Kifaa kilichobuniwa kienyeji kinavyowasaidia walio na matatizo ya uti wa mgongo

Kifaa kilichobuniwa kienyeji kinavyowasaidia walio na matatizo ya uti wa mgongo
Iliyochapishwa

Charles Muigai ni mtaalam wa viungo katika hosptiali ya rufaa ya Kilifi iliyopo mwambao wa pwani nchini Kenya.

Ameweza kuwaletea afueni familia nyingi katika eneo hilo kwa uvumbuzi wake wa kifaa kiitwacho ‘Cervical Traction Device’ ambacho husaidia wagonjwa walio na shida ya uti wa mgongo kutokana na sababu kama ajali au kuathirika na magonjwa kama kiharusi au shida za neva.

Uvumbuzi huu umepunguza gharama za kwenda hospitali kila siku kwani kinaundwa nyumbani na mgonjwa anaweza kukitumia akiwa ametulia kwake nyumbani, na bei yake ni nafuu zaidi kuliko kununua kifaa hicho dukani.