Urusi na Ukraine: Maafa makubwa yaripotiwa mapigano yakiendelea Bakhmut

Chanzo cha picha, afp via getty images
Ukraine na Urusi zote zimeripoti hasara kubwa kwa kila mmoja, huku vita vya kuudhibiti eneo la kati la mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine vikiendelea.
Moscow imekuwa ikijaribu kuudhibiti mji huo wa mashariki mwa Ukraine kwa miezi kadhaa.
"Katika muda wa chini ya wiki moja, kuanzia Machi 6, tulifanikiwa kuua zaidi ya wanajeshi 1,100 wa adui Bakhmut pekee, hasara isiyoweza kutenduliwa ya Urusi, huko karibu na Bakhmut," Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema katika hotuba yake ya usiku ya video.
Aliongeza kuwa "wanajeshi 1,500 wa Urusi walijeruhiwa vibaya vya kutosha kuondolewa kwenye mapigano."
Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema kuwa vikosi vya Urusi vimewaua "zaidi ya wanajeshi 220 wa Ukraine".
Kuteka mji huo kungeleta Urusi karibu na lengo lake la kudhibiti eneo lote la Donetsk, mojawapo ya mikoa minne ya mashariki na kusini mwa Ukraine ambayo Urusi ilinyakua Septemba iliyopita baada ya kura za maoni ambazo nchi za Magharibi ziliziona kuwa "udanganyifu".
Kama Urusi, Ukraine pia imeweka umuhimu wa kisiasa kwa Bakhmut, huku Rais Zelensky akiufanya mji huo kuwa "ishara ya upinzani".
Alipotembelea Washington mwezi Desemba, aliuita "ngome yetu ya motisha" na akawasilisha bendera ya Bakhmut kwa Bunge la Marekani.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kamanda wa vikosi vya ardhini vya Ukraine, Kanali Oleksandr Sersky, alisema kuwa Kundi la Wagner la Urusi linashambulia vikosi vyake kutoka pande kadhaa, katika jaribio la kupenya ulinzi na kusonga mbele hadi maeneo ya kati ya mji.
Sersky alieleza kuwa hali ya Bakhmut ilikuwa ngumu, akiongeza kuwa vikosi vyake vinazuia majaribio yote ya Urusi ya kuudhibiti.
Kundi la Wagner lilikuwa katikati ya shambulio la Urusi dhidi ya Bakhmut. Kamanda wake, Yevgeny Prigozhin, alielezea wasi wasi wake kuhusu sifa yake na ya jeshi lake la kibinafsi kuchukua Bakhmut.
Siku ya Jumapili, alisema kuwa hali ya jiji ni "ngumu, ngumu sana, adui anapigana kila mita ... lakini tunasonga mbele na tutasonga mbele."
"Kadiri tunavyokaribia katikati mwa jiji, ndivyo mapigano yanavyozidi kuwa makali," alisema katika rekodi ya sauti iliyowekwa kwenye Telegram.
Baada ya kudhibitiwa kwa Bakhmut, alisema, "tutaanza kuajiri watu wapya kutoka mikoani.
Siku ya Jumamosi, Taasisi ya Utafiti wa Vita, taasisi ya wataalam ya Marekani, iliripoti kwamba mashambulizi ya Moscow yalikwama.
"Wapiganaji wa Wagner Group watajipata wamekwama zaidi katika maeneo ya mijini, na hivyo kupata ugumu wa kufanya maendeleo makubwa," aliongeza.
Kulikuwa na takriban watu 70,000 waliokuwa wakiishi Bakhmut kabla ya vita kuanza, lakini ni elfu chache tu waliosalia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jiji hilo lilikuwa maarufu kwa madini yake ya chumvi na kiwanda chake kikubwa cha divai.
Katika muktadha unaohusiana, watu walio na habari walisema kuwa Rais wa China Xi Jinping anapanga kusafiri hadi Urusi kukutana na mwenzake, Vladimir Putin, mapema kama tu kama wiki ijayo.
Mshirika mkuu wa Rais Vladimir Putin alisema Jumatatu kwamba anashuku mabomba ya Nord Stream yalilipuliwa na kundi linalounga mkono Ukrainian, na akasema Moscow bado haijui ni aliyehusika.
