Ukraine inaweza kujiunga na EU?

Iliyochapishwa

Ukraine iko tayari kuwa muombaji rasmi wa uanachama wa Muungano wa Ulaya (EU), ikiwa ni hatua ya kwanza ya kujiunga na muungano huo wenye nchi 27.

Viongozi wa EU wanatarajiwa kuunga mkono hatua hiyo katika mkutano unaofanyika tarehe 23 ma 24 Juni. Rais wa Ukraine ameonya kuwa Urusi inaweza kuongeza mashambulio yake ya kulipiza kisasi.

EU ni nini?

Muungano wa Ulaya (EU) ni muungano wa kiuchumi na kisiasa baina ya nchi 27 za Ulaya, ambao ulibuniwa baada ya Vita Kuu vya Pili vya Dunia. Bidhaa , husuma na pesa hutumiwa kwa uhusu baina ya mataifa wanachama wa EU. Wananchi wa EU wanaweza kuishi na kufanya kazi popote miongoni mwa nchi wanachama wa muungano huo.

Hutumia sarafu moja, ya Euro ambayo inatumiwa na zaidi ya watu milioni 340 katika nchi 19 kati ya 27 wanachama wa EU.

Viwango vya kawaida vinatumiwa kote katika nchi wanachama katika maeneo kadhaa mkiwemo usalama wa chakula, kilimo na haki za kuajiriwa. EU pia husaidia maeneo ya Ulaya masikini zaidi kuimarisha chumi zao.

Kwanini Ukraine inataka kujiunga?

Rais Volodymyr Zelensky alianza kuwasilisha maombi ya uanachama wa EU siku tano baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine Februari 2022. Aliomba kuweza kujiunga mara moja , lakini mchakato unaweza kuchukua miaka.

Kutakuwa na faida za kifedha kujiunga na EU. Lakini sababu kuu ya Ukraine sio ya kiuchumi, anadai Dr Zach Paikin kutoka kituo cha wasomi wa stadi za ya Ulaya- Centre of European Policy Studies , mjini Brussels.

"Uanachama wa EU wa Ukraine utaifanya Ukraine kuwa taifa huru kamili , lenye kujitawala ," anasema. "Sio sehemu ya ulimwengu wa Urusi."

Nchi hujiunga vipi na EU?

Kwanza kabisa, Tume ya Ulaya, huduma za raia za EU, hutathmini iwapo nchi ni muombaji anayefaa kujiunga na muungano. Huangalia iwapo imeimarika, kidemokrasia, kuheshimu haki za binadamu, na ina uchumi wa soko huru.

Wanachama wote wa muungano wa EU wanapaswa kukubali kabla ya nchi mpya kuweza kuwa muombaji rasmi.

Iwapo itafanikiwa, nchi itatakiwa kutumia sheria na kanuni zote za EU. Hii kwa kawaida huchukua miaka kadhaa.

Hatimaye, nchi husaini mkataba wa kujiunga ambao umeidhinishwa na nchi nyingine za EU.

Inachukua muda gani kujiunga na EU?

Kwa nchi zilizojiunga hivi karibuni Bulgaria, Romania na and Croatia, mchakato mzima ulichukua kati ya miaka 10 na 12.

Albania, North Macedonia, Montenegro na and Serbia zimekuwa waombaji rasmi kwa miaka kadhaa, lakini maombi yao yamekwama.

Uturuki ilikuwa muombaji rasmi mwaka 1999. Hatahivyo, maombi ya kukubaliwa yalisitishwa kutokana na hofu kuhusu rekodi ya nchi ya haki za binadamu.

Jirani wa Ukraine, Moldova, ilikubaliwa kama muombaji katika siku moja sawa na Ukraine. Georgia imeomba uanachama, lakini iliambiwa ni lazima ifanye mageuzi.

Ni mahusiano yapi iliyonayo Ukraine na EU?

