Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 19.02.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Kylian Mbappe alifanya mazungumzo na Manchester City siku moja kabla ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 kutangaza kuwa anaondoka Paris St-Germain mwishoni mwa msimu. (Cadena Ser – In Spanish)
Mkurugenzi wa michezo wa Newcastle Dan Ashworth amewekwa kwenye likizo baada ya kuomba kuondoka klabuni hapo huku Manchester United ikiwa na nia ya kumsajili. (Subscription Required)
Manchester United lazima walipe fidia kubwa ikiwa wanataka kumteua Ashworth, au wamsubiri kutumikia miaka miwili ya likizo yake iliyoandikwa katika mkataba wake wa Newcastle. (Mail)

Chanzo cha picha, getty Images
Chelsea wanafuatilia hali ya Harry Kane katika klabu ya Bayern Munich huku kukiwa na ripoti kwamba mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30 hana furaha kabisa nchini Ujerumani. (Football Insider)
Liverpool wanatumai kumnasa meneja wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Simon Rolfes kuchukua nafasi za Jurgen Klopp na Jorg Schmadtke wanaoondoka msimu huu. (Football Insider)
Tottenham wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Everton Mwingereza James Garner mwenye umri wa miaka 22 msimu wa joto. (TeamTalks)

Chanzo cha picha, Reuters
Oliver Glasner amekubali mkataba wa miaka miwili na nusu kumrithi Roy Hodgson kama meneja wa Crystal Palace. (Sky Sports)
Arsenal ilimchunguza kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg Oscar Gloukh siku ya Jumamosi wakati wanafikiria mbinu ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Israel, 19. (Football Transfers)
Meneja wa zamani wa Wales Chris Coleman ameibuka kuwania nafasi ya kuinoa Jamhuri ya Ireland baada ya mazungumzo na meneja wa timu ya vijana ya chini ya miaka 21 ya Uingereza Lee Carsley kukwama. (Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Bayern Munich Thomas Tuchel hatatimuliwa licha ya timu hiyo ya Bundesliga kupata kipigo cha tatu ndani ya siku tisa dhidi ya Bochum Jumapili. (Sky Germany)
Rais wa Barcelona Joan Laporta ameomba ripoti zaidi za uchunguzi kuhusu Roberto de Zerbi anapofikiria kumkaribia bosi wa Brighton ili kumrithi Xavi kama meneja mwishoni mwa msimu huu. (Sport – In Spanish)
Beki wa Birmingham wa Jamhuri ya Ireland, Kevin Long, 33, anakaribia kukamilisha uhamisho wa kwenda Toronto FC ya MLS. ( Birmingham mail )












