Tetesi za soka Ulaya Jumapili 31.03.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti anasema hana wasiwasi kuhusu winga wa Brazil Vinicius Jr kuondoka katika klabu hiyo, baada ya uvumi kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anaweza kuhama kwa sababu ya unyanyasaji wa kibaguzi aliofanyiwa. (Diario Sport – In Spanish)
Chelsea inapanga kuwauza wachezaji wake wawili wa kimataifa wa Uingereza - beki wa kulia Reece James, 24, na kiungo wa kati Conor Gallagher, 24 - msimu huu ili kuepuka kukiuka kanuni za faida na uendelevu za Ligi ya Premia. (Times – Subscription Required)
West Ham wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 28, katika mpango wa "taarifa" kwa klabu hiyo. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Paris St-Germain Luis Enrique bado anatumai kuwa anaweza kumshawishi fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25, kusalia katika klabu hiyo badala ya kujiunga na Real Madrid mkataba wa mshambuliaji huyo utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. (Goal)
Ruben Amorim anasema bado anaangazia Sporting Lisbon na kushinda mataji akiwa na klabu hiyo huku kukiwa na tetesi kwamba anaweza kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp kama meneja wa Liverpool. (Star)
Mkufunzi wa Getafe Jose Bordalas anasema hayuko wazi juu ya mustakabali wa Mason Greenwood katika klabu hiyo, huku Manchester United bado hawajafanya uamuzi iwapo mshambuliaji huyo wa Uingereza atarejea. (Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images
Sporting Lisbon wanataka pauni milioni 68.5 kumnunua mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 25, huku Arsenal na Chelsea zikiwania. (Mirror on Sunday)
Bayern Munich wamethibitisha kuwa kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, 29, hataongeza mkataba wake katika klabu hiyo hadi watakapopata meneja mpya kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel, ambaye anaondoka mwishoni mwa msimu huu. (Sky Germany, via 90min)
Barcelona na Chelsea wote wanafanya kazi ya kumnunua Mbrazil Estevao Willian mwenye umri wa miaka 16 wa Palmeiras, huku kipengele cha kutolewa kwa winga huyo kinaripotiwa kuwa £51m. (Mirror on Sunday)
Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 32, amechukizwa na kukosa muda wa kucheza Manchester United na ataruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Mirror on Sunday)












