Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 18.04.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona na Manchester City wamefanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa kati wa RB Leipzig na Uhispania Dani Olmo, 25, wiki iliyopita. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)
Chelsea na Barcelona ni miongoni mwa klabu kadhaa za Ulaya zinazofikiria kumnunua mshambuliaji wa Roma mwenye umri wa miaka 30 kutoka Argentina Paulo Dybala. (Rudy Galetti)
Beki wa zamani wa Mexico Rafa Marquez ni mmoja wa wanaowania kurithi mikoba ya Xavi wakati Mhispania huyo atakapojiuzulu kama kocha wa Barcelona mwishoni mwa msimu huu. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich na Tottenham wameungana na Manchester United katika kufikiria kumnunua beki wa Everton mwenye umri wa miaka 21 Muingereza Jarrad Branthwaite. (TeamTalks)
Klabu za Saudi Pro League zinavutiwa na kiungo wa kati wa Senegal Idrissa Gana Gueye, 34, ambaye huenda asipewe ofa mpya na Everton mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)
Newcastle na Liverpool zimeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ivory Coast Ousmane Diomande, ambaye pia anasakwa na Chelsea. (Football Transfers)

Chanzo cha picha, Reuters
Newcastle imetuma maskauti kuwatazama kiungo wa Boca Juniors Muargentina Kevin Zenon, 23, na mlinzi wa Argentina Nicolas Valentini, 23. (HITC)
Kazi ya Sean Dyche kama meneja wa Everton haiko hatarini licha ya matokeo mabaya ya klabu hiyo. (News – Subscription Required)
Nottingham Forest wanataka zaidi ya pauni milioni 20 kumnunua beki wa kati wa Brazil Murillo, 21, huku Liverpool, Chelsea, Manchester United na Paris St-Germain pia zikimnyatia . (Football Insider)
Manchester United wanaweza kumuuza Mason Greenwood kama sehemu ya mpango wa kumsajili beki wa Brazil Gleison Bremer, 27, kutoka Juventus. (Gazzetta dello Sport – In Italy , Subscription Required)
Imetafsiriwa na Abdalla Seif Dzungu












