Bunge la Congress Marekani  latambua ndoa ya jinsia moja ili kuilinda dhidi ya mahakama

g

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Muswada wa Heshima ya Ndoa unatoa haki kwa watu wa jinsia moja na watu wa jamii tofauti kuoana kwa ngazi ya shirikisho (taifa)
Iliyochapishwa

Baada ya  Bunge la seneti, bunge la Congress pia limepitsha kwa kura sheria ya kihistoria inayotambua ndoa ya watu wa jinsia moja katika ngazi ya  shirikisho. Sasa waraka wa sheria hiyo utapelekwa kwa rais Joe Biden, ambaye tayari amekwishaelezea wazi kuwa anaiunga mkono.  

Sheria hiyo iliandikwa na Wademocrat ili kuzuia uwezekano wa kubadilishwa kwa haki za ndoa ya jinsia moja na majaji Warepublican wa mahakama ya juu zaidi na walivyofanya  wakati walioondoa haki za utoaji mimba wakati wa msimu wa kiangazi.

 Kutokana na ukweli kwamba sheria hiyo ya shirikisho ilipitishwa na wabunge warepublican na Wademocrat, ni dhihirisho kuhusu ni jinsi gani ndoa ya jinsia moja inavyokubalika katika jamii ya Wamarekani kwa sasa ililinganishwa na mwaka 1996, wakati sheria ya ndoa iliyobainisha kuwa ndoa ni kati ya mwanaume na mwanamke.   

 Sheria mpya  "Juu ya heshima ya ndoa" ilipigiwa na wabunge wa congress 258 , wakiwemo Wademocrat na Warepublican 39.  Warepublican 169 walipiga kura ya kuikataa.

 Sheria ya ‘Heshima ya ndoa’  ilikuwa ni moja ya sheria zilizoandaliwa na Wademocrat  ambazo zilitakiwa kushughulikiwa kwa dhrarura katika Congress ,kabla mamlaka hayajahamia kwa Warepublican.

 Warepublican bado wameendelea kuwa wengi  katika Bunge la Wawakilishi, lakini Republican walishinda kwa ushindi mdogo katika uchaguzi wa nusu muhula , na bunge hilo litakutana  mwezi wa Januari.

Hatahivyo majaji wa mahakama wamebadilika tangu wakati huo . Majaji sita kati ya tisa wa kudumu wa Mahakama ya juu zaidi ya Marekani wamekuwa wakichaguliwa na Marais Warepublican , na walau watano kati yao wana sifa ya kuwa na ushawishi ndani ya chama cha Republican.

Wakati wa msimu wa kiangazi, Waconservative walio wengi bungeni  katika Mahakama ya juu zaidi walieleza bayana kwamba, mahakama hiyo iko tayari hiyo  kuangalia upya kesi iliyopita kwa kubadili uamuzi wa kesi   Roe v. Wade kwa kuzingatia haki za kikatiba za utoaji mimba (ambazo kwa sasa zinatekelezwa tofauti kulingana na maamuzi ya kila jimbo, baadhi ya majimbo yanaruhusu utoaji mimba mengine hayaruhusu).

Hili liliibua hofu kwamba kugeuzwa kwa hukumu kungeathiri ndoa ya jinsia moja, hususan kwa sababu mmoja wa majaji Mconservative Clarence Thomas alidokeza kuwa kuhusu hili katika maoni yake.   

Haki ya ndoa ya jinsia moja nchini Marekani iko vipi? 

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mahakama ya juu ya Marekani ilianzisha sheria inayolinda ndoa ya watu wa jinsia moja katika uamuzi yake wa kihistoria wa mwaka 2015 katika uamuazi wa kesi ya Obergefell v Hodges.

Uamuzi huo uliondoa marufuku zilizopo za jimbo dhidi ya ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, na kuwapa wenzi wa jinsia moja haki ya kuoana kote  nchini Marekani na kuwapatia haki za kisheria  na maslahi ya kimataifa ambayo  watu walioona kama mume na mke wanayapata nchini Marekani.

Lakini Mahakama ya juu zaidi ya sasa ina msimamo  mkali zaidi, na haki kuhusu ndoa zimekuwa hofu yake  ya kwanza tangu ilipoondoa haki ya kikatiba ya utoaji mimba katika kesi ya   Dobbs v Jackson , kesi iliyohusisha   Shirika la wanawake la afya mepema mwaka huu.

