Jinsi wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa wanavyosaidiwa kuishi kimapenzi

w

Chanzo cha picha, ReSex

Maelezo ya picha, Hlib Stryzhko (kushoto) anaigiza katika tangazo la ReSex, shirika la hisani linalowasaidia maveterani wa Kiukreni maisha yao ya ngono.
Iliyochapishwa

Katika ofisi ya kisasa katikati mwa Kyiv, mwanajeshi mkongwe wa Ukraine mwenye umri wa miaka 26 anajivunia kucheza video kwenye simu yake inayomwonyesha akimbusu kwa upendo kijana mdogo wa kike jikoni.

Ni tangazo la ReSex : shirika la hisani ambalo hujaribu kuwasaidia wanajeshi wa zamani na maisha yao ya ngono, baada ya kupata kiwewe cha kimwili na kiakili.

Mnamo Machi mwaka jana, vikosi vya uvamizi vya Urusi vilizingira kikatili mji wa bandari wa Mariupol wa Ukraine, na kuharibu sehemu kubwa yake.

Hlib Stryzhko - wakati huo baharini - alikuwa mmoja wanajeshi waliokuwa wakipambana kulilinda jiji hilo.

Mlipuko wa mashambulio ya Urusi ulimwangusha kutoka ghorofa ya tatu ya jengo hadi chini. Kisha aliangushwa chini ya kifusi.

Kiuno cha Hlib, taya na pua vilivunjika, na vilevile akawa amechanganyikiwa vibaya, anasema joto la mlipuko huo liliyeyusha miwani yake ya kiufundi usoni mwake. Kisha alitekwa na vikosi vya Urusi na kuchukuliwa kama mfungwa wa vita.

Mwezi uliofuata, Hlib aliachiliwa na kurudishwa katika eneo la Ukraine kama sehemu ya kubadilishana wafungwa. Lakini anasema alipata huduma ndogo ya matibabu wakati alipokuwa kifungoni.

BBC ilizungumza kwa mara ya kwanza na Hlib wiki chache tu baada ya kuachiliwa, na baadaye ikimpata katika hospitali moja iliyopo katika mji wa magharibi wa Lviv.

f
Maelezo ya picha, Hlib Stryzhko alivunjika mfupa wa nyinga na taya mnamo Machi 2022 alipokuwa askar iwa kikosi cha majini Mariupol.

Ilikuwa wakati Hlib akifanya kazi ya kupona ambapo ReSex ilimkaribia.

"Baada ya kuumia mfupa wa nyonga nilikuwa na matatizo ambayo yalichukua muda kupona. Na [suala la ngono] halikuzungumzwa sana, kwa hivyo nisingependa hilo litokee kwa watu wengine kama mimi," anasema.

"Hiyo ilikuwa motisha ya kushiriki katika mradi huo."

Ivona Kostyna ni mmoja wa waanzilishi wa Veteran Hub, kikundi kinachoendesha mradi wa ReSex.

Anasema walikuwa na wazo la kwanza la mradi huo mnamo 2018, baada ya kusoma taarifa kuhusu suala hilo kwa wanajeshi wa Marekani.

f
Maelezo ya picha, Ivona Kostyna muasisi mwenza wa Veteran Hub

Baada ya kupata ufadhili na kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi, walizungumza na wanajeshi na wataalamu wa Ukraine, ili kuhakikisha wanafikisha msaada wao haswa kwa wanaume na wanawake wanaohitaji.

Walikabiliwa na mkanganyiko kutoka kwa umma - na wanajeshi wa zamani- walipouliza kwa mara ya kwanza majibu ya maswali mtandaoni. "Watu wanakufa, unafikiria ngono!" Ivona anasema.

Pia ilibidi wakabiliane na baadhi ya dhana zao - kama vile dhana potofu kwamba wanajeshi waliojeruhiwa wote wangekuwa wanahangaika na maisha yao ya ngono.

