Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mchuuzi wa Nigeria aliyesafirishwa Uingereza kwa njama ya kutolewa figo
Seneta wa Nigeria Ike Ekweremadu na mke wake Beatrice wamepatikana na hatia ya kumtumia vibaya kijana mdogo kutoka katika familia masikini kwa kumleta London nchini Uingereza kutoa kutolewa figo kama zawadi. Huku wakisubiri hukumu , BBC inafichua maelezo kuhusu kisa hiki.
Mwanafunzi Sonia Ekweremadu anaonekana kuwa na maisha ya mazuri kutokana na wazazi matajiri nchini walioko katika mfumo wa siasa nchini Nigeria, na hivyo basi alipelekwa katika Chuo kikuu cha Uingereza – lakini alikuwa mgonjwa sana na alikuwa anahitaji kufanyiwa uoandikizaji wa figo. Baba yake , Ike Ekweremadu, alimlilpalimlipa mtu ambaye angemsaidia kuhakikisha mwanaye anapata figo maelfu ya pauni ili kupanga njama ya kumoata mtu atakayetolewa figo kwa ajili ya binti yake.
Daniel, ambaye jina lake halisi haliwezi kufichuliwa kutokana na sababu za kisheria, alikulia katika familia kubwa iliyoko katika kijiji cha Nigeria, ambacho hakina maji ya bomba wala umeme.
Katika umri wa miaka 15 alikuwa kiuza bidhaa za simu kwa niaba ya mwenye duka katika jiji kuu la Nigeria Lagos na kutuma pesa nyumbani kwao kijijini.
Mnamo mwaka 2022, akiwa na umri wa miaka 21, aliingia kwenye kituo cha polisi karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Uingereza Heathrow, akiwa amechoka, bila makazi na alikuwa mwenye uoga mkubwa. Aliiambia polisi kuwa alikuwa ametoroka kwasababu watu walikuwa wanataka kuchukua moja ya mafigo yake.
Ekweremadu na mke wake walimtafuta mtu wa kuwasaidia ku kutimiza haja yao ya kupata fikgo. Alikuwa ni Dr Obinna Obeta, ambaye Julai 2021, binafsi alikuwa amepokea msaada wa figo, walitaka atumie watu aliowafahamu kuhakikisha hili linafanyika: Daktari mwrafiki yahe Mnigeria katika Cambridge alichangisha pesa, na kijana mdogo wa kutoa figo alipatina nchini Nigeria, na operesheni ya kisiri ilifanyika katika hospitali ya London's Royal Free Hospital.
Familia ya Ekweremadu ilitaka Dkt Obeta t kurudia mchakato huo kwa ajili ya Sonia. Dkt Obeta alimuomba mtoaji wa figo alilopewa kumtafuta mtu ambaye yuko tayari kutoa msaada wa figo kwa Sonia. Akampendekea Daniel.
Daniel alidai kuwa Dkt Obeta alikuwa ameahidi kumpeleka Uingereza na hakuwahi kutaja kuhusu upandikizaji wa figo. "Aliniambia nitakuwa ninaishi nyumbani kwake na kumfanyia kazi…aliniambia niwafahamishe watu kuwa ninakuja Uingereza’’ ," Daniel aliiambia mahakama.
Wakati Dkt Obeta alimtaka Daniel afanyiwe vipimo vya kimatibabu, ambavyo Daniel alidhani vilikuwa ni kwa ajili ya maombi ya visa.
Visa yake ya kuelekea Uingereza ilipatikana Januari 2022. Habari njema, Daniel alifikiri kuwa msaada wa Dkt Obeta ulikuwa kama ‘’umetoka kwa Mungu’’ alisema.
Wakati alipofika London, hatahivyo, ilibidi alale kwenye viti vya Dkt Obeta na anasema Dkt Obeta alimtumikisha kama mfanyakazi wa nyumbani.
Wakati huo, Ike Ekweremadu, akiwasiliana naye kupitia babakaka yake, daktari alikuwa akitakiwa kumlipa Dk Obeta karibu pauni 2,000. Daniel alitakiwa kupokea pauni 6,000kwa ajili ya kutolewa figo lake, huku upasuaji , katika hospitali ya kibinafsi ya Royal Free katika kitengo cha matibabu binafsi, ungegarimu pauni 80,000.
