Henry Kissinger: Mwanadiplomasia aliyezua mgawanyiko aliyekuwa na usemi mkubwa kuhusu maswala ya ulimwengu

Chanzo cha picha, Getty Images
Henry Kissinger - ambaye amefariki, akiwa na umri wa miaka 100, nyumbani kwake Connecticut - alikuzua mgawanyiko.
Akiwa mtendaji aliyejitolea kufanya mambo kwa "uhalisia" katika mahusiano ya kigeni, alitumukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel na kulaaniwa vikali kama mhalifu wa vita.
Akiwa Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani na Waziri wa Mambo ya Nje, alifuata kwa bidii sera ya détente - ambayo ilipunguza uhusiano na Umoja wa Kisovieti na Uchina.
Diplomasia yake ya kusafiri ilisaidia kumaliza mzozo wa 1973 wa Waarabu na Israeli; na mazungumzo ya makubaliano ya amani ya Paris yaliiondoa Marekani katika jinamizi la mzozo wake la muda mrefu Vietnam.
Lakini kile wanaomuunga mkono walikielezea kama "Realpolitik" (Siasa halisi), wakosoaji wake waliilaani kuwa inakwenda kinyume na maadili.
Alishutumiwa kwa - angalau - kuunga mkono kimyakimya mapinduzi ya umwagaji damu ambayo yaliipindua serikali ya mrengo wa kushoto nchini Chile, na kufumbia macho 'vita vichafu' vya jeshi la Argentina dhidi ya watu wake.
Aliposikia kwamba Kissinger alikuwa ametunukiwa Tuzo ya Nobel, mcheshi Tom Lehrer alitangaza kwamba "kejeli za kisiasa zimepitwa na wakati".

Chanzo cha picha, Getty Images
Kukimbia Ujerumani ya enzi ya Nazi
Heinz Alfred Kissinger alizaliwa katika familia ya Kiyahudi yenye kipato cha kati mjini Bavaria mnamo tarehe 27 Mei 1923.
Familia hiyo ilichelewa kukimbia unyanyasaji wa Wanazi, lakini ilijiunga na jumuiya ya Wajerumani-Wayahudi mjini New York mnamo 1938.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Henry" alikuwa kijana mwenye haya, ambaye hakuwahi kupoteza lafudhi yake au kupenda soka.
Alihudhuria masomo ya shule ya sekondari usiku, alipokuwa akifanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza brashi zinazotumiwa na vinyozi kazi aliyofanya mchana; na alipanga kusomea uhasibu lakini akasajiriwa jeshini.
Alipopewa kazi ya mwanajeshi wa kikosi cha ardhini , akili na ujuzi wake wa lugha vilimfanya ahudumu kama jasusi jeshini . Kissinger alishuhudia Vita vya Bulge, na akajikuta akiongoza mji wa Ujerumani uliotekwa - licha ya kuwa na tu cheo cha Private tu jeshini.
Kuelekea mwisho wa vita, alijiunga na kikosi cha ujasusi cha Counter Intelligence. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 alipewa jukumu la kuongoza kikosi cha kuwasaka maafisa wa zamani wa Gestapo, ambacho kilikuwa na uwezo kamili wa kuwakamata na kuwazuilia washukiwa.
Vita vidogo vya nyuklia
Aliporudi Marekani, alisoma sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Harvard - na kupanda ngazi kitaaluma.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mnamo 1957, alichapisha kitabu, Vita vya Nyuklia na Sera ya Kigeni - ambacho kilielezea kwamba vita vichache vya atomiki vinaweza kushinda. Akionekana mwenye lugha ya kupinga mashaka, alidai kuwa matumizi ya "mbinu" na "kimkakati" ya aina mpya ya kombora dogo yanaweza kuwa ya busara.
Kitabu hicho kilimfanya atambulike. Safari ndefu ya Kissinger ya kupata umaarufu na ushawishi ilikuwa imeanza; na nadharia ya "vita vidogo vya nyuklia" bado ina ushawishi.
Akawa msaidizi wa gavana wa New York . Na Richard Nixon aliposhinda Ikulu ya White House mnamo 1968, Kissinger alipewa cheo kizuri: Mshauri wa Usalama wa Kitaifa.