Tangu mwaka 2017, Ukraine imeweza kufanya biashara na mataifa ya EUbila kulipa ushuru, chini ya kile kinachoitwa makubaliano ya muungano.

Nchi hiyo ilikuwa tayari imelipa ushuru nafuu baada ya kujiunga na eneo la biashara huru la EU katika mwaka 2016.

Kama sehemu ya maandalizi yake ya kuw mwanachama, Ukraine tayari imekwishabadilisha sheria zake nyingi na taratibu kukidhi viwango vya EU.

Ni nini kingine Ukraine itahitaji kukifanya?

Rais wa Tume ya Muungano wa Ulaya Ursula von der Leyen anasema "kazi nzuri imekwisha fanyika", lakini kwamba Ukraine lazima ifanye ''mageuzi muhimu'' zaidi.

Hii inajumuisha kuimarisha utawala wa sheria, kuboresha hakiza binadamu, kupunguza mamlaka ya mabwanyenye, na kushughulikia ufisadi. "Pia kuna haja ya Ukraine kujenga biashara huria kikamilifu," anasema mtafiti Zach Paikin, "jambo ambalo ni gumu kwa Jamhuri ya baada ya Usoviti ." Changamoto nyingine itakuwa ni kusafisha mfumo wa mahakama wa Ukraine, ambao umekuwa ukikosolewa kwa sana.

Wanachama wa EU huwasaidia vipi wanachama wapya?

Tangu ilipojiunga miaka 15 , iliyopita pato la ndani ya nchi la Romania limeongezeka mara tatuna la Burgaria limeongezeka mara dufu. EU imetoa mabilioni ya euro kwa nchi zote kupitia Mfuko wa Muundo na uwekezaji wa Ulaya. Fedha hizi husaidia maendeleo ya kiuchumi kwa mfano kwa ujenzi wa barabara na bandari.

Kati ya mwaka 2014 na 2020, Bulgaria ilipokea euro bilioni 11.2 na Romania euro bilioni 35.

Hatahivyo, Transparency International inadai pesa nyingi zimepotea kupitia ufisadi.

Bulgaria imesalia kuwa nchi ya mwisho miongoni mwa wanachama wa EU kwa utoaji wa mishahara ya chini, afya na elimu, lakini Romania imepanda kutoka nchi ya pili masikini zaidi hadi kuwa nchi ya sita kwa umasikini zaidi.

Waburgaria wapatao milioni 1.5 na Waromania milioni 4 wametumia sera ya EU ya "uhuru wa matembezi" kusafiri nje ya nchi, kulingana na Benki ya Dunia. Wakosoaji wanahofia "kuchukuliwa kwa watu wenye akili" kunaweza kuharibu malengo ya nchi zote mbili.

Urusi imesemaje kuhusu matarajio ya uanachama wa EU wa Ukraine?

Ingawa Rais Vladimir Putin amekuwa mkosoaji wa muda mrefu wa nia ya Ukraine ya kujiunga na Muungano wa kijeshi wa Nato , anasisitiza hana chochote dhidi ya " Ukraine kuwa mwanachama wa EU.

Hatahivyo msemaji wake, Dmitry Peskov, anasema Kremlin inaona kuipatia uanachama Ukraine "kutaongeza wasi wasi " kwasababu EU inaangalia uwezekano wa kuunda kikosi chake cha ulinzi.

"Jeshi , ulinzi na uslama ni mambo yanayojadiliwa," alisema Bw Peskov. "Bila shaka tunaliangalia kwa kina." Rais wa Ukraine Zelensky ameonya kwamba Urusi inawea kulipiza kisasi dhidi ya hatua ya kujiunga kwake na EU.

"Bila shaka, lazima tutarajie uhasama mkubwa zaidi kutoka Urusi," alisema. "Na sio tu dhidi ya Ukraine, bali pia dhidi ya nchi nyingine za Ulaya''