Kwa nini ninapeleka majivu ya mwanangu mwezini

A group photo showing the seven members of the Anand family, including Liam

Chanzo cha picha, Anand Family

Maelezo ya picha, Liam Anand, kulia, akiwa na Nadine, baba yake Sanjiv na kaka na dada zake wanne.
    • Author, Peter Ball
    • Nafasi, BBC World Service
  • Iliyochapishwa

Katika siku ya mwaka mpya, roketi italipuka kutoka Cape Canaveral kwa lengo la kuwapeleka watu zaidi ya 70, akiwemo Liam Anand mwenye umri wa miaka 16 kwa ajili ya mapumziko.

Mama yake Nadine aliiambia BBC "nitakapoondoka kwenda nje na kutazama juu na kujua kwamba sehemu ya mwili wake iko kwenye Mwezi... litakuwa ni jambo la muujiza , la kihisia na la kutuliza."[moyo]

Wakati Liam, ambaye ni mzaliwa wa Dieppe nchini Canada, alipofariki katika ajali ya pikipiki mwaka 2018, familia yake ilitaka kufanya mazishi ambayo si ya kawaida kwa ajili yake.

"Tulijua kuwa yatakuwa ni kitu ambacho kilimuwakilisha," Nadine alisema.

Liam, alikuwa ni kijana mwenye nguvu ambaye familia yake inasema kila wakati alionekana mtu mwenye harakati , alikuwa na ndoto ya kushiriki katika safari ya kuelekea kwenye sayari ya Marsatakapokuwa mtu mzima, au biashara inayohusiana na vimondo (asteroids).

Alikumbuka jinsi alivyokuwa akipenda masuala yanayohusiana na anga za mbali, na alianza kurambaza mtandaoni na kwa bahati aliweza kuona huduma mpya ya safari za anga kwa ajili ya kumbukumbu za watu waliofariki.

Sasa sehemu ya majivu ya Liam itakuwa ndani ya chombo cha Peregrine - kinachokwenda mwezini wakati kitakapotua huko Januari.

Nadine anasema akupanga mwanawe awe sehemu ya safari kumesaidia mchakato wa familia yake kpona kihisia, na mahali hapa pa kipekee pa kupumzika kutawapa njia ya kudumu ya kumkumbuka.

"Alitaka kuingia katika anga za juu. Kwa njia hii familia yake, marafiki zake, yeyote anayemkosa au anayetaka kumsherehekea, anaweza tu kuangalia juu ya Mwezi na kusema hi (Salamu).

"Ni kama vile tunamheshimu."

Ndoto ya utotoni

Charles Chafer smiling stood in front of a partially assembled rocket

Chanzo cha picha, Celestis

Maelezo ya picha, Mkurugenzi Mtendaji wa Celestis Charles Chafer akiwa amesimama mbele ya roketi ya Vulcan Centaur ambayo itazindua lander ya Peregrine kwenye Mwezi
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa Charles Chafer Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayotoa huduma, upande wa binadamu wa biashara ni muhimu kama sayansi ya roketi.

"Nilipoanzisha kampuni, nilidhani tutakuwa kampuni ya anga," alisema. "Lakini nilijifunza mapema sana kwamba sisi ni kampuni ya ushauri wa huzuni."

Baada ya kutazama ujumbe wa Mwezini wa Apollo alipokuwa mwanafunzi wa shule, alianza kazi katika sekta ya anga za juu, ikiwa ni pamoja na kusaidia kufyatua roketi ya kwanza ya kibiashara inayofadhiliwa na watu binafsi.

Mwaka 1995, alianzisha kampuni ya Celestis ambayo hapo awali ilianza kupelekea sampuli za majivu vinasaba au DNA za watu katika mwezi. Katika ujumbe wa mwezi kampuni hiyo imenunua nafasi kwenye chombo cha Peregrine,ambacho lengo lake kuu ni kufanya majaribio ya kisayansi kwenye Mwezi.

Bwana Chafer anasema, huduma hiyo mpya, inagharimu sawa na "kiasi cha mazishi ya kawaida ya Marekani" kwa karibu dola 13,000.

"Gharama za roketi za hiyo ni ndogo ni ya kushangaza ," aliongeza. "Ni biashara yenye mwelekeo wa huduma."

