Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini ziara ya Joe Biden nchini Saudia imekuwa mwiba kwa taifa hilo
Siku moja baada ya Ikulu ya White House kutangaza safari ya Rais Joe Biden nchini Saudi Arabia, kundi la wanaharakati lilikusanyika kuubatiza mtaa nje ya ubalozi wake wa Washington "Khashoggi Way".
Walitangaza kuwa itakuwa ukumbusho wa kila siku kwa wanadiplomasia "waliojificha nyuma ya milango hiyo" kwamba serikali ya kifalme ilihusika na mauaji ya 2018 ya mwandishi wa habari wa Saudi na mkosoaji wa serikali Jamal Khashoggi.
Na walishutumu uamuzi wa Rais Biden kukutana na mtu aliyelaumiwa na ujasusi wa Marekani kuwa ndiye aliyeamuru mauaji hayo - Mwanamfalme Mohammed bin Salman, anayejulikana sana kama MBS.
"Ikiwa itabidi kumpaka mtu mafuta zaidi ya kuheshimu kanuni na manufaa ya maadili," alisema mchumba wa Khashoggi Hatice Cengiz katika hotuba yake iliyosomwa kwenye hafla hiyo, "unaweza angalau kuuliza mwili wa Jamal uko wapi? Je, hastahili kuzikwa ipasavyo?"
Kwanini hatua hii ina utata?
Mahusiano ya miongo kadhaa ya Marekani na Saudi Arabia yamehusisha biashara kati ya maadili ya Marekani na maslahi ya kimkakati.
Lakini Rais Biden alisisitiza waziwazi haki za binadamu katika uhusiano huo, na sasa, anapokubali ukweli wa kisiasa, anakabiliwa na hatari ya kupoteza Washington kutokana na hasira ya kitendo hicho. Mwandishi wa habari na mkosoaji mashuhuri wa mwana mfalme wa Saudia Khashoggi aliuawa na kukatwa vipande vipande katika ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul.
Akiwa mgombea urais, Bw Biden alichora mstari , akiapa kuhakikisha kuwa ufalme huo ‘umetengwa’ kwa sababu ya rekodi yake mbaya ya haki za binadamu. Alitumia maneno hayo makali kujitofautisha na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliyeikumbatia Saudi Arabia bila kipingamizi. Bw Trump aliwahi kujigamba kuwa "alimuokoa [MBS'] kutoka kwa kilio cha kifo cha Khashoggi.
Lakini ni nini kilichosababisha mabadiliko hayo?
Mara baada ya kutawala, Bw Biden alisitisha uuzaji wa silaha na akakataa kabisa kuzungumza na mwanamfalme huyo. Lakini kulikuwa na shaka ndani ya utawala kwamba hii ilikuwa mbinu endelevu kwa mtu ambaye labda hivi karibuni atakuwa mtawala wa Saudi. Mabadaliko yalianza kufanyika mwaka uliopita, na vita vya Urusi nchini Ukraine vilimsukuma rais wa Marekani kuwa muhusika.
Kupanda kwa bei ya mafuta ndio iliosababisha msukumo. Marekani ilitoa wito kwa Saudia kuzalisha mafuta zaidi ili kusaidia kupunguza bei. Awali Riyadh ilipinga maombi hayo. Lakini siku chache kabla ya safari ya rais kutangazwa, Opec Plus, kundi la wazalishaji wa mafuta ambalo Saudi Arabia ni kiongozi mkuu, liliidhinisha ongezeko la kawaida la uzalishaji.
Wachambuzi wanasema kunaweza kuwa na makubaliano ya kiksiri na Saudis kuhusu ongezeko jingine kwasababu makubaliano yaliopo yanakamilika mwezi Septemba. Lakini hilo haliwezi kuzungumziwa katika safari safari hii.
Lengo kuu ni kuhusu usimamizi wa muda mrefu wa masoko ya nishati katika nyakati hizi zenye msukosuko, alisema Ben Cahill, mtaalam wa usalama wa nishati katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa (CSIS).
‘’Nadhani kuna msukumo ndani ya ikulu ya Whitehouse kuchukua hatua na kuanza kufanya majadiliano endelevu na washirika wengi katika ulimwengu wa mafuta na hilo linaaanza na Saudia,’’alisema
Je anataka nini?
Lakini iwapo ziara hiyo haitakuwa na athari za moja kwa moja katika vituo vya mafuta vya taifa hilo, je ni athari gani zitakazoathiri hatua hiyo ya rais.