Ulikuwa uhusiano mgumu. Rais alihisi kutegemea ushauri wa Kissinger katika uhusiano wa kimataifa, lakini alikuwa na mwelekeo wa chuki dhidi ya Wayahudi aliwashuku Wayahudi wa Marekani.
Vita Baridi ilikuwa katika kilele chake: Armageddon (n vita vya kiama) ilikuwa imeepukwa tu juu ya Cuba, wanajeshi wa Amerika walikuwa bado Vietnam na Urusi ilikuwa imevamia Prague karibuni.
Détente
Lakini Nixon na Kissinger waliamua kupunguza mvutano na Muungano wa Usovieti: kufufua mazungumzo ili kupunguza ukubwa wa maghala yao ya nyuklia.
Wakati huo huo, mazungumzo yalianzishwa na serikali ya China, kupitia Waziri Mkuu Zhou Enlai. Hii iliboresha uhusiano wa (China na Marekani) uliofahamika kama Sino-US, na kuweka shinikizo la kidiplomasia kwa uongozi wa Usoviet - ambao ulimuogopa jirani yake mkubwa.
Juhudi za Kissinger zilipelekea moja kwa moja kufanyika kwa safari ya kihistoria ya Nixon nchini China mwaka 1972, alipokutana na Zhou na Mao Zedong - na kuhitimisha miaka 23 ya kutengwa na uhasama wa kidiplomasia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vietnam
Wakati huo huo, Marekani ilikuwa ikijaribu kujitoa katika Vietnam.
"Amani pamoja na heshima" ilikuwa ahadi kuu ya uchaguzi wa Nixon; na Kissinger alikuwa amehitimisha kwa muda mrefu kuwa ushindi wowote wa kijeshi wa Marekani haukuwa na maana yoyote - kwani haungeweza "kufikia ukweli wa kisiasa ambao ungeweza kustahimili uondokaji wetu wa mwisho."
Aliingia katika mazungumzo na Vietnam Kaskazini, lakini alikubaliana na Nixon kufanya mashambulizi ya siri ya mabomu dhidi ya Kambodia isiyoegemea upande wowote - katika jitihada za kuwanyima wakomunisti wanajeshi na vifaa.
Sera hiyo ilisababisha vifo vya raia wasiopungua 50,000; na kukosekana kwa uthabiti wa nchi kulisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Kambodia na utawala wa kikatili wa Pol Pot.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati wa msururu wa mazungumzo magumu na Viet Cong mjini Paris, Kissinger - ambaye alikuwa wakati huo waziri wa mambo ya nje - alijadili kujiondoa kwa jeshi la Marekani katika Vietnam Kusini.
Hilo lilimwezesha kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel - pamoja na Le Duc Tho wa Vietnam Kaskazini - tuamuzi ambao ulipingwa vikali na wanaharakati wa amani.
Kissinger alikubali tuzo Marekani waliouawa kwenye vita. Miaka miwili baadaye, wakati majeshi ya kikomunisti yalipoivamia Vietnam Kusini, alijaribu kuirejesha.
Siasa halisi
Diplomasia yake ya usafiri ilileta usitishaji vita kufuatia vita vya Waarabu na Israeli vya 1973.
Mfumo wa siri wa Nixon wa Ikulu ya White House wa kurekodi taarifa wa ulimnasa Waziri Mkuu wa Israel Golda Meir akitoa shukrani za kutosha kwa jinsi yeye na Kissinger walivyoitendea nchi yake.
Lakini baada ya kuondoka, kanda hizo zilifunua Realpolitik (siasa halisi )nyeusi zaidi. Iwe Kissinger au Nixon hawakuwa na nia yoyote ya kuweka shinikizo kwa Muungano wa Usovieti kuwaruhusu Wayahudi wa Kirusi kutafuta maisha mapya katika Israeli.
"Kuhama kwa Wayahudi kutoka Muungano wa Usovieti sio lengo la sera ya nje ya Marekani," alisema Kissinger. "Na kama watawaweka Wayahudi kwenye vyumba vya gesi katika Muungano wa Kisovieti, sio wasiwasi wa Marekani. Labda ni wasiwasi wa kibinadamu."

