Wanafunzi waliokwama walazimika kumzika rafiki yao Sudan

Maelezo ya video, Sudan: Wanafunzi waliokwa walilazimika kumzika rafiki yao Sudan
Wanafunzi waliokwama walazimika kumzika rafiki yao Sudan
g
Iliyochapishwa

Wanafunzi na wafanyakazi katika Chuo Kikuu cha Khartoum wanasema wamekwama katika makabiliano ya silaha kwa siku nne, bila chakula na maji.

Kuna takriban wanafunzi 88 na wafanyakazi wa chuo kikuu waliokwama katikati ya mji mkuu wa Khartoum huku mapigano yakiendelea kuchacha baina ya makundi hasimu ya uongozi wa kijeshi wa Sudan.

Mwanafunzi mmoja amethibitishwa kufariki katika makabiliano hayo. Ilibidi mwili wake uzikwe nyuma ya jengo la kitivo cha uhandisi cha Cho kikuu cha Khartoum.

Wanafunzi wanayataka mashirika ya kimataifa yawapatie msaada wa dharura na uokoaji.