Upendo wake wa sayansi ulimleta katika sekta hiyo, lakini sasa anafurahia kusaidia familia kukabiliana na majonzi, na anaona ni jambo la kufurahisha sana kwamba huduma hiyo inaweza kuleta furaha kwa watu ambao ni wagonjwa.

Anasema kila mara anaguswa na watu wanaosema: "Baba hakutabasamu sana katika siku zake za mwisho, lakini tulipomwambia kile tutakachomfanyia, alitabasamu maisha yake yote."

"Hakuna kazi nyingi ambapo unaweza kupata hisia hizo."

Miaka 100,000

Alan Clive sat a desk using braille terminal

Chanzo cha picha, Clive Family

Maelezo ya picha, Alan Clive, ambaye alipoteza uwezo wake wa kuona katika miaka ya 20, alikuwa shabiki wa hadithi za sayansi ya muda mrefu

Alan Clive, ambaye alipoteza uwezo wake wa kuona akiwa na umri wa miaka 20, alikuwa shabiki wa hadithi za sayansi ya muda mrefu.

Michael Clive anakumbuka wakati alipomwambia baba yake, Alan, ambaye alikuwa mgonjwa sana na saratani, kwamba alipanga kutuma majivu ya mwili wake kwenye Mwezi.

"Licha ya dawa zote, tuliweza kumfikia," alisema.

"Nilipomwambia baba yangu kwamba tutatuma majivu yake kwenye Mwezi, alitabasamu na kusema: 'Naam, hilo ni jambo zuri.'"

Kusoma hadithi za sayansi kama mvulana katika miaka ya 1950 kulimpa Alan upendo wa muda mrefu wa hadithi za sayansi na Michael anakumbuka familia ikitazama Star Trek na yeye na dada yake wakielezea matukio kwenye skrini kwa Alan, ambaye alikuwa hana uwezo wa kuona.

Baba yake pia alihusika katika vikundi vya elimu ya anga, ikiwa ni pamoja na Planetary Society na Kituo cha Challenger, na kupitia Clive na Alan walikutana na Eugene Shoemaker.

Kwa sasa, mwanaanga maarufu na mwanajiolojia, ambaye alikufa mwaka 1997, ndiye mtu pekee ambaye majivu ya mwili wake yalipelekwa kwenye Mwezi.

Baadhi ya mabaki yake yalikuwa yakifanyiwa uchunguzi na kituo cha safari za anga za mbali cha Nasa.

Michael anafurahi kwamba majivu ya baba yake yanapaswa kufika kmahali tulivu zaidi kwa kutua kwenye uso wa mwezi, usio na hali ya hewa inamaanisha wanaweza kulala huko bila kusumbuliwa.

A graphic showing the Peregrine lander on the Moon with Earth in the background

Chanzo cha picha, Astrobotic

Maelezo ya picha, Kampuni ya kumbukumbu ya Celestis imenunua nafasi kwenye ujumbe wa Peregrine Lander mwezi

"Katika miaka 1,000, majivu haya yataendelea kuwepo huko , na katika miaka 10,000 labda badoyatakuwa huko, na labda hata katika miaka 100,000.

"Hakunavitu vingi ambavyo vinaweza kudumu muda kama huo duniani."

Hata ana matumaini kwamba wakati watoto wake wadogo wamekua, siku moja wanaweza kusafiri kwenda mwezini kumtembelea babu yao, ikiwa teknolojia mpya itafanya safari ya anga kuwa ya kawaida zaidi.

Katika siku za usoni, Nadine anatarajia kutazama uzinduzi wa chombo cha Peregrine na mumewe Sanjiv na ndugu zake wanne wa Liam.

"Kama Liam angeweza kuona kile tunachofanya kwa ajili yake, angekuwa na furaha," alisema. "Angekuwa na furaha kwa sababu anapenda umakini kidogo, lakini sio sana."

"Safari hii ya majibu itakuwa ni sehemu ya mchakato wetu wa uponyaji na huzuni yetu," aliongeza.

"Itakuwa ni wakati wa furaha. Najua kutakuwa na machozi kwa uhakika, lakini yatakuwa machozi ya furaha."

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi