Vita Vya Ukraine: Mpiganaji atoa siri za yaliyotokea wakati wa uasi wa kikundi cha Wagner

Chanzo cha picha, BBC RUSSIAN SERVICE
Wiki tatu baada ya uasi wa muda mfupi wa Kikundi cha Wagner, bado kuna maswali zaidi kuliko majibu juu ya kile kilichotokea mnamo Juni 23-24, na ni nini mustakabali wa mamluki na kiongozi wao Yevgeny Prigozhin.
Wapiganaji wa Wagner mara chache huzungumza na vyombo vya habari, lakini BBC imefanikiwa kuwasiliana na kamanda kijana ambaye alikubali kueleza uzoefu wake lakini hakitaka kutotambulishwa.
Wakati Yevgeny Prigozhin alipeleka askari wake katika jiji la kusini la Urusi la Rostov mnamo Juni, Gleb - sio jina lake halisi - alijikuta katikati ya hatua hiyo.
Gleb ni kamanda kijana ambaye tayari alikuwa ameshiriki katika mashambulizi dhidi ya jiji kama hilo Bakhmut, mashariki mwa Ukraine.
Alikuwa amepumzika na kikosi chake katika kambi moja katika eneo linalokaliwa la Luhansk, walipopokea simu ya kujiunga na safu ya wapiganaji wa Wagner wanaoondoka Ukraine.
Simu hiyo, mapema asubuhi ya Juni 23, agizo ilitolewa na kamanda wa Wagner ambaye Gleb hataki kumtaja kwa sababu za usalama, lakini ambaye alikuwa akifanya kazi kwa maagizo kutoka juu kwa amri ya Prigozhin.
"Ni kupelekwa moja moja," aliambiwa. "Tunaunda safu, twende".
Gleb anasema kwamba walianza safasi. Wapiganaji hao wa Wagner hawakukutana na upinzani wowote, alisema, wakati walivuka mpaka wa Urusi hadi eneo la Rostov.
"Sikuona walinzi wowote wa mpaka," anakumbuka. “Lakini polisi wa usalama barabarani walitusalimia njia nzima.

Chanzo cha picha, WARGNER
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Akaunti za Telegram zinazohusishwa na kwa karibu na kundi la Wagner zilidai kwamba walinzi wa mpakani katika kituo cha ukaguzi cha "Bugayevka" waliweka silaha zao chini wakati wapiganaji wa Wagner walipofika.
Akaunti hizi zilisambaza picha inayodaiwa kupigwa katika eneo la tukio ikionyesha zaidi ya watu dazeni mbili wasio na silaha wakiwa wamevalia nguo za kijeshi.
Wakikaribia Rostov-on-Don, wapiganaji hao waliamriwa kuzunguka majengo yote ya serikali katika jiji hilo na kutka uwanja wa ndege wa kijeshi. Kitengo cha Gleb kiliamriwa kushikilia jengo la ofisi ya kikanda ya FSB (huduma ya siri ya Kirusi) Oblast, mkoa wa Rostov.
Walipokaribia jengo hilo, lilionekana kufungwa kabisa na lilikuwa tupu. Walirusha ndege isiyo na rubani juu ya jengo hilo ili kuangalia kama kuna dalili zozote za watu, na baada ya nusu saa mlango ulifunguliwa na watu wawili wakatoka nje.
Walisema, "Ndugu, tunaweza kukubaliana," anasema Gleb. Nikasema, "Kuna nini cha kufanya? Huu ni mji wetu."
"Kwa hiyo tulikubaliana. Wangetoka kwenda kuvuta sigara mara kwa mara."
Waandishi wa habari wa Rostov waliripoti suala hilo kuhusu kushikiliwa kwa majengo mengi ya serikali katika jiji hilo na mazingira yake. Hakuna mtu aliyeruhusiwa kutoka, lakini baadhi waliruhusiwa kuingia na chakula.
Hakuna maelezo
Wakati huo huo, kiongozi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin, alikuwa katika makao makuu ya Wilaya ya Kijeshi ya Kusini ya jeshi la Urusi na alikutana na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Luteni Jenerali Yunus-bek Yevkurov na Naibu Mkuu wa Wafanyakazi Mkuu Lt. Jenerali Vladimir Alexeyev.
Prigozhin alidai kwamba wawakabidhi Mkuu wa Wafanyakazi Mkuu, Valery Gerasimov, na Waziri wa Ulinzi, Sergei Shoigu.

