Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 09.06.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle wamewasilisha dau la pauni milioni 16 kwa Burnley kumnunua mlinda mlango wa Uingereza James Trafford, 21, lakini Clarets wanataka pauni milioni 20. (Mail)
Manchester United wanatarajia kukamilisha dili la kumnunua beki wa Everton, Jarrad Branthwaite kabla ya Juni 30 baada ya kiongo huyi kuachwa nje ya kikosi cha England cha Euro 2024 (Liverpool Echo)
The Red Devils wanajiandaa kuwasilisha ofa ya pili kwa kiungo wa Benfica Joao Neves, 19, baada ya ofa ya awali ya £51m kukataliwa. (A Bola - kwa Kireno)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wanataka kumbakisha mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez na hawatapokea ofa zozote za mkopo kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Fabrizio Romano)
Atletico Madrid wamekuwa wakihusishwa na Alvarez lakini rais wa klabu yao Enrique Cerezo anasema haamini kuwa mshambuliaji huyo ataondoka Etihad Stadium. (Standard)
Leicester City wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter kuhusu nafasi yao ya ukocha. (Telegraph - usajili unahitajika)
Bayern Munich wamefufua tena mazungunzo na Fulham kuhusu kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28. (Mchezo)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 27, anatazamiwa kuondoka Tottenham kama mchezaji huru msimu huu wa joto. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Fulham Marco Silva anaweza kulengwa na Nottingham Forest iwapo meneja wao Nuno Espirito Santo ataondoka kwenye Uwanja wa City. (Mail)
Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal anasema kuwa kocha mwenzake wa Uholanzi Erik ten Hag hafai kufutwa kazi na klabu hiyo ya Ligi ya Premia. (Metro)
Kiungo wa kati wa Everton Mbelgiji Amadou Onana, 22, anahusishwa na kuhamia Arsenal na anasema angependa kuchezea "klabu ya kimataifa ya dunia". (Standard)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












