Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Kenya 2022: Wakazi wa pwani kumpigia kura atakayetatua suala la ardhi
Wakati Kenya ikielekea katika uchaguzi mkuu mnamo mwezi Agosti mwaka huu, baadhi ya wananchi kutoka eneo la Pwani ya nchi hiyo, wanasema mpaka sasa hawajajua nani wa kumpigia kura, kutokana na serikali zilizopo madarakani kushindwa kuwatatulia baadhi ya changamoto walizonazo ikiwemo ile ya ardhi.
Kwa miongo kadhaa, baadhi ya wakazi wa maeneo ya pwani ya nchi hiyo kama vile Jomvu, Kisauni, Bombolulu wanadai kushindwa kuendeleza ardhi wanazokalia kutokana na migogoro iliyopo.
Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau ametembelea eneo la Kwa Bullo huko Bombolulu na kukutana na baadhi ya familia zinazopitia masaibu hayo.