"Kuna ngono hospitalini, ngono nyumbani, ngono kabla ya taratibu, Kuna ngono nyingi nzuri zinazoendelea," Ivona anasema. "Tulifikiria na kujiuliza, Eeh!, sawa, tunawezaje kusaidia hapa?".

Lakini kwa ujumla, anasema, mwitikio umekuwa mzuri sana.

f
Maelezo ya picha, ReSex wamechapisha vijitabu - vinavyoitwa "Do Love" - kwa wanawake na wanaume
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Shirika la misaada limechapisha vijitabu 6,000 na kuvituma kwenye vituo vya matibabu, wapiganaji wa zamani na familia zao kote Ukraine, na kuvifanya vipatikane mtandaoni.

ReSex pia imezindua kampeni ya mitandao ya kijamii yenye video, michoro na nambari ya usaidizi. Shirika la hisani linashughulikia kila kitu kutoka kuanzia kujichua hadi vinyago vya ngono na hata biolojia ya kimsingi.

"Tunajaribu kuandika yote," Ivona anasema, akiongeza kuwa pia kuna sehemu ya kijitabu mahsusi kwa ajili ya wapiganaji vijana waliojeruhiwa ambao wanaweza kuwa mabikra.

"Kwa hivyo ngono baada ya jeraha itakuwa ngono yao ya kwanza, ambayo ni tofauti kabisa na vile wangeweza kuifikiria."

Kateryna Skorokhod, meneja wa mradi wa ReSex, anasema walichapisha miongozo tofauti kwa wanawake na wanaume ili kuhakikisha wenzi husika wana ushauri maalum unaolenga uzoefu wao na miili yao.

Anasisitiza hata hivyo kwamba lengo la mradi ni zaidi upande wa kihisia kuliko wa kimwili.

"Ni kuhusu jinsi unavyoweza kujikubali, jinsi unavyoweza kujipenda, na jinsi unavyoweza kujenga uhusiano na wewe mwenyewe na mpenzi wako baada ya majeraha haya - kwa ngono na kwa urafiki katika mahusiano."

h
Maelezo ya picha, Meneja wa mradi wa ReSex Kateryna Skorokhod anasema wanataka wanajeshi hao wa zamani waliojeruhiwa kujifunza kujipenda.

Lakini pia wamejifunza mengi kuhusu wapiganaji wa zamani wenye majeraha wa Ukraine. Hasa, waligundua kuwa majeraha ya kiwewe ya ubongo mara nyingi hayatambuliwi na hayatibiwi nchini - jambo ambalo anasema linaathiri "hamu ya kufanya ngono na utendaji wote wa ngono sana".

Lugha inayotumika kujadili ngono ni muhimu pia, Ivona anasema.

"Kwa hakika si lugha ya kushangaza. Kwa hakika si kuhusu 'kushinda vikwazo' - hiyo pengine ni nzuri kwa michezo, lakini inatokea kwamba ngono haiko katika kiwango sawa.

Anasema ni muhimu kuhakikisha kwamba wakongwe wanajua kuwa si lazima wafanye ngono isipokuwa wanataka, na kwamba ngono inaweza kuwa ngumu au chungu mwanzoni.

g
Maelezo ya picha, Hlib hakika anazungumza vyema kuhusu mradi ambao amejiunga.

Hlib hakika anazungumza vyema kuhusu mradi ambao

amejiunga.

Alipoulizwa kama ana mpenzi tangu majeraha yake, anacheka.

"Baada ya kurudi kutoka kwenye utumwa wa hospitali, nilikuwa na rafiki wa kike, halafu mwingine nilipokuwa nafanya mazoezi ya mradi na sasa nina mpenzi," anasema.

Lakini alisema anashukuru kwa kila mtu ambaye alikuwa amechumbiana naye mwaka uliopita. "Kila mpenzi niliyekuwa naye alikuwa muhimu kwangu, katika kupata ujasiri wangu tena. Ninashukuru sana kwa hilo."