Kwanini kukaa kwa muda mrefu ni hatari kwa maisha yako

Chanzo cha picha, TO BREAK
Ulimwengu tunaoishi sasa sio mkubwa kama ilivyokuwa zamani. Zamani watu walikuwa wakitembea, kwenda sokoni, kulima, kuwinda, na kusafiri.
Ulimwengu wa kisasa unahimiza kukaa sana, iwe watu wanataka au la.
Watu wengi hutumia saa nyingi kwenye gari, shuleni, ofisini, nyumbani hasa tunapotazama TV.
Wanasayansi na wataalamu wa matibabu wameonyesha kuwa kukaa sana kunaweza kusababisha hali nyingi mbaya za afya ambazo zinaweza kukudhoofisha.
Baadhi ya magonjwa na hali ya kiafya ambayo kukaa sana kunaweza kusababisha ni pamoja na: Kisukari, magonjwa ya moyo, baadhi ya saratani, unene (unaosababisha magonjwa mengine mengi) na kifo.
Dk Emma Wilmot alithibitisha hilo huku akieleza kuwa utafiti wao ulionyesha kuwa watu wanaokaa chini kwa muda mrefu mara nyingi hupata magonjwa hayo.
Ukweli ni kwamba imefanyiwa utafiti kuwa kukaa muda mrefu huathiri utengenezwaji wa nishati katika mwili wa binadamu iitwayo ‘Glucose’ pamoja na kitu kiitwacho ‘insulini’ ambacho ndicho husaidia Glucose kuwa kwenye damu ya binadamu kwani inapaswa kuwa..

Chanzo cha picha, TO BREAK
Mtaalamu mwingine Dk.Udodi Okoli naye alisema “kukaa kwa muda mrefu kunaweza kuleta matatizo kwenye mgongo wa mtu hasa mtu asipokaa vizuri au hatumia kiti kilichotengenezwa kwa ajili ya kukaa vizuri”
Alieleza kuwa mtu akikaa kwa muda mrefu mbele ya kompyuta yake na asiweke kichwa au shingo yake kwa njia ifaayo, shingo inaweza kuanza kuwa na maumivu.
Okoli alisema kuwa kujaribu kusimama na kutembea kunaweza kusaidia kupunguza hali hizi.
Pia alisema kutofanya mazoezi ya viungo kunaweza kufanya roho yake kushuka au kuathiri afya yake ya akili kwa njia mbaya.
Jinsi ya kujisaidia

Chanzo cha picha, TO BREAK
Kubadilisha tabia sio jambo rahisi lakini inawezekana ikiwa mtu anaweza kuchukua uamuzi sahihi.
Baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia kupunguza muda unaotumia kukaa ni pamoja na:
- Jaribu kuweka kikumbusho kwenye simu yako au uandike kwenye kipande cha karatasi karibu nawe unapoinuka kutoka kwenye kiti chako kila mara, kila siku.
- Ukiweza, simama unapofanya kazi yako, ikijumuisha wakati wa mikutano ofisini kwako (Unaweza kuweka kompyuta yako mezani na kusimama kufanya kazi yako.)
- Anza kunywa maji au chai mara kwa mara - hii ni bora ikiwa mtoaji wa maji katika ofisi yako hayuko karibu nawe.
- Pia kumbuka kuwa maji ya kunywa yatakufanya ukojoe jambo ambalo litakufanya unyanyuke kwenye kiti chako.
- Punguza muda unaotumika kutazama TV
- Jaribu kuanza kufanya mazoezi kila siku - hata ikiwa ni kutembea, kuruka kamba, kukimbia, kuendesha baiskeli, kunyanyua vyuma au kitu kingine ambacho unafurahia kufanya.