Chanzo cha picha, BBC RUSSIAN SERVICE
Prigozhin alipokuwa katika mkutano huo, safu nyingine ya wapiganaji wa Wagner ilikuwa ikiendelea kusonga mbele.
Gleb anathibitisha ripoti za vyombo vya habari kwamba safu hii iliongozwa na mwanzilishi wa Wagner Dmitry Utkin, afisa wa zamani wa kikosi maalum ambaye ni nadra kuonekana hadharani.
Safu hii ilikuwa kwenye barabara kuu kuelekea Voronezh na, na Moscow, anasema Gleb.
Alipoulizwa ni kulikuwa na mpango gani wakati huo wa uasi,na nini Prigozhin alikusudia au alipanga kufanya, Gleb anajibu: "Hatukuwa na tunajua lolote."
"Tulijifunza na kujua kilichokuwa kikitokea kuupitia Telegram, kama wewe," anaongeza.
Siku ikiendelea, picha za kile kilichokuwa kikitokea Rostov zilitangazwa kote ulimwenguni. Watu walishangaa kuona wakazi na hata waandishi wa habari wa eneo hilo wakitabasamu na kupiga soga na baadhi ya wapiganaji wa Wagner wanaokalia mji wao, wakati kwa kawaida huwa na busara sana.
Kwa wapiganaji wenye uzoefu kama Gleb, ambao waliandikishwa muda mrefu kabla ya vita nchini Ukraine, sheria zinaeleweka vyema zaidi.
Gleb aliiambia BBC kwamba muda fulani awali walikuwa wameambiwa na makamanda wa juu kwamba mtu yeyote ambaye atazungumza na vyombo vya habari "atatengwa", yaani, atauawa. Maveterani kadhaa wa Wagner walituambia jambo ilo hilo pia.
Jioni ya Juni 24, mmoja wa wakuu wa Gleb aliwasiliana naye na kumwambia, bila maelezo yoyote, kwamba yeye na kitengo chake walipaswa kurudi kwenye kambi Luhansk.
Waliporudi kwenye ngome, walifuatilia habari kwenye Telegram.
Ni wakati huu walipojua kwamba kwamba kuna kesi za jinai zilikuwa zimefunguliwa dhidi ya Prigozhin, kisha kutelekezwa, na kwamba alipaswa kwenda uhamishoni huko Belarus.
Pia walisoma kwamba wapiganaji wa Wagner hawatawajibishwa kwa hatua yao ya kufanya uasi sababu ya "sifa zao za vita", zilizorejelewa na katibu wa waandishi wa habari wa Rais Putin, Dmitry Peskov.