Bwana Biden amepuuza umuhimu wa kukutana na MBS, akisisitiza kwamba atahudhuria mkutano wa kikanda wa Kiarabu huko Jeddah ambapo mwanamfalme huyo atahudhuria .
Na ametetea uamuzi wake wa kufanya ziara hiyo akisema anatekeleza kwa awamu ombi la Israeli, na alianza safari yake kwa kusisitiza umuhimu wa Israeli "kuunganishwa kabisa" katika eneo hilo.
Sehemu kubwa ya hiyo ni kusaidia kuhalalisha uhusiano wa Israel na Saudi Arabia, kwa kutilia mkazo zaidi uhusiano wa karibu wa usalama wa Waarabu na Israel. Wazo ni kuratibu mifumo ya ulinzi wa anga ili kukabiliana na tishio la makombora kutoka Iran na washirika wake.
Mpango huo umeshika kasi kutokana na kukwama kwa juhudi za Marekani za kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran, mpango wa nyuklia unaoendelea kwa kasi wa Iran, na ongezeko la mashambulizi ya kikanda ya makombora kutoka kwa washirika wa Iran wa Houthi.
"Mpangilio mzima umejikita, kwa hakika, kutoka kwa mtazamo wa Israel, lakini pia kutoka kwa mtazamo wa Ghuba ya Kiarabu, juu ya uadui dhidi ya Iran," alisema.
Walakini, hakuna tangazo la mafanikio linalotarajiwa. Saudi Arabia ina ushirikiano wa siri na Israel, lakini inajizuia kupiga hatua zaidi bila harakati za kusuluhisha mzozo wa Palestina.
Baadhi ya hatua ndogo bado zinatarajiwa, kama vile upanuzi wa safari za ndege za Israel katika anga ya Saudia, safari za ndege za moja kwa moja kwa mahujaji Waislamu kwenda Makka kutoka Israel na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, na uhamisho wa visiwa viwili vya Bahari Nyekundu kutoka Misri hadi Saudi Arabia kwa dhamana njia inayotumiwa na meli kwa upande wa Isreal.
Je doa la kisiasa linalomkabili?
Ingawa huko Marekani, macho yote yatakuwa kwenye taswira ya mazungumzo ya Bw Biden na mwana mfalme wa Saudia. Rais amewashtua wengi katika jumuiya ya haki za binadamu, lakini uamuzi wake unaweza pia kumgharimu mtaji wa kisiasa ndani ya chama chake cha Democratic.
Wote wanahoji kuwa njia pekee ya yeye kugeuza safari kuwa ya "ushindi" ni kuibua kwa kiasi kikubwa masuala ya haki za binadamu. Wanamhimiza kushinikiza kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa na kuondolewa kwa marufuku ya kusafiri na vikwazo vingine kwa wanaharakati.
Pia wanamtaka arejelee hadharani madai kwamba wauaji wa Khashoggi wawajibishwe.
Na katika barua ya pamoja wenyeviti wa kamati sita za Bunge walimtaka rais kuendelea kusimamisha uungaji mkono wa kiuchokozi kwa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unaopigana nchini Yemen. Kuhusu vita hivyo, ufalme huo umedhibiti msimamo wake, na kukubali mapatano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa mwaka huu na kuongeza mazungumzo na waasi wa Houthi wa Yemen. Bw Biden amesifu hatua hizi na anasema atalenga kuendeleza juhudi za kuleta amani.
Je Wasaudia wanataka nini?
Kwa hakika, MBS, ambaye analaumu mauaji ya Khashoggi kufanywa na baadhi ya maafisa wake wa usalama, amewasilisha maombi kadhaa nchini Marekani akitaka kutuzwa kupitia kurejesha uhusiano, kuanzia na makubaliano ya usalama wa pande mbili.
Wasaudi pia wanataka ufafanuzi juu ya nia ya Bw Biden katika ziara hiyo, alisema Jonathan Panikoff, afisa wa zamani wa ujasusi wa kitaifa sasa na Baraza la Atlantiki.
"Haikuwa kama rais aliingia madarakani na kubadilisha uhusiano na Saudi Arabia. Umekuwa tu katika hali isiojulikana kwa muda wa miezi 18 iliyopita na hakuna mtu aliyejua mawasiliano hayo yanaelekea wapi ," alisema.