Dhana potofu zinazouziwa wanaume wanaojaribu kuongeza idadi ya mbegu za kiume

.
Maelezo ya picha, Simon, mwenye umri wa miaka 28, hufuata utaratibu wa hatua mbalimbali ili kulinda uwezo wake wa kuzalisha.
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Simon huamka kila siku asubuhi na kuingia kwenye bafu ya mvuke au sauna. Anasema joto hilo humsaidia kutoa jasho na sumu mwilini ambayo baadaye humsaidia katika uzalishaji wa manii, ila anasema yeye hujikinga kutokana na joto kali.

Akizungumza na BBC, Simon anasema, "mimi huweka mfuko wa barafu kwenye korodani ila kudumisha idadi ya juu ya manii"

Ingawa matokeo yake hayajathibitishwa kisayansi, yeye ameendelea kutumia mtindo huu kuongeza uzalishaji wake wa manii.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Venezuela anayeishi mjini Miami, Florida nchini Marekani, huhakikisha anaota jua kila siku na kufanya mazoezi kila mara.

Yeye hunywa maji kila mara na kuvaa suruali yap amba ili kujiepusha na sumu mbalimbali.

Licha ya hayo yote, Simon hana mpango wa kupata watoto hivi karibuni na pia hana mpenzi, anajali tu afya yake na uwezo wake wa kuzalisha manii kwa wingi.

"Uwezo wa chini wa uazazi unaweza kuathiri seli zinazozalisha homoni, viwango vya testosterone, au homoni nyingine, na hilo ni jambo linalotia wasiwasi," alisema.

Hata hivyo, mfumo wa endocrine unaweza kuathiri idadi ya manii, lakini uwezo duni wa uzazi wenyewe hauvurugi moja kwa moja mfumo wa endocrine wala viwango vya homoni ya testosterone.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Simon ni miongoni mwa idadi kubwa ya wanaume wanaojali kiwango chao cha uzalishaji wa manii.

Kote duniani maudhui ya uwezo wa kuzaa imekua ikipata watazamaji wengi kwenye mitandao ya tiktok na Instagram.

Kwenye mtandao wa Reddit watu wanaotaka kujua sana kuhusu uwezo wa kuzalisha wa wanaume umeongezeka kuanzia mwezi Januari.

Watalaam wa afya ya kume wanasema kumekuwa na ongezeko kote duniani wa wanaume wanaotaka kujua afya yao ya manii na uwezo wao wa kuzalisha.

Watalaam wanasema hii huenda ni kutokana na tiba ya kuongeza testosterone na pia kujali kuhusu sumu zinazopatikana katika mazingira yetu ya kila siku inayoweza kuathiri uwezo wa kuzalisha.

Barsafoor Suks Minhas, mtaalamu wa uzazi mwenye kutoka Uingereza, anasema kuwa ongezeko hili la hamasa kuhusu afya ya uzazi wa wanaume una pande chanya na hasi.

"Kuongezeka kwa uelewa kuhusu tatizo la utasa wa wanaume ni jambo muhimu. Lakini je, tunachochea hofu hii bila sababu za msingi?"

Mtaalamu huyo aliongeza kuwa, kando na hilo, pia kumeibuka soko la mtandaoni na bidhaa zinazotumia wasiwasi uliopo kuhusu afya ya uzazi ya kiume kujinufaisha.

Kama ilivyo kwa watu wengi, Simon alikumbana na mada hii kwa mara ya kwanza kupitia mitandao ya kijamii. Hata hivyo, bado hajafanyiwa kipimo cha manii na hana sababu maalumu ya kuhofia afya yake.

"Ni jambo ambalo kwa ujumla hunitia hofu, ndiyo maana ningependa kuhifadhi uwezo wangu wa kupata watoto," alisema.

Waziri wa Afya wa Marekani, Robert F. Kennedy Jr pia hivi karibuni alizungumzia "matatizo ya uzazi," akisema kwamba mwaka 1970 idadi ya mbegu za kiume kwa wanaume ilikuwa "mara mbili ya ilivyo kwa wanaume wa leo."

Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba vijana wa leo wana idadi ndogo ya mbegu za kiume au manii kuliko wanaume wa miaka ya 1970.

Ingawa uchambuzi mpana wa tafiti zilizofanywa hapo awali zinaonyesha kuwa kumekuwa na upungufu mkubwa wa idadi ya mbegu za kiume duniani tangu miaka ya 1970, eneo hili bado halijafanyiwa utafiti wa kutosha.

BBC ilizungumza na wanaume saba kutoka sehemu mbalimbali duniani waliotumia mchanganyiko wa dawa za aina hii kama steroids ili kurejesha uwezo wao wa kupata watoto baada ya kupata matibabu ya Testosterone Replacement Therapy (TRT)

Kwa sababu kununua dawa kama vile steroids kupitia kwa mitandao ni kinyume cha sheria katika maeneo mengi, watu hao waliomba majina yao yasichapishwe.

Mmoja wa wanaume hao alisema;

"Ninaamini nitapata watoto wengi baada ya kutumia dozi kubwa za HMG na HCG."

Mtu mwingine alisema;

"Nina uhakika nitaweza kupata mtoto baada ya kutumia mchanganyiko huu wa dawa."

Awali Jamal,  alitumia steroids na testosterone kuongeza ukubwa wa misuli yake.
Maelezo ya picha, Awali Jamal, alitumia steroids na testosterone kuongeza ukubwa wa misuli yake.

Mwanaume mmoja, ambaye tumebadilisha jina lake na kumwita Jamal, alitumia dozi kubwa za testosterone na steroids kwa ajili ya kujenga misuli. Kutokana na matumizi hayo, uwezo wake wa kupata watoto ulipungua.

Aliacha kutumia dawa hizo mwishoni mwa mwaka jana, yeye na mwenzi wake walipoanza kufikiria kupata watoto.

Alitafuta ushauri kuhusu uzazi kupitia tovuti na video za YouTube ambako wanaume wengine waliokuwa wamepitia hali kama yake walielezea uzoefu wao.

Jamal anasema "Kwenye mtandao watu walikuwa wakisema, 'Unaweza kuitumia hivi, au unaweza kuitumia vile.'

Hata hivyo, mbinu hizo ziliposhindwa kutoa matokeo, aliamua kutafuta msaada wa kitaalamu na kumwona Profesa Jayasena.

Hadi wakati huo, hakuwa akijua hatari za kutumia dawa za kuongeza uwezo wa uzazi bila usimamizi wa daktari.

"Unapoanza kutumia steroids zinazoongeza homoni za kiume, tayari unakubali kwamba zinaweza kuathiri afya yako. Unakuwa umeamua kubeba hatari hiyo. Kwa hiyo, huwa hujali sana hata madhara ya dawa kama HCG."

Kwa kufuata ushauri wa Profesa Jayasena, Jamal aliacha kutumia dawa zote, zikiwemo dawa za kuongeza uwezo wa uzazi.

Baada ya miezi sita, kiwango cha asili cha testosterone kilianza kuongezeka. Hata hivyo, homoni inayochochea uzalishaji wa manii ilikuwa bado ipo katika kiwango cha chini ila kuna matumaini ya hali hiyo kuboreka muda unavyokwenda.

Kwa mujibu wa Profesa Jayasena, ingawa kuongezeka kwa uelewa kuhusu uzazi wa wanaume ni jambo zuri, pia kumesababisha pengo la taarifa sahihi.

Kutokana na hali hiyo, wanaume wengi kama Jamal huomba ushauri kutoka kwa watu maarufu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuwasiliana na wataalam.