Kuhusu makubaliano ya kuuza nafaka ya Ukraine kuvuka Bahari Nyeusi, Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar alisema anaamini kuwa makubaliano hayo yatarefushwa zaidi ya tarehe ya mwisho ya Machi 18.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilisema Jumapili kwamba wawakilishi wa Urusi bado hawajashiriki katika mazungumzo ya kurefusha mpango huo.
Kwa upande wake, Kamishna wa Viwanda wa Ulaya Thierry Breton alisema Jumatatu kwamba Umoja wa Ulaya "utahakikisha" kuongeza uzalishaji wa silaha kwa Ukraine, ambayo inasimamiwa na "viwanda 15 katika nchi 11" ambazo ni wanachama wa umoja huo.
"Lazima tuchukue hatua haraka sana, kwani vita vya kutisha vya Ukraine vilivyoanzishwa na (Rais wa Urusi) Vladmir Putin vinakaribia kugeuka kuwa vita vya ana kwa ana, na bila shaka kuna mbio za kutuma kiasi kikubwa zaidi cha risasi kutoka pande zote mbili," aliiambia redio ya Ufaransa RMC siku ya Jumatatu. Alisema kuwa Ukraine "hutegemea" Ulaya kuwapa risasi.
"Umuhimu wa kupigana”

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuhusiana na hilo, baadhi ya watu nchini Ukraine wanashangaa juu ya hitaji la vikosi vya Kiev kupigania jiji hili, na maana yake katika suala la hasara katika safu zake.
Kuna uwezekano kwamba hasara hizi zitaongezeka ikiwa vikosi vya Urusi vitaweza kuizingira Bakhmut, baada ya kufanikiwa kukata njia kadhaa muhimu za kupeleka vifaa kwa wanajeshi wa Ukraine.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alionya wiki iliyopita kwamba Bakhmut unaweza kuanguka "siku zinazokuja”.
Kwa uongozi wa kijeshi wa Ukraine, ni suala la kuhifadhi Bakhmut kwa muda mrefu iwezekanavyo, ili Urusi itumie huko idadi kubwa zaidi ya wanajeshi wake, silaha na risasi, na kujikuta dhaifu wakati Ukraine inapozindua mashambulizi yake.
Ukraine ni nchi ya tatu kwa silaha
Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI) ilisema kuwa uagizaji wa silaha barani Ulaya uliongezeka, ukiongezeka karibu maradufu mwaka 2022.
Kiev imekuwa kituo cha tatu kwa silaha, na peke yake ilichangia asilimia 31 ya uagizaji wa silaha barani Ulaya na asilimia 8 ya mikataba ulimwenguni, kulingana na takwimu zilizopokelewa na AFP kutoka kwa taasisi hiyo katika mfumo wa ripoti yake ya kila mwaka, baada ya kutorekodi uagizaji wa silaha muhimu kabla ya vita.
Taasisi hiyo ilisema kuwa uagizaji wa bidhaa za Ukraine, pamoja na vifaa vinavyotolewa na nchi za Magharibi, uliongezeka kwa zaidi ya mara sitini mnamo mwaka 2022.
Jinping anaweza kufanya ziara Urusi
Katika muktadha unaohusiana, watu walio na habari walisema kuwa Rais wa China Xi Jinping anapanga kusafiri hadi Urusi kukutana na mwenzake, Vladimir Putin, mapema kama tu kama wiki ijayo.
Mshirika mkuu wa Rais Vladimir Putin alisema Jumatatu kwamba anashuku mabomba ya Nord Stream yalilipuliwa na kundi linalounga mkono Ukrainian, na akasema Moscow bado haijui ni aliyehusika.
Kuhusu makubaliano ya kuuza nafaka ya Ukraine kuvuka Bahari Nyeusi, Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar alisema anaamini kuwa makubaliano hayo yatarefushwa zaidi ya tarehe ya mwisho ya Machi 18.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilisema Jumapili kwamba wawakilishi wa Urusi bado hawajashiriki katika mazungumzo ya kurefusha mpango huo.












