidini yameunga mkono muswada, likiwemo kanisa la Jesus Christ of Latter-day Saints, ambalo lilisema katika taarifa mwezi huu kwamba muswada huo na ulinzi wake wa uhuru wa kidini "ni njia inayofaa".
Lakini Bw Obergefell alisema kuwa ni bora awe na sheria hiyo kuliko kutokuwa na nayo kabisa.
"Siipendi, lakini nitaichukua," Alisema Bw Obergefell.