Teknolojia ilivyosaidia kutenganisha mapacha walioungana ubongo

Iliyochapishwa

Jozi ya mapacha ambao walikuwa wameungana kichwani walitenganishwa kwa ufanisi kwa msaada picha halisi (virtual reality ) kutoka kwa madaktari wa nchi nyingine.

Upasuaji wa watoto Bernardo na Arthur Lima wenye umri wa miaka 3, ulifanyika Rio de Janeiro, kwa maelekezo kutoka Hospitali ya Great Ormond Street huko London ambayo waliyapata moja kwa moja kupitia picha katika chumba kilichowekwa vifaa vya teknolojia hiyo.

Kwa miezi kadhaa, timu za madakrati wa upasuaji zilijaribu aina tofauti za mbinu kwa kutumia picha za mapacha hao katika teknolojia ya picha ambayo ilitegemea uchunguzi wa CT na MRI.

Daktari wa upasuaji Noor ul Owase Jeelani alielezea kuwa ni kama "kitu kutoka katika anga za juu".

Bernardo na Arthur ni moja ya michakato mgumu zaidi ya utengano ambao umefanikiwa, kulingana na taasisi ya Jeelani, Gemini Untwined.

Alisema kuwa kwa mara ya kwanza, kikundi cha madaktari wa upasuaji kutoka nchi tofauti walivaa vifaa vya sauti na kufanya kazi ya upasuaji pamoja katika ‘chumba kilichowekwa teknolojia inayoonesha uhalisia wa upasuaji huo ‘

Mapacha hao wa Siamese walifanyiwa upasuaji mara 7: wa mwisho alihitaji upasuaji wa zaidi ya saa 27 na timu ya zaidi ya wataalamu 100 wa afya.

"Ni kama kuishi kwenye sayari ya Mars"

Akielezea kipengele cha video wakati wa upasuaji huo, Jeelanie aliliambia shirika la habari la PA: "Inashangaza. Inapendeza sana kuona zoezi zima na kufanya upasuaji na kutowaweka watoto katika hatari ya aina yoyote."

"Unaweza kufikiria jinsi hii inavyotia moyo kwa madaktari wa upasuaji."

"Kwa njia fulani, shughuli hizi zinachukuliwa kuwa ngumu zaidi kwa wakati wetu na baada ya kuifanya katika hali halisi ya picha ni kama suala la kuishi kwenye Mars."

Alisema uchunguzi wa mwili wa watoto hao wakiume mapacha ilikuwa ngumu kutokana na ukuaji wa kovu baada ya majaribio ya awali kushindwa kuwatenganisha na kwamba "anaogopa sana" kuhusu upasuaji huo mgumu.

Jeelani alisema "alihuzunishwa sana" lakini baada ya upasuaji huo wa saa 27, ambapo alichukua mapumziko mara nne tu ya dakika 15 kula na kunywa maji, ilikuwa "ajabu" kuona familia nzima ikiwa na furaha baadaye.

Aliongeza kuwa, kama inavyotokea katika kesi zote za mapacha walioungana, shinikizo la damu la watoto na mapigo ya moyo "yalipigwa shoti" hadi walipounganishwa siku 4 baadaye na kushikana mikono.

Mapacha hao walikuwa wakiendelea vyema hospitalini na wataendelea kupata matibabu kwa miezi sita.

Kubadilisha maisha  

Huu ni upasuaji wa sita kwa Jeelani akiwa na Gemini Untwined, baada ya kufanya upasuaji wa mapacha nchini Pakistan, Sudan, Israel na Uturuki.

Aliongoza utaratibu huo pamoja na Dk. Gabriel Mufarrej, mkuu wa upasuaji wa watoto katika Taasisi ya Ubongo ya Jimbo la Paulo Niemeyer nchini Brazili.

Mufarrej alisema hospitali anayofanyia kazi imekuwa ikiwahudumia watoto hao kwa miaka miwili na nusu. Aliongeza kuwa kutenganishwa kutabadilisha maisha yao.

"Tangu walipofika Rio miaka miwili na nusu iliyopita kutoka nyumbani kwao katika mkoa wa Roraima, wazazi wa watoto hao wamekuwa sehemu ya familia hapa hospitalini. Tunafurahi kwamba upasuaji ulikwenda vizuri. 

Bernardo na Arthur, karibu umri wa miaka minne, ndio mapacha wakubwa zaidi wa waliungana kichwani katika ubongo kutenganishwa.

Kulingana na shirika hilo, mtoto mmoja kati ya watoto 60,000 wanaozaliwa kama mapacha walioungana na ni asilimia 5 tu kati yao wana wmeunga sehemu za kichwani.