Yaliomo katika video zilizobebwa na wapiganaji wa Hamas wakati wa uvamizi Israel

.

Chanzo cha picha, IDF HANDOUT

Maelezo ya picha, Jeshi la Israeli lilikagua picha zilizochukuliwa kutoka kwa kamera zilizovaliwa mwilini na Hamas, CCTV, kamera za mbele ya gari na simu za rununu.
Iliyochapishwa

Makala haya yana maelezo ya vurugu ambayo baadhi ya wasomaji wanaweza kupata yanahuzunisha.

Jeshi la Israel lilifanya uchunguzi kutoka kwa waandishi wa habari siku ya Jumatatu kuhusu picha zilizopatikana kutoka kwa kamera za Hamas, katika juhudi za kukumbusha ulimwengu juu ya ukatili wa shambulio la Israel wiki mbili zilizopita.

Picha za kamera zilizokatwa pamoja na klipu za CCTV, na kamera za simu za mkononi za wapiganaji wa kundi la Hamas na wahasiriwa, zilionyesha kwa undani kabisa hofu kubwa iliyokuwa kwenye tamasha la muziki na vitongoji vya familia kusini mwa Israeli.

Jeshi la Israel pia lilitoa hati ambazo walisema zilipatikana kutoka kwa wanachama waliokufa wa Hamas, zenye mipango ya kina ya operesheni na maagizo ya kushambulia vitongoji na kuchukua mateka.

Picha za dakika 43 zilizoonyeshwa katika kambi ya kijeshi karibu na Tel Aviv Jumatatu zilichukulkiwa kutoka kwa mamia ya picha zilizokusanywa tangu shambulio hilo, jeshi la Israeli lilisema.

Video hizo zilikuwa na sehemu za watu wenye silaha wa Hamas wakishangilia kwa furaha wakati wakiwapiga risasi raia barabarani, na baadaye kuvizia vijiji vya kibbutzim na kuwaua wazazi na watoto majumbani mwao.

Msururu mmoja wa kiwewe, uliochukuliwa kutoka kwa kamera za nyumbani ndani ya kibbutz, ulionyesha baba akiwakimbiza wavulana wake wawili kwenye makazi ya juu ya ardhi, sekunde chache kabla ya washambuliaji wa Hamas kurusha guruneti, na kumuua baba na kuwajeruhi wavulana.

Huku wavulana hao wawili, wakiwa na damu na mshtuko, walijikongoja na kurudi nyumbani kwao wakipiga kelele, mtu mwenye bunduki wa Hamas aliingia kwa utulivu na kuchungulia kwenye jokovu iliyokuwa mbele yao, akatulia kuchukua kinywaji kabla ya kutoka tena.

Mmoja wa wavulana alimlilia kaka yake: "Baba amekufa, huu sio mchezo," na akarudia "Kwa nini niko hai"? Ndugu yake inaonekana alipofushwa na guruneti. Msemaji wa jeshi aliyekuwepo kwenye uchunguzi huo hakuweza kusema iwapo walinusurika.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zaidi ya Waisraeli 1,400 waliuawa wakati Hamas iliposhambulia jamii kusini mwa Israel, karibu na Ukanda wa Gaza.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Filamu hiyo pia ilikuwa na sauti iliyorekodiwa ya mmoja wa wapiganaji wa Hamas akiwapigia simu wazazi wake huko Gaza kutoka kwa simu ya mwathiriwa akijigamba kwamba "amewaua Wayahudi 10 kwa mikono yake".

ONYO: `Taarifa ifuatayo ina maelezo ya wazi ya vurugu

"Tafadhali fungua WhatsApp uone ni wangapi waliokufa," aliwasihi wazazi wake mara kwa mara, akimaanisha picha au video aliyokuwa ametuma nyumbani ikionyesha shambulio hilo.

“Mwanao aliua Wayahudi wengi sana,” alisema. "Mama, mwanao ni shujaa."

Msururu mwingine ulionyesha mshambulizi mmoja wa Hamas akipiga risasi maiti za raia waliokuwa ndani ya kibbutz kwa njia ya kusherehekea, na jaribio la kumkata kichwa mtu ambaye alionekana bado yu hai kwa kutumia jembe la bustani.

Picha hizo, baadhi zilichukuliwa kutoka kwa simu za waathiriwa, pia zilionyesha hofu kuu ya wale waliojificha katika vyumba salama na malazi huku milio ya risasi na milipuko ikikaribia.