Chanzo cha picha, BBC RUSSIAN SERVICE
Kwa Gleb na kikosi chake, mustakabali wa maisha yao sasa hauna uhakika. Waliamriwa kubaki katika kambi yao huko Luhansk na kungoja amri zaidi.
Wenyeji wao, mamlaka ya Jamhuri ya Watu wa Luhansk, wapiganaji wanaounga mkono Urusi wanaotaka kujitenga kutoka mashariki mwa Ukraine, wanataka kujua zaidi kuhusu mipango yao ya siku za usoni na nini kitatokea kwa vifaa na silaha zao.
Tulimuuliza Gleb kwa nini hakuondoka tu: "Mkataba wangu bado haujaisha," anajibu.
Kituo kinachofuata ni Belarus?
Tangu mwisho wa uasi wa Wagner, taarifa zimekuwa na mabadiliko mengi yasiyotarajiwa.
Ilibainika hivi majuzi kwamba siku tano tu baada ya ghasia hizo, Rais Putin alikutana na Prigozhin na makamanda wa juu 35 wa Wagner huko Kremlin.
Haijabainika hawa makamanda 35 walikuwa nani.
Makamanda wawili wa Wagner, wanaojulikana kama "Zombie" na "Lotus", mara nyingi hunukuliwa na waandishi wa habari wa Urusi wanaounga mkono vita.
Katika taarifa kwenye mitandao ya Telegraph iliyo karibu na kikundi cha Wagner, makamanda hawa wawili walieleza kuhusu mlolongo wa matukio.
"Sote tumepelekwa likizo hadi mwanzoni mwa Agosti," Lotus, jina halisi Anton Yelizarov alisema.
"Binafsi, imepita miaka mitano tangu niende likizo kukutana na familia yangu, na vijana wengine pia wamezama katika masuala ya familia sasa," alisema kupitia Telegram.
“Uamuzi uliochukuliwa na baraza la makamanda ni kumpa nafasi kila mmoja kupumzika kabla ya kazi kubwa iliyo mbele yetu.
Lotus anasema "kazi kubwa" hii inahusisha wapiganaji wa Wagner wanaozunguka kulingana na kile alichokiita "maeneo ya mbali". Yamkini alikuwa anarejelea maeneo kama Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako mamluki 600 wa Urusi waliripotiwa kurudishwa nyumbani hivi karibuni.
Hatua hiyo inafuatia malalamiko mengi kutoka kwa familia za wapiganaji wa Wagner, ambao wanasema wapendwa wao wamekwama katika nchi za Afrika kwa zaidi ya mwaka mmoja, licha ya kusaini kandarasi za miezi sita pekee.

Chanzo cha picha, BBC RUSSIAN SERVICE
Anton Yelizarov pia alizungumzia kuhusu Belarusi na mipango ya kuhamisha baadhi ya wapiganaji wa Wagner kwenda nchini humo.
"Jambo la pili na gumu zaidi ni kuingia Belarus," alisema. "Tunahitaji kuandaa misingi, misingi ya mafunzo, kuratibu pamoa na tawala za mitaa na mashirika binafsi, kuandaa ushirikiano na vikosi vya usalama vya Belarusi na vitu vingine.
Kamanda wa pili, "Zombie", pia alizungumza kupitia Telegraph juu ya mustakabali wa Wagner.
"Hatujaunganishwa tu na mkataba, lakini pia na wazo moja, la kupigana," alisema. "Hatutaki tu kutumikia kifungo chetu, lakini kuwa na manufaa kwa nchi," Zombie aliendelea.
Mtangazaji wa Runinga ya Urusi na mtangazaji wa propaganda Vladimir Solovyev alimtambua "Zombie" kama mpiganaji wa zamani wa kikosi maalum anayeitwa Boris.
"Wengi wanatuchukulia kama mamluki, lakini hiyo si kweli. Tuna uzalendo zaidi kuliko wengine," Zombie alisema. "Tunapigana bila kujitolea maisha yetu. Na kiongozi anatuunganisha, kama misheni ya pamoja," anaeleza.
"Zombie" aliulizwa ikiwa yeye na wenzake watafikiria kujiunga na jeshi la kawaida, kama ilivyopendekezwa na Rais Putin.
"Nitakuwa na wapiganaji wangu katika Kampuni ya Kijeshi ya Wagner au kupumzika nyumbani kutazama TV," alijibu. "Na hivyo ndivyo kila mtu anavyofikiri.
BBC iliuliza swali kama hilo kwa Gleb, ambaye sasa yuko Luhansk na kikosi chake. Anadai hamjui hata mtu mmoja ambaye amesaini mkataba na Wizara ya Ulinzi hadi sasa.