 Katika uamuzi wake, Jaji, Clarence Thomas, pia alisema kuwa maswala hayo yalichangia  msingi wa maamuzi muhimu – ikiwa ni pamoja na  haki za za ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, na dawa za kuzuia mimba – yanaweza kupingwa. 

Jim Obergefell, ambaye alikuwa mlalamikaji mkuu katika kesi hiyo ya Mahakam ya juu mwaka  2015  aliiambia BBC kwamba  "hajaridhishwa kabisa" na Sheria ya Heshima ya Ndoa.

Uamuzi huo uliondoa marufuku zilizopo za jimbo dhidi ya ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, na kuwapa wenzi wa jinsia moja haki ya kuoana kote  nchini Marekani na kuwapatia haki za kisheria  na maslahi ya kimataifa ambayo  watu walioona kama mume na mke wanayapata nchini Marekani.

Jim Obergefell, ambaye alikuwa mlalamikaji mkuu katika kesi hiyo ya Mahakam ya juu mwaka 2015 aliiambia BBC kwamba "hajaridhishwa kabisa" na Sheria ya Heshima ya Ndoa.

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Sheria inayolinda ndoa ya watu wa jinsia moja katika uamuzi wake wa kihistoria wa mwaka 2015, lakini majaji wa sasa wamebadilika  

Kutokana na wasi wasi wa kubatilishwa kwa sheria ya ndoa ya jinsia moja, Wademocrat katika Baraza la Congress waliandaa muswada unaotoa hakikisho ya haki ya ndoa ya jinsia moja kwa kiwango cha kitaifa.   

Mwishoni mwa Novemba, sheria hii iliidhinishwa na Seneti, ambapo kwa mara ya kwanza Wademocrat 50 na Warepublican 50  waliketi. Kati yao watu 61  waliupiga kura kuunga mkono muswada: Wademocrat 49  (Mdemocrat mmoja hakuwepo) na Warepublican 12. Wabunge 36 (wote Warepublican) waliupinga.

 Rais Joe Biden amekwishaashiria kwamba, iwapo utaidhinishwa na Bunge la wawakilishi , atausaini kuwa sheria.   

 "Marekani inakaribia kuthibitisha tena ukweli wa kimsingi kwamba : mapenzi ni mapenzi na wamarekani wanapaswa kuwa na haki ya kumuoa mtu yeyote wanayempenda,"rais alisema katika taarifa yake. "Kwa mamilioni ya Wamarekani, sheria hii inatoa hakikisho  la haki na ulinzi kwa watu wa jamii za wapenzi wa jinsia moja LGBTQI+ na wenzi wa jamii tofauti na watoto wao ".

Je sheria ya kulinda ‘Heshima ya Ndoa’ inasemaje?

Sheria mpya ilibadilisha rasmi  kinga ya sheria ya ndoa, ya mwaka 1996 ambayo inaelezea ndoa baina ya mume na mke  pekee.  Mahakamu ya juu zaidi iliamuru kuwa sheria hiyo ni kinyume cha katiba mwaka 2013.

Muswada wa Seneti pia unayataka majimbo kutambua ndoa za jinsia moja ambazo zimefanyika katika majimbo mengine, na kuhakikisha maslahi ya shirikisho yanawafikia wenzi waliooana kama wapenzi wa jinsia moja.

Kura hiyo imepigwa baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo ua pande mbili za kisiasa, na kura hii ya Seneti ilifanyika baada ya uchaguzi wa nusu muhula.

Toleo la wali la muswada huo liliidhinishwa na Bunge la Wawakilishi mapema mwaka hu una baadhi ya Warepublicans mwaka huu.  

Huku baadhi ya Warepublicans wakielekea  kufanikiwa kupitisha miswada katika Bunge la seneti na Bunge la wawakilishi, wengi katika chama hicho bado hawaiungi mkono sheria hiyo.     .

Mwezi Julai 2022  kura ya maoni ya Gallup ilibaini kuwa 71% ya Wamarekani waliunga mkono ndoa ya jinsia moja.