Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Sikuweza kusoma hadi miaka 18 – na sasa mimi ni profesa wa Chuo Kikuu cha Cambridge'
Mwanaume ambaye hakuweza kusoma wala kuandika hadi alipotimiza umri wa miaka 18 anakuwa profesa wa kwanza mweusi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufundisha katika chuo kikuu cha Uingereza cha Cambridge. Jason Arday alikuwa na ugonjwa wa usonji na kuchelewa kwa ujumla kujifunza mambo mbali mbali katika miaka yake ya mwanzo hadi alipofikia umri wa miaka 11 . Sasa akiwa na umri w amiaka 37 yuko tayari kuwa profesa wa elimu ya kijamii katika cho kiku cha kifahari.
Prof Arday aliiambia BBC kwamba anataka hususan kuboresha uwakilishaji wa jamii za walio wachachwe katika elimu ya juu