Chanzo cha picha, PICHA ZA GETTY 515114332. HAKUNA ADA
Kuchaguliwa kwa Salvador Allende kama rais wa Chile, hata hivyo, kuliisumbua Marekani. Serikali mpya ilikuwa inaiunga mkono Cuba na makampuni ya Kimarekani yaliyotaifishwa.
Shirika la ujasusi la Marekani CIA ilifanya operesheni za siri nchini Chile, katika jaribio la kuyasaidia makundi ya upinzani kuipindua serikali mpya. Kissinger aliongoza kamati iliyoidhinisha hatua hiyo.
"Sioni kwa nini tunahitaji kusimama karibu na kutazama nchi ikiingia katika ukomunisisti kutokana na kutowajibika kwa watu wake," alisema. " Ni muhimu sana kwa wapiga kura wa Chile kuachwa wajiamulie wenyewe."
Hatimaye, wanajeshi waliingia; na Allende alifariki katika mapinduzi makali ambayo yalilipelekea Jenerali Pinochet kutwaa mamlaka. Wanajeshi wake wengi walibainiwa kuwa walilipwa na CIA.
Katika miaka ya baadaye, Kissinger mwenyewe alifuatiliwa na mahakama kadhaa zinazochunguza unyanyasaji wa haki za binadamu na vifo vya raia wa kigeni chini ya utawala wa kijeshi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwaka mmoja baadaye, Kissinger alitamsuhudia Richard Nixon aliyekuwa akitokwa na machozi akiondoka Ikulu ya White House - akizongwa na kashfa ya Watergate. Mrithi wake, Gerald Ford, alibaki naye kama katibu wa serikali.
Aliweka shinikizo kwa serikali ya wazungu wachache ya Rhodesia kuachia madaraka, lakini alishutumiwa kwa kupuuza "kutoweka" kwa junta -wakosoaji wa serikali ya Argentina
Nguvu: Aphrodisiac ya mwisho
Utata ulimfuata baada ya kuondoka madarakani mwaka wa 1977: ofa aliyokuwa amepewa ya kuwa mwenyekiti katika Chuo Kikuu cha Columbia iliondolewa baada ya maandamano ya wanafunzi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Alikua mkosoaji mkubwa wa sera ya nje ya Jimmy Carter na Bill Clinton, akisema marais wanataka kufikiwa kwa haraka kwa amani katika Mashariki ya Kati. Kwa Kissinger, hiyo inaweza kutokea inchi kwa inchi tu.
Baada ya 9/11, George W Bush alimuomba awe mwenyekiti wa uchunguzi wa mashambulizi ya New York na Washington, lakini alilazimika kuacha kazi hiyo ndani ya wiki - baada ya kukataa kufichua orodha ya wateja wake na kujibu maswali kuhusu migogoro ya maslahi.
Alifanya mikutano na Rais Bush na Makamu wa Rais Dick Cheney, ili kuwashauri kuhusu sera nchini Iraq kufuatia uvamizi wa 2003. "Ushindi dhidi ya waasi," aliwaambia, "ndio mkakati pekee wa kuondoka."
Daima akiwa na ushawishi mkubwa, alimweleza Donald Trump kuhusu masuala ya kigeni baada ya kuchaguliwa kwake mwaka wa 2017 - akipendekeza, kati ya mambo mengine, kukubaliwa kwa uvamizi wa Vladimir Putin wa Crimea.
Ingawa, hadi alipofikia umri wa miaka 100 mnamo 2023, alikuwa amebadilisha maoni yake juu ya Ukraine. Baada ya uvamizi wa Urusi, alisema kuwa nchi ya Rais Zelensky inapaswa kujiunga na Nato baada ya amani kupatikana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Henry Kissinger alikuwa na orodha kubwa ya mawasiliano na mwenye mazungumzo yaliyojaa ucheshi . "Mamlaka", kama alivyopendelea kusema , ni "hamu ya ngono ".
Alijikuta katikati ya mamlaka wakati wa matukio muhimu zaidi ya karne iliyopita.
Lililoakarisha wengi ni kwamba , hakupenda kujutia kuhusu msimamo wake wa kulinda maslahi ya Marekani, na kutetea msimamo wake kuhusu maisha ya watu nchini.
"Nchi inayodai ukamilifu wa kimaadili katika sera yake ya kigeni", aliwahi kutamka, "haitafikia ukamilifu wala usalama".
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