Nchini Uingereza sheria ya kupasua mwili wa binadamu kwa ajili ya kumlipa au kuwalipa watoaji , inasema ni lazima mtoaji wa viungo vya mwili na mpokeaji ni lazima wawe ni watu wa familia moja au wenye uhusiano wa karibu kihisia.
Ekweremadus alionekana kujua hili. Walimkaribisha Daniel kwa chakula cha mchanakatika mgahawa mmoja wa chakula cha Afrika Magharibi uliopo kusini mwa London, wakamwambia avae nadhifu. Sonia alikuwa pale na picha yake ilichukuliwa na Daniel.
Wazazi wake Sonia na Dkt Obeta walikuwa wanajifanya kuwa mabinamu. Sonia alikuwa anafahamu fika ‘’maigizo haya’’
Mtoaji, mpokeaji na daktari wa ngazi ya juu wa figo Dkt Peter Dupont wote pamoja walikutana kwa mara ya kwanza ana kwa ana tarehe 22 Februari 2022.
Daniel aliliambia jopo la mahakama ya Old Bailey jury: "Aliniuliza iwapo ninajua kuwa ninaenda kufanya upandikizaji wa figo. Nilishtuka. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kusikia kuhusu upandikizaji wa figo ." Anasema pia ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kusikia jina Ekweremadu: "Nilikuwa ninalia na kutetemeka."
Wakati huo huo, Ekweremadu na mke wake pamoja na DR Obeta walimtumia mtu Daniel ili kuboresha hadithi yake ya udanganyifu, ambapo walimlipa mkalimani kumfundisha maneno atakayomwambia daktari watakapokutana.
Daktari wa pili , Dkt Philip Masson, pia alikuwa na wasi wasi huenda Daniel hakuelewa hatari za kutoa msaaada wa figo. Dkt Dupont alisitisha mchakato, alibaini kuwa Daniel alikuwa na "matatizo ya kiakili na asingeweza kudhibiti hisia zake ", "hakuwa na uhusiano na mpokeaji wa figo ", hakuwa na uelewa wa mtu mzima na hakuweza kufadhili matibabu yake ya siku zijazo .
Katika kipindi cha wiki kadhaa , Ike Ekweremadu alikuwa akimtumia jumbe za picha binti yake Sonia za watu wacheche ambao wangeweza kumtolea msaada wa figo. Alijibu : "Mweusi anaonekana bora zaidi. Mweupe anaonekana kana kwamba anaweza kutoroka."
Wakati huo huo, Daniel alitembelewa na wanaume wawilikatika makazi ya Dkt Obeta kusini mwa London.
Alisema mmoja wao , ambaye ni daktari, alimkanda kkwenye tumbo lake, jambo lililomtia uoga sana Daniel, ambaye alifikiri kuwa huenda wakajaribu kumtoa figo lake pale atakaporudi Nigeria.
Alikimbilia polisi na Ike, Beatrice na Sonia walikamatwa, pamoja na Dkt Obeta.
Katika mahakama ya Old Bailey, watatu ao bado hawajapatikana na hatia ya kuvunja sheria ya utumwa mamboleo kwa kumleta Daniel nchini Uingereza kutoa figo kwa ajili ya Sonia.
Upandikizwaji wa figo wa Sonia ulitibuliwa – lakini hospitali ya Royal Free awali ilifanya upasuaji ambao ulimuwezesha Dkt Obeta ambaye alidanganya kuwa ni ndugu wa mtoaji kupata figo.
Mtu muhimu katika kesi zote ni daktari mwenye makao yake Cambridge- Chris Agbo, ambaye anaendesha biashara ya kando ya kuwasaidia wagonjwa kutoka mataifa ya kigeni kupata matibabu nchini Uingereza .
Ilikuwa ni Dkt Agbo ambaye alichangisha pesa kwa ajili ya uandikizaji wa figo kwa Dkt obeta.
Kwa kijana huyo mdogo Mnigeria ambaye alisafirishwa Kwenda London kutoa figo kwa Dkt Obeta , BBC ilimpata akiishi katika nyumba ndogo ya gorofa mashariki mwa London, akiwa bado mwenye maumivu na mdhaifu, athari za kutoa kiungo muhimu cha mwili wake.