Uamuzi wa kuchuja picha za waandishi wa habari ulionyesha kuchanganyikiwa dhahiri miongoni mwa vitengo vya jeshi la Israeli kwamba utangazaji wa habari wa shambulio la kikatili la Hamas mnamo Oktoba 7 ulitoa nafasi ya kuangazia mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Gaza na mgogoro wa kibinadamu uliosababishwa na amri ya Israel kwa watu wa Gaza kuhamia kusini.

Akizungumza na vyombo vya habari vya kimataifa vilivyokusanyika baada ya mchujo huo, Meja Jenerali Michael Edelstein, kamanda wa zamani wa kitengo cha IDF Gaza, alisema "ameshtushwa" na utangazaji huo.

"Tunaona kwamba baadhi ya njia zinajaribu kulinganisha kile ambacho Israel inafanya na kile magaidi hao wabaya wanafanya," Jenerali Edelstein alisema.

"Siwezi kuelewa mtu yeyote anayelinganisha," alisema. "Na baada ya yale tuliyokushirikisha, unapaswa kujua."

Zaidi ya Waisraeli 1,400 wameuawa tangu shambulio la Hamas tarehe 7 Oktoba, kulingana na mamlaka ya Israel - idadi kubwa katika shambulio la awali. Zaidi ya 220 wanaaminika kuchukuliwa mateka ndani ya Gaza.

Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza inasema zaidi ya Wapalestina 5,000 wameuawa tangu mashambulizi ya anga ya Israel yaanze, na kwa mujibu wa wizara ya afya ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, Wapalestina 91 wameuawa tangu tarehe 7 Oktoba.

.

Chanzo cha picha, IDF Handout

Maelezo ya picha, Picha za Dashcam zilionyesha wakati watu wenye silaha wa Hamas walipofyatulia risasi gari la raia, na kupasua kioo cha mbele

Baada ya kuonyeshwa kwa video hizo siku ya Jumatatu, Jeshi la Israel pia lilitoa miongozo miwili ya maagizo iliyochukuliwa kutoka kwa wapiganaji wa Hamas waliouawa, ikiwa na mipango ya kina ya shambulio hilo na kuchukua mateka.

"Lazima wawapige risasi wahasiriwa wengi iwezekanavyo, wachukue mateka na kuwapeleka baadhi yao Ukanda wa Gaza kwa kutumia magari mbalimbali," ilisema sehemu moja ya mwongozo huo.

Katika waraka tofauti hasa kuhusu mateka, watendaji wa Hamas waliagizwa "kuwaua wenye matatizo na wale ambao ni tishio" na kuwakusanya wengine pamoja ili kuwatumia kama "ngao’’.

Jeshi la Israel bado linayumbayumba kutokana na shambulio la Oktoba 7, ambalo ni uvunjaji mbaya zaidi wa ulinzi wake kusini katika kipindi cha miaka 50.

Licha ya rasilimali kubwa kuwekwa katika kuharibu mahandaki ya Hamas na kupanua uzio wa usalama wa Israeli chini ya ardhi na nje hadi baharini, Hamas iliweza kuvamia na kuvunja uzio kwa kishindo.

Zaidi ya wanamgambo 1,000 walivuka na kuingia Israel katika uvamizi wa awali, Jenerali Edelstein alisema Jumatatu. Sehemu za kwanza za utayarishaji wa video hiyo zilionyesha makundi ya magari ya kubebea mizigo yakiwa yamejazwa na watu wenye silaha wa Hamas, yakiendeshwa kwa uhuru kwenye barabara kuu za Israel na kuwafyatulia risasi raia wapendavyo.

Nyaraka zilizopatikana kutoka kwa miili ya wanamgambo wa Hamas zilionyesha wazi kwamba Hamas "ilikuja na amri ya kuchinja na kuchoma raia", Jenerali Edelstein alisema.

"Waliamua tu kuchoma familia ndani ya nyumba zao. Na walichukua mateka wakiwa hai, walikuwa na lengo la kuwapeleka watoto Gaza," alisema.

"Amri zilikuwepo za kuua wangapi, na wangapi wachukuliwe kama mateka. Amri zilikuwepo za kubaka, yote yaliandikwa na kuamriwa."

Akizungumza kabla ya video hizo kuchujwa , msemaji wa jeshi la Israel Rear Admiral Daniel Hagari alisema kuwa wanajeshi walikuwa na mjadala wa iwapo picha hizo zioneshwe , lakini aliamua kufanya hivyo binafsi.

"Tunaelewa tayari kwamba tunahitaji kuunda kumbukumbu ya pamoja kwa siku zijazo," alisema. "Hatutaacha ulimwengu usahau."