Ni sehemu gani ya mwili inauma zaidi wakati wa kuchora tattoo?

Gucci akitolewa tattoo na mashine ya Laser
Iliyochapishwa

Mwalimu wa sayansi na baiolojia wa Uingereza Natalie Wilsher ana tattoo ya Albert Einstein kwenye mkono wake.

Pia anazo nyingine kwenye miguu, viganja vya mikono na vifundo vya miguu.

Kati ya tatoo zote alizokuwa amechora, zilizokuwa zinauma sana ni zile za miguuni na kwenye vifundo vya miguu.

"Maumivu ni njia ya mwili wetu kujikinga, na mishipa yetu ndiyo hugundua hilo," anaeleza mwalimu huyo kwenye podcast ya BBC inayoitwa "Nifundishe somo".

Sehemu ya mwili iliyo na uchungu zaidi kuchora tatoo ni ile ina mafuta kidogo na mishipa zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sehemu ya mwili iliyo na uchungu zaidi kuchora tatoo ni ile ina mafuta kidogo na mishipa zaidi

"Itakuwa na maumivu zaidi kujichora tattoo sehemu ambapo kuna mafuta kidogo na miisho ya neva zaidi," aeleza, katika mazungumzo na watangazaji Bella Mackie na Greg James.

Mbali na miguu na vifundo vya mguu, chini ya goti, kwapa na mbavu pia zimo kwenye orodha ya maeneo nyeti, anasema Wilsher, ingawa yote inategemea hisia za kila mtu.

"Mishipa ya eneo ambalo linatobolewa wakati tattoo inachorwa hutuma ishara ya maumivu kwenye ubongo," mwalimu anaongeza.

Tattoo ya kwanza

Hata hivyo, matokeo ya mtu mmoja katika mchakato wa kupata tattoo si lazima kulinganishwa au yafanane na mwingine.

"Kiwango cha kustahimili maumivu ni tofauti kabisa kutoka kwa mtu mmoja hadi mtu mwingine," anasema.

Wilsher anashangaa jinsi walivyoponya majeraha yaliyosababishwa na kupasuka kwa ngozi na kudhani kuwa ilichukua miezi kupona.

Ötzi, aliyeishi kabla ya piramidi ya kwanza ya Misri kujengwa, ndiye mummy wa zamani zaidi aliyehifadhiwa kwenye barafu.

Chanzo cha picha, SOUTHTYROLARCHAEOLOGYMUSEUM\EURAC\M.SAMAD

Maelezo ya picha, Ötzi, aliyeishi kabla ya piramidi ya kwanza ya Misri kujengwa, ndiye mummy wa zamani zaidi aliyehifadhiwa kwenye barafu.

"Inashangaza kwamba nyakati hizo, zama za mawe na zama za shaba waliweza kufanya tattoos hizo na hawakuumwa kutokana na kufanya hivyo. Inashangaza kwamba walikuwa na ujuzi huo," anaongeza.

Baada ya muda, tattoo zikawa njia ya kila mtu kusimulia hadithi yake mwenyewe.

"Simulizi zinasema kwamba Kapteni James Cook, mwishoni mwa Karne ya 18 katika safari zake za kuzunguka Pasifiki, aliona watu tofauti wakiwa na tattoo tofauti. Inasemekana kwamba 90% ya wafanyakazi wake walichora tattoo kuashiria safari yao," aeleza mwalimu huyo wa shule ya upili.

Kiwango za uchungu kinategemea kutoka mtu mmoja hadi nyingi

Chanzo cha picha, Getty Images

Mabaharia katika jeshi la wanamaji la Uingereza walirithi mila hii na kuanza kuchora tattoo za safari zao, ambazo zilitengenezwa kwa mkojo na baruti kwa matayarisho ambayo hapo awali yaliitwa wino wa baharini, anasema Wilsher.

Mwishoni mwa Karne ya 19, mashine ya tattoo ilitokana mashine ya kuchapisha (Printer) ya Thomas Edison.

"Iliundwa mwaka wa 1875, na tangu wakati huo haijabadilika sana. Bado inaweza kuchubua ngozi kati ya mara 50 na 3,000 kwa dakika."

Wino wa tattoo huingizwa kwenye dermis, ambapo mishipa inayohusika na maumivu iko

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wino wa tattoo huingizwa kwenye dermis, ambapo mishipa inayohusika na maumivu iko

Kiungo kikubwa zaidi katika mwili

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ngozi ni chombo kikubwa zaidi cha mwili, karibu 50% ya uzito wa mwili na tabaka la juu zaidi hutengenezwa upya kila baada ya siku 28. Kwa nini wino haufifii baada ya kuumwaga kwenye ngozi hiyo?

Profesa Wilsher anafafanua kuwa ngozi ina tabaka tatu kuu: epidermis ya juu; dermis katikati ambapo mishipa ya damu, tezi za jasho, vinyweleo na mishipa hupatikana na sehemu ya ndani na nene ambayo ni hypodermis, tabaka la mafuta ya ngozi.

"Wino wa tattoo hudungwa kwenye dermis, ambapo mishipa inayohusika na maumivu ipo. Tatoo hukaa [hazififii] kwa sababu safu ya kati ya ngozi inalindwa na epidermis safu ya juu," anaelezea.

Wilsher anabainisha kwamba wakati wino unapoingizwa kwenye ngozi ya kati, "mwili wako unasema, 'Ee mungu wangu, nimepata jeraha.'Na hutuma macrophages, chembe nyeupe za damu, katika eneo hilo na hujaribu kula wino huo na kisha kuutuma kwenye mkondo wa damu."

Hata hivyo, rangi za wino ni kubwa sana kwa macrophages kuondoa, kwa hivyo hukwama hapo. "Ndiyo maana tunaweza kuziona kupitia epidermis," anaongeza.