Tetesi za soka Ulaya Jumatano 02.10.2024

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1

Liverpool wako tayari kuchuana na Manchester United kwa ajili ya kumnunua mlinzi wa kati wa Everton Jarrad Branthwaite na wanaweza kumnunua Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 22 mwezi Januari. (Mail)

Lakini Sean Dyche atapewa fedha za kuboresha kikosi cha Everton mwezi Januari mara tu Kundi la Friedkin litakapomaliza kutwaa klabu hiyo na hakuna wachezaji wakubwa watakaouzwa. (Football Insider)

Kocha wa zamani wa Uingereza Gareth Southgate ndiye mteule bora wa Manchester United kuchukua nafasi ya Erik ten Hag kama meneja. (ipaper)

Klabu hiyo ya Old Trafford pia ina nia ya kuzungumza na meneja wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri iwapo watamfuta kazi Mholanzi Ten Hag. (Football Insider)

Lakini Ten Hag anaendelea kuungwa mkono na wachezaji wakuu katika klabu ya Manchester United licha ya timu hiyo kuanza vibaya msimu huu. (Telegraph)

Meneja wa zamani wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuzilia mbali uvumi kuwa atachukua nafasi ya meneja wa Ujerumani. (Mail)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Hispania Andres Iniesta, 40, anatarajiwa kutangaza kustaafu soka siku zijazo. (Goal)

Kiungo wa kati wa Crystal Palace na England Adam Wharton, 20, na kiungo wa kati wa Atalanta wa Brazil Ederson mwenye umri wa miaka 25 wako juu kwenye orodha ya Manchester City iwapo watajaribu kuchukua nafasi ya Mhispania Rodri, 28, aliyejeruhiwa mwezi Januari. (Caught Offside)

Winga wa Uingereza Anthony Gordon, 23, anatazamiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Newcastle hadi 2030. (Fabrizio Romano).