Je Makasisi wa Kanisa Katoliki wanaweza kuoa?... je Papa Francis alisemaje?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Pape Francis, kiongozi wa ngazi ya juu zaidi wa Kanisa la Kikristo la Katoliki alitoa kauli iliyoibua hisia . Kauli yake kuhusu wazo kwamba mapadre wa Kikatoliki wanaweza kuoa ilisababisha mjadala miongoni mwa Wakristo kote duniani .

Ni kwanini kuna mjadala mkubwa kuhusu maneno yake, ni kwanini Wachungaji wanaoa n ani kwanini inaruhusiwa? Kwanza Kabisa , tunahitaji kujua kuhusu Kanisa Katoliki

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Kanisa Katoliki la Roma

Kuna aina mabali mbali za Ukatoliki.

Wakatoliki ni wale wanaomtambua Papa katika Jiji la Vatcan kama kiongozi wa Wakristto duniani na kufuata nyayo zake. Kwao kanisa ni mfumo mkubwa sana. Wana mpangilio wa ngazi za uongozi wa Kanisa unaofahamika kuanzia makasisi au mapadre. Huu ni mfumo wa kanisa ambao umekuwa ukifuatwa kwa mamia ya miaka.

Kinyume na Waprotestanti ni wale wanaoendesha makanisa yao binafsi na wao huendesha makanisa yao kwa niaba ya wamishonari.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Mtu yeyote, mwenye umri wowote , anaweza kuanzisha kanisa. Yeyote anaweza kuwa mchungaji. Waprotestant wanaweza kuoa na kuwa na watoto.

Fungu la kumi hutolewa kwa ajili ya misaada miongoni mwa Waprotestanti, lakini hili halizingatiwi sana katika Ukatoliki.

Makanisa ya Kikatoliki yana mali ambazo huzalisha kipato na mishahara kwa ajili ya Mapadre.

Katika Ukatoliki kila kitu kuanzia ujenzi wa Kanisa hadi kuteuliwa kwa padre hufanyika chini ya uongozi. Wakatoliki humuita Baba na Kaka, huku Waprotestant wakimuita Mchungaji.

Makaka, Mapadre, katika makanisa ya Kikatoliki ni maseja. Hawapaswi kuoa na kuolewa na hawafai kuwa na watoto . Chaguo lao ni gumu. Yeyote anaweza kuwa kasisi katika Kanisa katoliki baada ya miaka 12 ya mafunzo ya shule.

Mwanaume anatakiwa kuwa muumini wa Kikatoliki walau kwa miaka 14 ili kukubaliwa kuwa kasisi. Wakiwa na umri wa miaka 13-14 hupelekwa katika shule inayoitwa Seminari .

Baada ya masomo ya mika 14 hadi 16 na kutimiza vigezo vyote vya kuwa mapadre hutawazwa kuwa mapadre. Hii itategemea utashi wake binafsi na iwapo viongozi wa kidini wanaona anafaa kuwa padre.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Useja – Makosa ya ngono

Kuna madai kuwa useja ndio sababu inayowafanya Wakatoliki wengi kutojiunga na upadre. Suala linguine muhimu ni kwamba baadhi ya viongozi wa kidini, ambao hawawezi kumudu useja, hutafuta mbinu nyingine za kukidhi haja zao za kingono, kufanya uhalifu wa kuficha makosa yao, na wakati mwingine hata kujiua.

Mara kwa mara katika habari tunasikia shutuma mbali mbali za kingono dhidi ya makasisi wa kikatoliki kutoka maeneo mbali mbali duniani na majibu ya Kanisa kuhusiana na shutuma hizo.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kauli za Papa Francis kuhusu useja iliibua mjadala miongoni mwa Wakristo wa kikatoliki

Je Papa Francis alisema nini?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Useja huenda usiwe utakatifu ," Papa francis mwenyewe alisema.

"Useja ni zawadi ya Mungu kwa viongozi wa kidini. Lakini hili lilikuwa ni la muda, hasa katika makanisa ya magharibu. Hakuna mahali ambapo mwalimu wa dini anapaswa kuoa. "Ni sheria ya muda katika makanisa ya Magharibi ," alisema Papa.

Alitoa kauli hizi katika mahojiano na shirika la habari la Argentina Infobay katika siku alipotimiza miaka kumi ya Upapa.

Kwa kawaida, kutunukiwa Upadre tukio takatifu katika Kanisa katoliki. Tukio hili huitwa kuwekwa wakfu.

"Useja huu sio wa kudumu kama kuwekwa wakfu," Papa alisema (Maana ni kwamba cheo cha kidini ni milele zaidi, lakini useja sio jambo la milele.)

Alitoa jibu la kufurahisha pale alipoulizwa iwapo kipengele cha useja kitarekebishwa "Ndio, Ndio. Watu wengi walioa katika Kanisa la Mashariki. Je walikuwa waseja kabla ya kuwekwa wakfu. Ndio. Watu wengi huoa katika Kanisa la Mashariki . Je wataoa? Kuna uwezekano wa kuchagua hilo," Papa alisema.

Alisema kuna Mapadre wa Kikatoliki ambao tayari wamekwishaoa na wana watoto. Alisema kuwa useja ni nidhamu tu

Je useja ni kwa ajili ya kutunza utajiri?

Kuna wale ambao wanadai kuwa kutunza mali ndii sababu ya useja kwa Mapadre wa Kanisa. Licha ya umuhimu wa kidini wa useja katika Ukristo, baadhi ya wanahistoria wanaamini kuwa mali ilikuwa ndio sababu kuu ya kuufanya useja kuwa sheria ya lazima.

Imekuwa takriban miaka maelfu tangu sheria ya useja iwekwe. Wanahistoria wengi wanasema kipengele hiki kilianzishwa katika karne ya 12. Inasemekana kuwa sheria hii iliwekwa kwa sababu hasa ya kulinda mali ya Kanisa.

Wanasema kimsingi ni kwamba kama padre wa Kanisa hana familia , mara moja mali inasalia ndani ya Kanisa