Kundi la Wagner : Vyombo vya habari vya serikali vya Urusi vyampaka tope Prigozhin

Chanzo cha picha, Izvestia
Televisheni inayodhibitiwa na serikali ya Urusi imeanza kampeni inayoonekana kumkashifu mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin kufuatia kushindwa kwake kuasi mwishoni mwa mwezi Juni.
Idhaa kuu zilionyesha kile walichosema ni picha zilizopigwa wakati wa upekuzi katika nyumba yake ya kifahari nje ya St Petersburg, vikihoji kwamba utajiri wake ulimpatia sura mbaya .
Pia walikumbuka uhalifu wake wa zamani na kupendekeza kwamba alikuwa akiongozwa na uchoyo, lakini walishindwa kutaja ukosoaji wa mara kwa mara wa Prigozhin wa jeshi la Urusi na jinsi linavyoendesha vita huko Ukraine.
Hii ni mara ya kwanza kwamba vyombo vya Habari vya serikali vimeripoti kuhusu Prigozhin , kibinafsi na Habari zilizojaa maelezo mabaya kuhusu wasifu wake.
Hadi hivi majuzi, Runinga ya Urusi ingeonyesha picha nzuri ya kundi la mamluki la Wagner, ambalo limepigana pamoja na jeshi la Urusi wakati wa uvamizi wake nchini Ukraine.
Picha zinazosemekana kuwa kutoka ndani ya nyumba ya Prigozhin zilionekana kwenye mtandao unaoendeshwa na serikali Rossiya 1 tarehe 5 Julai.

Chanzo cha picha, izvestia
"Wacha tuangazie jinsi mpiganiaji huyu wa ukweli aliishi, mtu ambaye ana hatia mbili za uhalifu na ambaye aliendelea kudai kuwa kila mtu alikuwa mwizi," alisema mchambuzi kwenye kipindi cha mazungumzo cha 60 Minutes.
"Hebu tuangalie ikulu iliyojengwa kwa ajili ya mwanaharakati huyu dhidi ya rushwa na uhalifu," Eduard Petrov alisema kwa kejeli.
Picha hizo zilionyesha rundo la pesa taslimu, silaha mbalimbali, mambo ya ndani ya nyumba hiyo yenye kupendeza na bustani kubwa - kamili ikiwa na helikopta iliyoegeshwa, aina mbalimbali za wigi na pasi za kusafiria ambazo dhahiri zimetolewa kwa Prigozhin kwa majina tofauti.

Chanzo cha picha, Izvestia
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Baadaye, picha kama hizo zilionyeshwa kama sehemu ya taarifa kuu ya habari ya jioni ya kituo mojawapo maarufu zaidi nchini Urusi. Pia iliangazia dhahabu na "pakiti zinazotiliwa shaka za poda nyeupe", ambayo Rossiya 1 alipendekeza inaweza kuwa dawa ya kulevya.
Pia iliangazia kwa muda mrefu kuhusu uhalifu wa zamani wa Prigozhin.
Alipatikana na hatia kwa mara yake ya kwanza mwaka 1979, akiwa na umri wa miaka 18 tu, na akapata kifungo cha miaka miwili na nusu kwa wizi. Miaka miwili baadaye, alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela kwa wizi tisa kati yake aliitumikia jela..
"Wanasema kwamba ni uzoefu na umaarufu aliyopokea kutoka kwa wakuu wa uhalifu akiwa jela ambao ulimsaidia kutoka kuwa muuzaji hot dog hadi kuwa mpishi mkuu," mwandishi wa Rossiya 1 alicheka, akirejelea jukumu la zamani la Prigozhin akiwa mpishi wa Kremlin.
Jukumu hili pia lilimpatia jina la utani "mpishi wa Kremlin".
Moja ya picha zilizoonyeshwa na TV ya serikali ya Urusi ilionyesha sledgehammer yenye maandishi "Tumia wakat iwa majadiliano muhimu ". Hii inaonekana kuwa inarejelea mauaji ya kikatili kwa kutumia nyundo dhidi ya mwanamume ambaye Wagner ilimtuhumu kwa usaliti mnamo Novemba 2022.

Chanzo cha picha, Ivestia
Jioni hiyo hiyo, Channel One ya runinga ya serikali ilipendekeza kwamba Yevgeny Prigozhin alihusishwa na ujasusi wa Magharibi, ambao sasa " ulikuwa na aibu sana" kukubali kuhusika katika uasi .
NTV, mojawapo ya vituo vitatu vya runinga vilivyotazamwa zaidi nchini Urusi, ilisema kwamba alikuwa akiongozwa na pupa na uhalifu wa zamani.
"Kilichotokea kina mizizi dhahiri katika utu wake, masilahi ya biashara na maisha yake ya zamani yaliyojaa uhalifu," ilisema. Kuhusu utajiri unaodaiwa wa Prigozhin, "kupigania ukweli kunagharimu pesa nyingi", NTV ilisema.
Hadi miezi kadhaa baada ya kuanza kwa vita kamili vya Urusi dhidi ya Ukraine, maafisa, vyombo vya habari na vyombo vya habari vya Prigozhin vilikanusha kuwepo kwa kundi la Wagner .
Kwa kipindi cha muda baadaye, TV ya serikali ilisherehekea kuhusika kwa Wagner katika "operesheni maalum ya kijeshi" nchini Ukraine.
Kutajwa kwa Wagner kulikuwa kumepungua katika vyombo vya habari vya serikali wakati Prigozhin alipoanza "maandamano ya haki", akiapa kuwaadhibu makamanda wa kijeshi wa Urusi ambao aliwashutumu kwa uzembe.

Chanzo cha picha, Izvestia
Prigozhin mwenyewe, ambaye amenyamaza kabisa kwenye mitandao ya kijamii baada ya uasi, hajatoa maoni yake juu ya picha hizo.
Lakini kituo kimoja kilichohusishwa na Wagner kilisema kuwa haikuwa kawaida kwa mfanyabiashara tajiri kama Prigozhin kumiliki nyumba ya bei ghali: "Ni nini cha kuvutia hapa basi?" kiliuliza.
Baada ya hapo awali kukanusha kuwa kulikuwa na uhusiano wowote kati ya Wagner na serikali, Rais Vladimir Putin - akizungumza muda mfupi baada ya maasi ya Prigozhin kushindwa - alisema serikali ilifadhili kikamilifu kampuni ya kijeshi, ikitumia sawa na $1bn (£787m) kuinunua mnamo Mei 2022 hadi Mei 2023 pekee.












