Mke wangu aliridhia nioe mke wa pili

Maelezo ya video, Mke wangu aliridhia nioe mke wa pili
Mke wangu aliridhia nioe mke wa pili
Iliyochapishwa

Kwa miaka mingi ndoa za zaidi ya mke mmoja zilishamiri katika jamii za kiafrika kutokana na mila na itikadi za baadhi ya jamii na hata baadhi ya dini lakini katika miaka ya hivi karibuni kuwa na zaidi ya mke mmoja ni suala linaloonekana kama lenye utata.

Familia moja ya mume mmoja na wake wawili Takid Master walizungumza na mtangazaji kinara wa BBC Roncliffe Odit kuhusu jinsi wanavyoishi katika uhusiano wao.